Katika mkutano huu kamtuma tena Makamu wa Rais, Mhe. Suluhu. Hata hivyo, sioni tatizo kwa yeye kutokwenda kwa sababu mikutano hii haina tija yoyote. Kwa wakati huu kipaumbele ni kuipanga safu yake ya uongozi na kuweka nidhamu inayotakiwa. Kama kiongozi lazima uwe na vipaumbele huwezi kuvamia kila kitu. Tunazo changamoto lukuki kama taifa, hivyo ni jambo jema kutumia muda mwingi na juhudi kubwa zaidi kwa kuzielelekeza huko. Kutuma wasaidizi wake bado ni jambo zuri kwani hata Makamu wa Rais anahitaji uelewa na weledi katika diplomasia na ushirikiano wa kimataifa. Hivyo, kutokana na uzito wamaujukumu ya kitaifa, naamini na ninaheshimu maamuzi yake kuwa ni vyema akawapa fursa wasaidizi wake nao wakajiimarisha kiweledi. Endapo asingetuma hata mwakilishi, ambaye ni kiongozi wa ngazi ya juu, hilo lingenipa maswali. Ila kwa sasa tumpe nafasi ya kuwatumikia watanzania kwa kasi. HAPA KAZI TU!