Kwanini Mungu ahitaji sadaka ya masikini?

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,140
Reaction score
138,239
Sipo hapa kuleta ligi. Mimi ni mkristo, kuwa mkristo haimaanishi hutakiwi kunifunza au kuuliza. Nauliza nijue ili kuamini zaidi badala ya kuamini juu juu tu.

Sihitaji kujua HOW(jinsi gani) hayo nayajua
Sihitaji kujua references (vyanzo), hivyo navijua. Labda viwe vyanzo vinavyoeleza sababu

Nahitaji kujua sababu, sababu ya Mungu kuhitaji sadaka kutoka kwa masikini. Si masikini hana uwezo anaunga-unga kujikimu? Kwa nini asipokee badala ya kutoa?
 
Siko hapa kuleta ligi. Mimi ni mkristo, kuwa mkristo haimaanishi hutakiwi kunifunza au kuuliza. Nauliza nijue ili kuamini zaidi badala ya kuamini juu juu tu.

Sihitaji kujua HOW(jinsi gani) hayo nayajua
Sihitaji kujua references (vyanzo), hivyo navijua. Labda viwe vyanzo vinavyoeleza sababu

Nahitaji kujua sababu, sababu ya Mungu kuhitaji sadaka kutoka kwa masikini. Si masikini hana uwezo anaunga-unga kujikimu? Kwa nini asipokee badala ya kutoa?
Kwanini Mungu anahitaji sadaka?Iwe ya masikini au tajiri?
 
Sipo hapa kuleta ligi. Mimi ni mkristo, kuwa mkristo haimaanishi hutakiwi kunifunza au kuuliza. Nauliza nijue ili kuamini zaidi badala ya kuamini juu juu tu.

Sihitaji kujua HOW(jinsi gani) hayo nayajua
Sihitaji kujua references (vyanzo), hivyo navijua. Labda viwe vyanzo vinavyoeleza sababu

Nahitaji kujua sababu, sababu ya Mungu kuhitaji sadaka kutoka kwa masikini. Si masikini hana uwezo anaunga-unga kujikimu? Kwa nini asipokee badala ya kutoa?

Kwenye suala la sadaka kila mtu hutoa kulingana na alivyokirimiwa...

Hivyo kiwango cha sadaka cha mtu masikini bila shaka tunategemea kitaendana na alichonacho...

Fahamu ya kwamba, sadaka si lazima iwe ni fedha au mali, sadaka inaweza ikawa hata muda, nafasi, mwili wako mwenyewe n.k...mathalani kutazama wagonjwa, kutembelea yatima, kujitoa kama mtenda kazi kwenye nyumba za ibada n.k vyote hivi ni sadaka pia...
 
Sadaka sio kwenda kwa Mungu moja kwa moja ila ni suala la kiroho , sadaka kuna makundi maalumu wanapelekewa kama sehemu ya ibada . Kufanikisha mambo kadhaa ya kiibada(Kuwazesha hata wanaohusika au kujitolea kwenye mambo ya ibada) , sadaka sio pesa ni neno pana sana ...Zaka ni kwa matajiri tu kwa vile kuna kiwango .

Kuna makundi mengi tu ambayo sadka inapelekwa , hata ukitoa mia fresh .. Haina kiwango ila sio kwamba anapewa Mungu ila kutoa kuwezesha wengine kama mafukara , mayatima , watu waliopata majanga , wakimbizi(walioathirika na vita) ,na wenye mahitaji maalumu.

Ni vile kila kona kuna mafisadi , walengwa hawafikiwi zaidi ya kuneemesha watu wachache .​
 
Maskini anatoa sadaka ili iweje,alafu wakati huohuo tajiri anaambiwa awasaidie maskini. Inamaana msaada anaopewa masikini anatakiwa pia akautoe sadaka. Na mbaya zaidi Biblia hiyohiyo inazungumza kuwa mwenye nacho huongezewa na asiyekuwa nacho hata hicho kidogo alichonacho hunyang'anywa. tukihoji wanasema Mungu hachunguziki. how come?
 
Sipo hapa kuleta ligi. Mimi ni mkristo, kuwa mkristo haimaanishi hutakiwi kunifunza au kuuliza. Nauliza nijue ili kuamini zaidi badala ya kuamini juu juu tu.

Sihitaji kujua HOW(jinsi gani) hayo nayajua
Sihitaji kujua references (vyanzo), hivyo navijua. Labda viwe vyanzo vinavyoeleza sababu

Nahitaji kujua sababu, sababu ya Mungu kuhitaji sadaka kutoka kwa masikini. Si masikini hana uwezo anaunga-unga kujikimu? Kwa nini asipokee badala ya kutoa?

Umelijenga swali lako katika msingi potofu.

Ni wapi ambapo Mungu amesema anahitaji sadaka ya maskini au ya tajiri?

Hivi unajua sadaka inatolewa kwaajili ya nini?

Yafahamu yafuatayo, hutauliza swali kama hilo tena:
Katika agano la kale, kulikuwa na sadaka za aina nyingi. Ni Walawi pekee ndio waliokuwa wameruhusiwa kula sadaka. Walawi ambao ni descendants wa Lawi, mtoto wa Yakobo, wao ndio waliokuwa wakitoa makuhani. Sadaka haiendi kwa Mungu bali inabarikiwa na Mungu kwaajili ya matumizi ya watumishi wake, ambao hawafanyi kazi ya kujitafutia kipato, bali wameyatoa maisha yao kwaajili ya kumtumikia Mungu.

Hata katika agano jipya, sadaka ndiyo zilizokuwa zikitumika na mitume katika kazi zao za kueneza ujumbe wa Kristo. Kuna wakati, sadaka hizo hizo zilitumika kuwasaidia watu maskini na wale waliokuwa katika dhiki.

Kwa hiyo, swali lako umelitengeneza katika msingi usio sahihi.

Ufahamu tu kuwa kila muumini anastahili kutoa sadaka yake kwa kadiri alivyojaliwa, kwa kadiri ya wema wake, na kwa kadiri ya nia yake. Kiimani, kila sadaka unayoitoa inatakiwa kwenda sambamba na nia yako. Sadaka haitolewi kama mchango.

Sadaka ni kwaajili ya kuhani, mapadre/wachungaji.

Zaka ni kwaajili ya maendeleo ya Kanisa.
 
Maskini anatoa sadaka ili iweje,alafu wakati huohuo tajiri anaambiwa awasaidie maskini. Inamaana msaada anaopewa masikini anatakiwa pia akautoe sadaka. Na mbaya zaidi Biblia hiyohiyo inazungumza kuwa mwenye nacho huongezewa na asiyekuwa nacho hata hicho kidogo alichonacho hunyang'anywa. tukihoji wanasema Mungu hachunguziki. how come?
Maskini anajiweza angalau labda useme ufakara .. Nahisi hata hekima za waswahili huzijui , ni hivi hata kama uwe tajiri unamsaidia maskini labda kumpa chakula , kuna siku unatakiwa nawe uende kuomba kwake hata fundo la chumvi yaani kidogo , naye atoe ili asifikirie kuhusu mnyonge .

Masikini anaweza kutoa hata shilingi 100 katika utafutaji wake na tajiri akatoa laki na zaidi , sadaka sio lazima kwamba unakamulia ni binadamu tu waliweka ..Kuna zaka ambayo inahusu matajiri pekee , hiyo ni lazima .
 
Mwamposlisaaa” ukitoa sadaka unaombewa upate gari, unapewa mafuta sasa kwa nn? Usitoe sadaka

Na kwani maskini anatoa sadaka asilimia ngapi? Ya alichonacho na hizo sadaka zinafanyiwa nn? Na nan?

Et..
 
Mungu anahitaji kusujudiwa. Ile sadaka ni njia ya kunyenyekea, unaonesha umemtanguliza yeye kwanza.

Watu wakishaamini kwenye ule uzima wa milele unaosadikika basi watafanya lolote kuupata.
 
Sipo hapa kuleta ligi. Mimi ni mkristo, kuwa mkristo haimaanishi hutakiwi kunifunza au kuuliza. Nauliza nijue ili kuamini zaidi badala ya kuamini juu juu tu.

Sihitaji kujua HOW(jinsi gani) hayo nayajua
Sihitaji kujua references (vyanzo), hivyo navijua. Labda viwe vyanzo vinavyoeleza sababu

Nahitaji kujua sababu, sababu ya Mungu kuhitaji sadaka kutoka kwa masikini. Si masikini hana uwezo anaunga-unga kujikimu? Kwa nini asipokee badala ya kutoa?
Hata mimi najiuliza kwanini serikali inahitaji kodi zetu wakati yenyewe inamiliki kila kitu.
 
Sadaka haina umuhimu kuitoa kanisani au msikitini sadaka itoe kwa mtu mwenye shida moja kwa moja na wewe utaongezewa maradufu.
 
Maskini anatoa sadaka ili iweje,alafu wakati huohuo tajiri anaambiwa awasaidie maskini. Inamaana msaada anaopewa masikini anatakiwa pia akautoe sadaka. Na mbaya zaidi Biblia hiyohiyo inazungumza kuwa mwenye nacho huongezewa na asiyekuwa nacho hata hicho kidogo alichonacho hunyang'anywa. tukihoji wanasema Mungu hachunguziki. how come?
😄😄😄🙌
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom