Wanabodi,
Naomba kuanza na angalizo, kuna watu humu wana allergy Magufuli akipongezwa, hivyo utawasikia kuwa huku ni kuusaka UDC mara njaa!. Naomba kusisitiza kuwa mimi sina chama, kwenye mazuri tupongeze, kwenye mabaya tukosoe.
As days go by, this man is getting, better and better, he is changing for the better!.
Leo nimemsikiliza rais Magufuli akihutubia kutokea Ukerewe, kiukweli kabisa, nimekuwa very impressed!, haswa alipozungumzia maendeleo hayana vyama, akampongeza mbunge wa Ukerewe ambaye ni wa Chadema, na akatoa fursa kwa wana CCM wanaotaka kwenda upinzani, hakutokea mtu, akasema nikiuliza wapinzani wanaotaka kujiunga CCM, wengi watakuja, lakini siulizi kwa sababu huu sio mkutano wa CCM ni mkutano wa serikali!. This is good!.
Big up kwa rais wetu Magufuli kuanza kutenganisha shughuli za kiserikali na shughuli za chama. Kama tulimlaumu rais Magufuli kutumia state platforms kufanya siasa za CCM ikiwemo kupokea wanachama wapya, na leo amesema wazi, hatumii mikutano ya kiserikali kuigeuza ya CCM, ni jambo jema.
Sisi jf japo tunalaumiwa na kulaaniwa kwa ukosoaji kwa rais Magufuli na Serikali yake kila inapoboronga, lakini kiukweli kabisa, wanaomkosoa rais Magufuli ndio wanaomsaidia zaidi kubadilika, changing for the better, kuliko wanaomsifia!.
Naamimi lile tukio la kupokea wanachama pale uwanja wa Sheikh Amri Abed, wakati wa kamisheni maofisa wapya wa jeshi, ni sisi JF pekee ndio tulikipinga, na leo kimezaa matunda.
Nimenote kupungua kwa vikao vya CCM kwenye ikulu yetu, sasa vikao vya CCM, vinafanyikia CCM Lumumba!.
Huwezi kujua, huenda hata ule uvunjaji wa katiba kuzuia mikutano ya siasa, soon utasitishwa only if atabaini, it was not right, kwa sababu rais wetu hana mamlaka hayo aliodhani anayo!.
Mnaweza msiamini, anaweza kuamua kuifumua Tume ya Uchaguzi NEC na kuunda tume huru zaidi ambayo ni inclusive!, kama ameweza kumchukua Prof. Kitila, na yule mama wa ACT, atashindwa nini kuifumua NEC ili uchaguzi wa 2020, uwe uchaguzi huru na wa haki kiukweli kweli!.
Nimemuona akihutubia kwa humility na genuinity, hivyo mnaweza kushangaa akasimamia kuhakikisha ofisi ya DPP inatenda haki kweli na haki ikaonekana inatendeka, hivyo wote wanaoozea kwenye mahabusu za nchi hii wengine kwa miaka 7 kama wakili Medium Mwale, na wale wanaozea Keko, Ukonga, Segerea na mahabusu nyingine kama Harry Kitilya, Sio Sumari, Sinare, kina Isaack Kasanga, kina Gonzaga, kina James Rugemalila na wengine wengi, watetendewa haki, na haki kuonekana ilitendeka!.
Huwezi jua, kufikia 2025, President Magufuli might end up being the best president, this country had ever had, na sisi Watanzania katika umoja wetu, tukamlilia aendelee na kufanya maandamano nchi nzima kushinikiza katiba ibadilishwe, kipengele cha ukomo kieondolewe!.
Hongera sana rais wetu Magufuli, you are changing for the better!.
Big up!.
Viva Magufuli!.
Viva Tanzania!.
Paskali.