Magufuli kumfilisi Lowassa

Inaonekana Magufuli ana furaha kutuona watanzania wote makapuku.Yaani ana mawazo ya kimaskini
 
Yeye na wenzake mafisadi watafilisiwa. Magufuli yupo siliace na kazi yake.

Hebu niulizie kwa magufuli hapo lini atarudisha hela zetu alizonunulia kivuko chakavu? Lini atarudisha hasara aliyosababishia serikali kwa kukurupuka kukamata meli yenye vibali vya kimataifa vya uvuvi? Ukiona kama anapata kigugumizi hebu mwulize mbona barabara zake ziko chini ya kiwango? Mathalan toka chato kwenda bukoba viraka ndio vimejaa barabaran?
 
Anamfilisi vipi? Huu ni upu mbavu wa migazeti ya kijingakijinga,,watu wanafilisiwa hivyo ? Hizo ni kelele tu na ujinga ulowajaa hawa watu wasiojua wafanyacho.
 

Wewe umetumwa,utendaji wa Magufuli sio wenye kupoteza kumbukumbu kama mzee wenu.
 
Diamonda hana mvuto tena baada ya kupuuzwa na wananchi.... Kwa sasa CCM wana mpango wa kupiga chini wasanii 34 kati ya wale 56 ili fedha hizo wampatie Chamelion apige show kanda ya ziwa....

Hakuna kitu kama hicho. Magufuli ni maarufu huko kuliko unavyodhani, waulize kina wenje watakujulisha. Mtu anapotea jukwaa, muda wote anaongozwa tena kwa kushikwa mkono, unategemea nani atamuamini? Nyinyi ni wakatili sana. Mnamkomalia tu Mzee wa watu Mkimpamba ili tu ajisikie yuko timamu kwa matarajio kuwa mtachukua nchi wakati mnaju kabisa hali yake. Kwanini msimpe break ya hata siku 5 tu?
 

Hahahahaha eti Magufuli ni maarufu.... Hahahaha, haya ngoja nikuache.... Ila kama unataka kujua ulisemalo ebu tembelea hapa Sumve afu utake jina la Magufuli kama wanamjua.... Hahahahaha endeleeni kumdanganya...

Anapozomewa kama jana Mbeya ndio nafkiri anaanza kupata akili kuwa hali ni ngumu...
 
Wewe umetumwa,utendaji wa Magufuli sio wenye kupoteza kumbukumbu kama mzee wenu.

Unafikiri halijui hilo? Anajitoa ufahamu kwa sababu hamna namna.Huwezi kumuunga mkono mtu asie na sababu ya kukushawishi umuunge mkono zaidi ya kisingizio cha kuleta mabadiliko bila kukueleza atayaleta vipi bila kujitoa ufahamu kwanza. Hana historia yoyote ya kiutendaji iliyotukuka, haongei chochote, ana historia ya wizi, amesababisha mauaji ya watu kwa migogoro ya wafugaji na wakulima, ni mdini na mkanda halafu bado tu unakomaa kuwa anafaa kuongoza.
 
Mods huu uzi mbona hamja ihamishia jukwaa la uchaguzi kama thread zingine?... Au kwa kuwa linasapoti CCM?
 
Anamfilisi vipi? Huu ni upu mbavu wa migazeti ya kijingakijinga,,watu wanafilisiwa hivyo ? Hizo ni kelele tu na ujinga ulowajaa hawa watu wasiojua wafanyacho.
Hivi unajua matumizi ya kampeni yalivyo? Sasa linganisha na matumzi ya kampeni ya Lowassa mwanzoni wakati anaanza. Si lazima utujibu,katulie utafakari.
 

Wuh, thank God kwa kukunyima jicho la ndani, uko sahihi sana unavyoamini, usije ukadanganyika kusikiliza propaganda tofauti na za chama kikuu
 
moja ya ujinga mkubwa ambao elimu ya tz imeshindwa kuuta ni ile hali ya kuaminishwa uongo kuwa ndo ukwelu na watu wakashangilia nankukubali
 

Sikusema hakuna wasiomuunga mkono. Kanda ya ziwa anapendwa sana. Migodi zaidi ya 25 iliyokuwa imechukuliwa imerudishwa kwa wananchi katika awamu hii, ameahidi kuirudisha zaidi na kuwapa wachimbaji wadogo teknolojia ya kuwasaidia katika uchimbaji. Kwetu tunaoujua uchimbaji wa madini hilo ni jambo kubwa kwa mchimbaji wa dhahabu. Ina maana watapata mpaka concentration equipment ambazo unaenda kuipata gold ikiwa nyingi na ikiwa na impurities chache sana baada ya kuprocess ore nyingi tofauti na kutumia karai. Unategema watataka kipi tena?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…