Magufuli bila madaraka yukoje?

Kumbe ..................!!
 
Enzi za mwanakijiji hizo,pesa ni mwanaharamu sana.hata yuda alimsariti bwana yesu kwa vipande 30 tu.namkumbuka mwanakijiji kipindi kile namsoma kwenye Tanzania daima
 
"Kumkoma Nyani Giladi"......Hiyo ndiyo ilikuwa misemo yao lakini sasa inamrudia na yeye!
 
N

Ni kweli kabisa! Rais Magufuli ni aina ya watu wachache wanoelewa ukubwa wa dhamana inayoendana na nafasi ya utendaji ya uteuzi au uchaguliwa. Kwa makala hii Mwanakijiji amenishangaza sana juu ya uwezo wake wa kuona kwa undani, na kuweza kupambanua kwa kina na usahihi uhalisia wa tabia ya kiongozi wetu wa awamu ya tano.

Who cant follow, cannot learn how to lead. Kitendo cha kutambua madaraka ya Rais na implications zake kulimsaidia kufanya uamuzi sahihi wa kutojiuzulu, ambayo ingehasisha hili tunalolizungumza sasa.

Kuna aina ya viongozi ambao wanatafuta nafasi za uongozi na wanapozipata wanashindwa kujua dhamana, na mamlaka yanayoambatana na nafasi hizo. Hao ni aina ya viongozi ambao utamsikia anailaumu serikali, bila kutambua kwamba yeye ni sehemu ya hiyo serikali, na uamuzi husika uko mikononi mwake, na unamuwezesha kuwa sehemu ya suluhisho na siyo muendelezo wa tatizo/changamoto zinazo wakabili aliojukumishwa kuwahudumia: Kwa sababu ya madaraka aliyopewa kwa mujibu wa sharia, kutokana na nafasi anayoishikilia, pia ndani ya mipaka na ukomo wa kiongozi anayemzidi au aliyemkasimisha madaraka husika

Aina ya watu kama Mh. Magufuli wana uwezo wa kutambua uzito wa madaraka wanayokabidhiwa, na uhalisi wa kisheria unaowathibitisha katika madaraka hayo. Kwa sababu hiyo, wana uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo makubwa kupitia nafasi zao za uongozi, kwa kuwa wanajua kwa uhakika uwezo unaoendana na nafasi husika. Kwa mantiki hiyohiyo, watu wa aina hiyo wanajua kwa uhakika, kwamba mara nafasi zao za uongozi zinapokoma, na mamlaka na uwezo wa kuathiri mifumo ya Taasisi wanazoziongoza inafikia ukomo pia. Hivyo ni kwelii nje ya nafasi za madaraka utawakuta watu wa namna hii, wakijishughulisha na mambo ya kawaida tu, kwa kuwa wanajua hawana dhamana ya madaraka husika. Nchi ikimpata kiongozi wa aina hii, ambaye hana nia ya kujijengea himaya ya kiuchumi (Kwa sababu hana nia ya kujijengea mamlaka yanayotokana na nguvu binafsi za kiuchumi): Nchi hiyo inakwenda mbali na kwa haraka sana.

Historia ya nchi yetu itakapoandikwa, Rais Magufuli atakuwa na nafasi ya pekee sana kutokana na jinsi Mungu alivyomuumba. Na Mzee Mwanakijiji aliweza kuona au kuonyeshwa moja kwa moja essence ya kiongozi wetu huyu.

Mungu mlinde na kumbariki Rais JPM, Mungu ibariki Tanzania, na wale wote wenye mapenzi mema na Watanzania.

NB: Viongozi wanaoamini kwamba chimbuko la mamlaka yao ni uwezo wao binafsi wa kiuchumi, na siyo dhamana ya madaraka ya kisheria waliyonayo; mara zote huharibu. JPM anautambua uzito, mamlaka, na uwezo unaoambatana na madaraka. Ni very focused: Atafanikiwa!
 
Mzee Mwanakijiji alipokuwa ktk ubora wake Enzi hizo. .. alikuwa msemakweli daima
 
Mpwa kumbe una maono kiasi hiki.
 
Mzee Mwanakijiji alipokuwa ktk ubora wake Enzi hizo. .. alikuwa msemakweli daima
Kwa kweli huyu mtu ni hazina, kama wapinzani wangemsikiliza wangefika mbali mno. Ona alivyomuona Magu vizuri as mtendaji anaejua kusimamia kazi na majukumu aliyopewa. JPM sio mwanasiasa, sio mwanaharakati, sio mpiga dili bali ni mtu anayebebwa na kazi yake nzuri anayofanya kwa moyo wote.
 
vp ndugu, huku kumbukwa kwenye Ufalme? Endelea utakumbukwa kama wakina Taratibu. Changamkia fursa Mkuu.
 
Kiongozi anayeamini katika kanuni na sheria tunamhitaji katika nchi hii kwa sasa. Nchi yetu haihitaji kiongozi wa kuwafurahisha watu bali mwenye 'discipline, vision, goals and action'.
Hatimae tukampata, Allah alisikia kilio chako, pamoja sasa haupo upande wake
 
Mzee Mwanakijiji alipokuwa ktk ubora wake Enzi hizo. .. alikuwa msemakweli daima
Watu wa Chadema wanazani kusema ukweli ni kuwasema viongozi wa serikali ya CCM.. ila akiwasema wa upinzani inaonekana msaliti.. Ukweli ni ukweli hauna upinzani au CCM.. Sasa ukawa na vibaraka wao.. Wao wanaona ukiwasema serikali ya CCM NDIO UKWELI ILA UKIWA SEMA CHADEMA AU UPINZANI BASI MSALITI
 
kati ya mawaziri waliokuwa wanamsifu Kikwete ndani ya utawala wake yumo
 


Duh.. prophetic one might say...
 
we we jamaa ni nabii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…