Magufuli is getting better and better, he is changing for the better. Hongera sana!

Magufuli is getting better and better, he is changing for the better. Hongera sana!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,103
Reaction score
128,723
Wanabodi,
Angalizo
Naomba kuanza bandiko hili kwa angalizo, kuna watu humu wana allergy kila rais Magufuli anapopongezwa kila ananapofanya jambo zuri, au jambo jema, wao wanakasirika, hivyo rais Magufuli akipongezwa kwa mazuri yoyote au mafanikio yoyote, wao wananuna, wanaumia, wanakasirika kwa sababu wanatamani ashindwe ili wakosoe. Ukimpongeza tuu rais Magufuli kwa lolote, utawasikia kuwa huku sii kupongeza bali ni kujikomba kuusaka uteuzi wa u-DC, au mara hizi ni njaa tuu za jina la Mayalla!!. Kama wewe ni mtu wa kundi hili, nakuomba uishie hapa ili nisije kukuharibia siku yako.

Japo Nina Chama, Lakini Sitafuti Uteuzi.
Naomba kusisitiza kuwa mimi Paskali, japo nina chama lakini sipongezi kusaka uteuzi wowote, ndio maana napongeza kwa mazuri na kukosoa madhaifu. Ningekuwa msaka uteuzi, ningeusaka zamani tangu enzi za Ben, maana mtoto wake ni class mate wangu darasa moja kwa miaka 4!. Ningekuwa msaka uteuzi, ningeusaka enzi za JK, maana Riz1, ni collage mate pale UD tena ni rafiki. Ningekuwa msaka uteuzi kwa Magufuli, ingekuwa siku nyingi nimeishaula, kwa taarifa yenu, kila nikisafiri kuelekea mitaa ya kule Biharamulo au Chato kikazi, nafikia kwa Magufuli!. Naendelea kusisitiza, kwa kipindi hiki chote ambacho mimi ni mwanahabari, japo nina chama ila itikadi yangu na ukada wangu uko moyoni mwangu tuu na sio kwenye kalamu yangu, Ila mwakani ninastaafu rasmi uandishi wa habari, hivyo nitaingia kwenye ulingo wa siasa na kuicheza ngoma, lakini kwa sasa kumtuhu mtu kama mimi kuusaka uteuzi, sio kunitendea haki!. Mimi siku zote ni mkweli daima, siegemei upande wowote, na nazidi kuusitiza ule wito wangu wa kwenye mazuri tupongeze, kwenye mapungufu tukosoe constructively, huku tukishauri the right thing to do na kwenye mabaya ndipo tulaumu na kulaani, bandiko hili ni la pongezi.

As days goes by, this man is getting, better and better, he is changing for the better!.
Leo nimemsikiliza rais Magufuli akihutubia kutokea Ukerewe, kiukweli kabisa, nimeguswa na hutuba ile na nimekuwa very impressed!, haswa alipozungumzia kuhusu, uzalendo, kuwa wakweli na kusisitiza maendeleo hayana vyama, akampongeza mbunge wa Ukerewe ambaye ni wa Chadema, na akatoa fursa kwa wana CCM wanaotaka kwenda upinzani, hakutokea mtu, akasema nikiuliza wapinzani wanaotaka kujiunga CCM, wengi watakuja, lakini siulizi kwa sababu huu sio mkutano wa CCM ni mkutano wa serikali!. This is good!.

Big up kwa rais wetu Magufuli kuanza kutenganisha shughuli za kiserikali na shughuli za chama. Kama tulimlaumu rais Magufuli kutumia state platforms kufanya siasa za CCM ikiwemo kupokea wanachama wapya, na leo amesema wazi, hatumii mikutano ya kiserikali kuigeuza ya CCM, ni jambo jema, ndio maana naendelea kusisitiza kwenye mazuri tupongeze.

Kutumia shughuli za kiserikali kupokea wanachama wapya wa CCM was not right, it was wrong. Katika bandiko hili,
Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! . - JamiiForums nilisema
Naendelea na huu msisitizo wa wasaidizi wa rais wetu sio malaika hivyo asaidiwe.
leo natoa ushauri rais wetu ni lazima atenganishe ni wakati gani atalihutubia taifa kama rais wa nchi na ni wakati gani atalihutubia kama Mwenyekiti wa CCM. Kitendo cha rais wa kufanya state event na kulihutubia taifa as Rais wa JMT na Amiri Jeshi Mkuu halafu ndani ya event anahutubia kama Mwenyekiti wa CCM na kuigeuza state event into CCM campaign event na kupokea wanachama wapya, not only it's not fair, it's not right, it is wrong!.

Wasaidizi wa rais msaidieni rais wetu kutenganisha ni events gani atahutubia kama rais wa JMT na ni events gani atahutubia kama Mwenyekiti wa CCM.

Mkuu wa nchi anapokuwa fair, nchi inabarikiwa, anapokuwa unfair, nchi inalaaniwa. Baraka hizo la laana hizo zinasababishwa na kitu kinachoitwa karma, karma haijui cha mfalme, cha rais wa nchi or nani ni nani, karma inataka haki bin haki kutendeka, viongozi wetu tutendeeni haki Watanzania ili Mungu nae awetendee haki, hata mkiwa na nguvu kiasi gani za mamlaka, msipotenda haki, Mungu atawaadhibu na kuiathibu nchi.
Paskali

Sisi jf japo tunalaumiwa na kulaaniwa kwa ukosoaji kwa rais Magufuli na Serikali yake kila inapoboronga, lakini kiukweli kabisa, wanaomkosoa rais Magufuli ndio wanaomsaidia zaidi kubadilika, changing for the better, kuliko wanaomsifia!.

Naamimi lile tukio la kupokea wanachama pale uwanja wa Sheikh Amri Abed, wakati wa kamisheni maofisa wapya wa jeshi, ni sisi JF pekee ndio tulilipinga humu, na leo limezaa matunda.

Nimenote kupungua kwa vikao vya CCM kwenye ikulu yetu, sasa vikao vya CCM, vinafanyikia ama CCM Lumumba, ama CCM Makao Makuu Dodoma!.

Mabadiliko haya ya mkuu wa nchi changing for the better ni very healthy kwa nchi yetu. Huwezi kujua, huenda hata ule uvunjaji wa katiba kuzuia mikutano ya siasa, soon nao pia utasitishwa only if kama atabaini, it was not right, it is wrong kuzuia jambo lililoruhusiwa na katiba ya nchi, kwa sababu rais wetu amezuia mikutano hiyo kwa nia njema kabisa, bila ya yeye kutambua kuwa hayuko juu ya katiba, hana mamlaka hayo aliodhani anayo, na wasaidizi wake wanaolijua hili, wamenyamaza tuu na kumuangalia tuu, tena wengine nawajua, walikuwa waalimu wetu pale UDSM, tena ni mabingwa wa sheria na katiba wenye GPA record ya 4.9! na haijawahi kuvunjwa mpaka leo!, lakini wapo wanaona kabisa rais anafanya kinyume cha katiba lakini wananyamaza badala ya kumshauri!. Rais Magufuli naye ni binaadam na sio malaika hivyo hawezi kujua kila kitu ndio maana ana wasaidizi!.

Tuendelee kumuombea rais Magufuli, Mungu azidi kumlinda na kumuongoza vema kuitawala vema nchi yetu, mnaweza msiamini, anaweza kuamua kuifumua Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC na kuunda tume huru zaidi ya Uchaguzi ambayo itakuwa inclusive!, kama ameweza kumchukua Prof. Kitila, na yule mama wa ACT, na kuwaingiza kwenye serikali yake, atashindwa nini kuifumua NEC ili uchaguzi wa 2020, uwe uchaguzi huru na wa haki kiukweli kweli!.

Nimemuona akihutubia kwa humility na genuinity, hivyo mnaweza kushangaa akasimamia haki na kuhakikisha ofisi ya DPP inatenda haki kweli na haki hiyo ikaonekana inatendeka, hivyo wote wanaoozea kwenye mahabusu za nchi hii wengine kwa zaidi ya miaka 7 kama wakili Medium Mwale, na wale wanaozea Keko, Ukonga, Segerea na mahabusu nyingine kama kina Harry Kitilya, Sioi Sumari, Shose Sinare, Isaack Kasanga, Gonzaga, James Rugemalila, Jamal Malinzi, Peter Noni, Dr Ringo Tenga, wale Ma Sheikh wa Uamsho na wengine wengi, wanatendewa haki, na haki kuonekana inatendeka!. Kuna watu wanaoshitakiwa kwa makosa ambayo ukikutwa na hatia adhabu yake ni kifungo cha mwaka mmoja jela, lakini mtu yuko mahabusu mwaka wa 7 sasa na kesi haijaanza kusikilizwa!, huu ni uchunguzi gani ambao haukamiliki, na hii ni haki ya aina gani inayocheleweshwa?!.

Huwezi jua, kufikia 2025, President Magufuli might end up being the best president, this country had ever had, kwa kutuachia katiba mpya!, hii itapelekea sisi Watanzania katika umoja wetu, tukamlilia aendelee na kufanya maandamano nchi nzima kushinikiza katiba ibadilishwe, kipengele cha ukomo kiondolewe!.

Hongera sana rais wetu Magufuli, you are changing for the better!.
Big up! and God bless you.

Viva Magufuli!.
Viva Tanzania!,
Mungu mbariki Magufuli, Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali.
Rejea
Rais Magufuli Akifanya Mazuri, Apongezwe: Hotuba Yake Kuzima Mwenge, Ni One of The Best! - JamiiForums
Tusilalamike Tuu, Kulaumu na Kulaani Kila Kitu, Kwenye Mazuri Tupongeze, Rais Magufuli is Changing For The Better!. - JamiiForums
Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! . - JamiiForums
Jee Aachwe Aseme Tuu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or Atumie Busara?!. - JamiiForums
 
Amesema leo ukitaka kumtawala mtu mnyime elimu, ukimnyima elimu unaweza kuwa Rais wa Milee na ukawatala millele.

Sasa msomi kama Pasco unavyokuja na bandiko la kupendekeza Raisi ikimpendeza atawale maisha napata ukakasi.

Hapa ndio utajua tatizo la Tanzania ni wasomi wetu na sio vinginevyo.

Toka alivyotoka Chato naona kama Magufuli anaongea kitaifa zaidi, japo hulka haiwezi kuisha kirahisi.

Maana kuna muda amesikika akisema "nipendwe mimi kwani Mwanamke" japo aliongea kwa kisukuma.
 
To be the best president ever"....wenzake 46 maraisi wako Beijini China kujadili $400 bn za China itakazo wekeza bara la Africa mwaka 2019/20 yeye iko ukelewe kuzindua mradi wa maji wa 1bn Tshilling that's amazing...public international relation is more important for both our economy and politics.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla,
Ni kweli kuna baadhi ya mambo yanakwenda vyema, ila kama Mkuu wa Nchi awe anahutubia kwa upole na upendo, lakini likija suala la kushughulikia uzembe, wizi na ufisadi awe mkali na kutumia wembe uleule, na uwe kwa wote. Mfano kuna Clip moja inaonyesha Rais akiahidi kulipa deni la Wafanyakazi la Tsh 3.7Bilioni.

Hapohapo akachomeka, mtazitaapika! Hii ilikuwa lugha kali kiasi. Angeweza tu kuwaasa kuwa anategemea watafanya kazi kwa weledi na uaminifu na yeyote atakaye kwenda kinyume taratibu za kinidhamu na kisheria zitawawajibisha. Huyu ndiye rais wetu na sisi ni wananchi wake, tuchukuliane kwa upendo na upole.
 
Paskali tangia upigwe biti pale ikulu siku zile plus kuambiwa kua jina lako linamaanisha njaa naona umechange gear angani unaanza kuutafuta UDC kwa nguvu na akili zote
 
Ni kweli kuna baadhi ya mambo yanakwenda vyema, ila kama Mkuu wa Nchi awe anahutubia kwa upole na upendo, lakini likija suala la kushughulikia uzembe, wizi na ufisadi awe mkali na kutumia wembe uleule, na uwe kwa wote. Mfano kuna Clip moja inaonyesha Rais akiahidi kulipa deni la Wafanyakazi la Tsh 3.7Bilioni. Hapohapo akachomeka, mtazitaapika! Hii ilikuwa lugha kali kiasi. Angeweza tu kuwaasa kuwa anategemea watafanya kazi kwa weledi na uaminifu na yeyote atakaye kwenda kinyume taratibu za kinidhamu na kisheria zitawawajibisha. Huyu ndiye rais wetu na sisi ni wananchi wake, tuchukuliane kwa upendo na upole.
Nadhani luga siyaukali. Tulikuwa na rais mpole mukasema mmechoka tukamuomba Mwenyezi Mungu atupe mukali nae Mungu akasikia maombi....... Sasa tena munataka mpole??
 
Wanabodi,
Naomba kuanza na angalizo, kuna watu humu wana allergy Magufuli akipongezwa, hivyo utawasikia kuwa huku ni kuusaka UDC mara njaa!. Naomba kusisitiza kwenye mazuri tupongeze.

As days go by, this man is getting, better and better, he is changing for the better!.

Leo nimemsikiliza rais Magufuli akihutubia kutokea Ukerewe, kiukweli kabisa, nimekuwa very impressed!, haswa alipozungumzia maendeleo hayana vyama, akampongeza mbunge wa Ukerewe ambaye ni wa Chadema, na akatoa fursa kwa wana CCM wanaotaka kwenda upinzani, hakutolea mtu, akasema nikiuliza wapinzani wanaotaka kujiunga CCM, wengi watakuja, lakini siulizi kwa sababu huu sio mkutano wa CCM ni mkutano wa serikali!. This is good!.

Big up kwa rais wetu Magufuli kuanza kutenganisha shughuli za kiserikali na shughuli za chama.

Sisi jf japo tunalaumiwa na kulaaniwa kwa ukosoaji kwa rais Magufuli na Serikali, lakini kiukweli kabisa, wanaomkosoa rais Magufuli ndio wanaomsaidia changing for the better, kuliko wanaomsifia!.

Naamimi lile tukio la kupokea wanachama pale Sheikh Amri Abed, wakati wa kamisheni maofisa wapya wa jeshi, ni sisi JF pekee ndio tulikipinga, na leo kimezaa matunda.
Nimenote kupungua kwa vikao vya CCM kwenye ikulu yetu, sasa vikao vya CCM, vinafanyikia CCM Lumumba.

Huwezi kujua, kufikia 2025, President Magufuli might end up being the best president, this country had ever had, na sisi Watanzania katika umoja wetu, tukamlilia aendelee na kufanya maandamano nchi nzima kushinikiza katiba ibadilishwe, kipengele cha ukomo kiendelee!.

Hongera sana rais wetu Magufuli, you are changing for the better!.
Big up!.

Viva Magufuli!.
Viva Tanzania!.
Paskali.
Hata ufanyeje hupati uteuzi nakuhakikishia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom