Huu nao ni ujuha,
Pombe kama ameanza vizuri haimaanishi miaka mitano atakuwa na kasi hiyo hiyo. No proof for that!
Isitoshe mara zote nasema, watazania walio jitoa kuwaunga mkono wana mabadilikowanatakiwa kujipongeza na hata wale ambao hawakufaya hivyo wanatakiwa kufanyahivyo. Kwa nini nasema hivyo??Historia inaonyesha kwamba Nchi nyingi tunapo onawanasiasa wanao fanya vizuri ni katika nchi ambazo kuna upinzani mkubwa ninamaana kwamba nguvu ya chama kinacho tawala ni karibu sawa nakile/vile visivyotawala / visivyo kuwa madarakani/ wapinzani.
Ni kwa sababu hii anaye pata nafasi yakuongoza anafanya kila kilicho cha heri ili ama yeye mwenyewe ama chama chakekuepuka kukosa nafasi ya kuongoza tena msimu/ misimu inayo fuata. Ni rahisi tu,TANU / ASP na sasa CCM vimekuwa madarakani kwa kipindi kirefu sana tangu 1940shadi kujijengea himaya ya kutokusikiliza ushauri wa wananchi wengi ambao ndiyowatanzania masikini katika nchi yao. Watawala hao hawakusikia wala kuona hatakunusa yale yanayo pigiwa kelele na wananchi. Kwa sababu wana uhakika wa kurudimadarakani kwa gharama,mbinu, uwezo na uzoefu wao wa kukalia nchi watakavyo.Kwa maana hiyo, Pombe amezinduka na kufanya yale wananchi wengi wnanyo pigiakelele kwa maudhi yake na ambayo bado yapo sana, tumshukuru yeye mwenyewebinafsi kwa mapenzi yake kuamua kuacha kufuata UNAZI wa chama chake CCM. Ilamnapo toa shukrani zenu muweke na akibaya kesho, hata mwezi sijui kamaamemaliza, bado miaka mitano kumpima. Hata unapo pewa madaraka au kazi kunamuda wa kupimwa. Je, Kipimo cha utendaji wa Rais ni muda gani? Siku ngapi?Miezi mingapi? Miaka mingapi? Nachelea kusema ni mapema sana kusifia na kutoashukrani zenu zinazo pitiliza kana kwamba ndiyo kamaliza miaka mitano!!!!!!!
Hata serikali itakayo fanya kazi kwaniaba yake au chini yake bado haijaundwa,Wasifuni mna jeuri gani ya kutoashukrani zenu kiasi hicho? Wekeni akiba ya maneno kesho msijilaumu tena kesho!
CCM ambacho ndicho kinga ya Rais wasasa ina furahia yanayo tendwa na mwakilishi wao? Je, chama kime bariki yanayoendelea na kipo tayari kuendelea kumuunga mkono Rais wake kwa mendo mema atkaoenendelea kufanya kwa ajili ya Watanzani maskini? Majibu kaa nayo!Je, Kasi hii ya Rais Pombe ni sawa namkimbiaji wa mita 100 au ni sawa na mwana riadha wa mita ndefu? Kasi ya mwanariadha wa mita 100 ni karibu sawa mwamzo mwisho hali hiyo ni tofauti kwa mwanariadha wa umbali / mita ndefu! Chukua angalizo!
Nitakuwa wa mwisho kuamini haya yanayofanywa na Rais Pombe na binafsi nieleweke kuwa naunga mkono jitihada hizo zaawali lakini sitaki kuanza kusifia kwani najua madhara ya kuumwa na nyoka namsemo kuwa ?MGEMA AKISIFIWA TEMBO HULITIA MAJI? Natoa angalizo kwenu wapambekwamba kuweni makini na vijisifa!
Na nita msifu Pombe ikiwa atawekamfumo wa yeyote anaye shika nafasi ya kuongoza ama kufanya kazi ya Wananchikuwajibika ipasanvyo bila kutegemea moyo na hulka ya kiongozi! Hili ni Zaidi yakujua ukiukaji SIYO UKAMATAJI wa wahujumu uchumi. Anaye hisiwa kuwa Mwizi wakuku hukamatwa tena kwa mbwembwe hadi kumwondolea heshima na ukiukaji wa hakiza binadamu, nilitegema kwa akili ya kawaida nguvu ya kukamatwa aukushughulukia mhujumu uchumi ingekuwa mara xxxxxxxx (exponent n) badala yakehata kutaja jina lake hadharani ni kosa! Haya siyo mazinga ombwe au???? Hiisiyo sawa na panyak umfunga paka kengele?
Rais ajenge mfumo wa uwajibikajikuliko hata ule ulipo katika sekta binafsi. Pombe atafanya anayojua lakini sinaimani kwamba CCM ya kesho itafanya hivyo, who knows? Nani anayejua kwamba RaisX wa kesho atakuwa mtendasji na mwajibikaji kama alivyo anza Pombe leo, nani?Nani anaye jua kwamba Pombe atawanyosha wakwepa kodi na watumishi Miungu watumwanzo mwisho kwa kuchukua hatua sitahiki kama SHERIA ZA NCHI zinavyo elekeza,nani? Nani anaye jua kwamba Rais
Pombe atawashughulikia ipasavyo waingiza wauzaunga mwanzo mwisho maana ya mwanzo wisho ni 2015-2020, nani? List ni kubwamuda sina!Nitakuwa wa ?Tomaso? na wa mwisho kuamini na kusifu!