Mgawo wa Umeme upo. Tanesco wanamuogopa Magufuli kulisema hili. Hii inatufanya tushindwe kupanga mipango yetu. Haiwezekani umeme unakatika mara kwa mara na kwa muda mrefu, tunaambiwa hakuna mgawo. Ni bora kuwa wazi na hali ya halisi kuliko utendaji usioeleweka. Kuna maeneo Dar es Salaam, kwa muda wa wiki sasa umeme umekuwa wa kusuasua. Tuambie ni nini? Vinginevyo tunakuja kula kwenye familia zenu. Maana service fees ipo pale pale na huduma hakuna. Tunawalipa TANESCO, si zama za kuwabembeleza.