Magufuli duniani Leo

#No one like JPM,

Kwa wote mnaojaribu kutuaminisha ujinga kaeni mkijua magufuli anapendwa sana na wanyonge wote Afrika.

juzi tu hapa tumetoka kushuhudia wazambia wakipagawa juu ya uwepo na kumshuhudia pale zambia.mpaka waziri mmoja akichanganyikiwa na kumpigia magoti.

Na kule kenya mpaka hata rais uhuru ameanza magufulification.

mambo ni hivyo dunia na afrika kwa ujumla wanamtambua kama rais mzalendo kwa bara la afrika.

mfano ni nchi za SADEC nk!

Wazungu hasa wamarekani na hao wa EU wanamuona mwiba,
wanamuona kama mtu anayetaka kuwashitua viongozi wengi barani afrika kuukataa unyonyaji wa raslimali za nchi zao.

Ukiongeza na jinsi alivyokataa kujipendekeza kwao tangu aingie madarakani,ni lazima wamtazame kwa jicho la tatu.
kwa hiyo nyinyi wapinzani wake wa ndani ya nchi,tunawajua ni kwa nini mnamchukia.

tuachieni bulldozer lifagie nchi.

viva JPM 2025
 
Visingizio. Uchafu wake unaonekana wazi.
Magufuli amefifia machoni kwa wazungu baada ya kuwakamata wezi wa dhahabu na makinikia pale bandarini. ndio walipoanza kumchukia na kutumika kwa vibaraka wa ndani (Mbowe, Zito, Tundu Lissu n.k.) kumchafua zaidi ili mataifa yamuone hafai.
 
Dikteta mzalendo? Hata kwa makaburu SA, ubaguzi ulipakwa lipstick na kuitwa 'separate development' policy.
 
Chakushangaza sasa kipindi chote hicho anasifiwa hukuleta uzi tujue
 
Unategemea kabisa nchi za Ulaya na US zitoe sifa kwa rais mzuri wa Afrika? Rais mzuri ni kama akina Mobutu, wale wanaoruhusu makampuni kupitisha makinikia. Ukiona rais wa Afrika anapewa sifa, ujue hakuna rais hapo!
 
Hiyo ilikuwa "initial euphoria".

Kiswahili tynasema "nguvu ya soda".

Mtuhani wa uongozi ni kuweza kuwa na "strategic staying power".

Magufuli si strategic na hana staying power.

Ndiyo maana ukiacha the low hangubg fruit kujenga infrastructure, hakyna la maana analofanya consistently and strategically.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wengi walianza kushtuka baada ya Acacia kudaiwa kodi ya shilingi trilioni190! Isitoshe mambo yaliyowasisimua baadhi ya watu ni mambo mepesi tu kama kufagia barabara, kufuta sherehe za kitaifa, kufukuza watumishi kazi hadharani, kuzuia safari nje ya nchi, kuzuia mikutano, warsha, semina, nk.
 
Baada ya Matukio ya watu kutekwa na kupotea, Lissu kushambuliwa mchana kweupe, na watu kukatazwa hata kukamatwa kwa kumuombea dua Lissu Dunia sasa imepata picha halisi ya huyo unaye mtaja.
Urembo wa kuchonga haudumu
Hakika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…