Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 79
Waziri wa Ujenzi John Magufuli jana ameumbuka kutokana na tuhuma zake. Hayo yametokea katika mkutano wa bodi ya barabara katika mkoa wa Dar es salaam uliofanyika mnazi mmoja.
Mara baada ya Mkuu wa Mkoa Mecky Sadiq kufungua mkutano huo mbele ya waandishi wa habari, alimkaribisha katibu tawala wa mkoa huo (jina halijapatikana) kusoma kuanza ajenda ya kuthibitisha muktasari wa mkutano uliopita.
Mbunge wa Ubungo, aliingilia kati na kutaka kwanza kikao kithibitishe ajenda na kutoa tuhuma kwamba ajenda moja imeingizwa kinyemela. Mnyika aliitaja ajenda hiyo kuwa ni ‘kupokea mapendekezo ya kupandisha hadhi barabara za Mkoa wa Dar es salaam" ambayo alieleza kuwa ikijadiliwa itaeleweka kuwa ndio sasa mkoa umeanza kushughulikia suala hilo.
Mkuu wa Mkoa alitetea uamuzi huo akidai kwamba kuingizwa kwa ajenda hiyo kutaonyesha kwamba wabunge, madiwani na watendaji wa mkoa wa Dar es salaam wamelipa uzito zaidi suala hilo kufuatia kauli ya Waziri Magufuli.
Hata hivyo Mnyika alisisitiza suala hilo lijitokeze kwenye yatokanayo ili badala ya kujadili mapendekezo taarifa itolewe kuhusu utekelezaji wa serikali baada ya mapendekezo kuwasilishwa kwa Wizara ya Ujenzi kwa nyakati mbalimbali.
Msimamo huo uliungwa mkono na Meya wa Kinondoni Yusuph Mwenda na kumlazimu Mkuu wa Mkoa ambaye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkutano na kukubali kuiondoa ajenda hiyo ili ijadiliwe kama sehemu ya yatokanayo na mkutano uliopita wa bodi hiyo ya barabara.
Katika ajenda hiyo ya yatokanayo suala hilo la kupandishwa kwa hadhi ya barabara za Mkoa wa Dar es salaam lilijadiliwa na wachangiaji wengi zaidi huku wajumbe wakielekea kukubaliana kwenye sehemu kubwa ya maoni na wakizungumza kwa hisia kali.
Wa kwanza kuzungumzia ajenda hiyo kwa mara nyingine tena alikuwa ni mbunge wa Ubungo ambaye alidai kwamba tayari bodi ya barabara ilishapeleka mapendekezo ya kupandishwa hadhi kwa barabara za Dar es salaam katika mikutano ya mwezi Februari na Oktoba 2011 lakini Waziri wa Ujenzi hajatoa majibu yoyote hali ambayo imechelewesha ujenzi wa barabara za kupunguza foleni.
Mnyika alisema kwamba suala hilo limesababisha Dar es salaam kutokutengewa Fedha za kutosha za ujenzi wa barabara, na akataka mwakilishi wa TANROADS na Wizara ya Ujenzi katika kikao hicho kueleza iwapo ni ukweli kwamba serikali inafedha za barabara kwa ajili ya Dar es salaam ambazo zimekaa bila kutumiwa kama alivyodai Waziri Magufuli. Mnyika alimalizia kwa kutaka vigezo vya kupandisha hadhi barabara vya mwaka 2009 vibadilishwe ili kuwe na vigezo maalum kwa ajili ya Dar es salaam ambavyo vitazingatia umuhimu wa jiji kitaifa na hali mbaya ya foleni ilivyo hivi sasa.
Wapili kuzungumzia hoja hiyo alikuwa Mbunge wa Kigamboni Dr Ndugulile ambaye alisema kwamba kama Serikali kupitia kwa Waziri wa Ujenzi imesema kwamba ina Fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Dar es salaam ni kwanini badala ya kuongeza hadhi ya barabara nyingi zaidi imeleta pendekezo jipya la kushusha hadhi za barabara na kuzirejesha kwa Manispaa. Dr Ndugulile alipinga mpango huo na badala yake alitaka Wizara ya Ujenzi ipandishe hadhi barabara zilizoombewa kwa muda mrefu kupandishwa hadhi.
Mwigine aliyezungumzia jambo hilo kwa ukali ni kiongozi wa chama cha wasafirishaji aliyejitambulisha kwa jina moja la Mabruk alinukuu gazeti la habari leo ambalo lilomnukuu Waziri Magufuli akieleza kuwa Wizara ya Ujenzi iko tayari kuondoa tatizo la foleni Dar es salaam isipokuwa Manispaa za Jiji la Dar es salaam zinang'ang'ania barabara hizo na kutaka maelezo ya TANROADS na Mhandisi wa Mkoa. Katika maelezo yao waataalamu walioshiriki kikao hicho walieleza kuwa kikwazo cha kupandisha hadhi barabara nyingi zilizoko chini ya Manispaa kwa sasa ni vigezo. Mabruk aliingilia kati na kudai kuwa kama kikwazo ni vigezo ambavyo vimetengenezwa na Waziri, kwanini Waziri huyo huyo anazisingizia Manispaa badala ya kufanya kazi inavyostahili.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni alisisitiza kwa Manispaa hazijawahi kuwa kikwazo na kuitaka Wizara ya Ujenzi iongeze fungu kwa ajili ya ujenzi wa barabara, sisi ndio tunaochangia kwa zaidi ya asilimia 70 kwenye Fedha zinazotokana na kodi ya mafuta lakini barabara zetu zinatengewa Fedha kidogo. "Serikali inafanya kama vile Dar es salaam tunapaswa kupiga magoti na kuomba, wakati Wizara ya Ujenzi inapaswa kufanya kazi ya kuleta maendeleo na kutoa mgawo mkubwa kwa barabara zetu kwa kuwa ni haki yetu.", alisema Mwenda.
Msimamo huo wa wajumbe ulifanya Mwenyekiti wa Mkutano aombe kwamba ajenda hiyo isiendelee na badala yake kuundwe kamati maalum ya kuonana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na Waziri Magufuli kuhusu barabara za Dar es salaam kupandishwa hadhi na kuongezewa Fedha za ujenzi. Pia, mkuu wa mkoa alisema kwamba hoja isiwe kiwango cha mapato kinachokusanywa toka Dar es salaam bali iwe ni umuhimu wa barabara za Dar es salaam na jiji lenyewe kwa kuwa zinatumiwa na wananchi wa kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Kufuatia kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa, Mnyika alitaka kwamba hoja kuu iwe ni hasara ya kifedha na athari za kiuchumi kutokana na matatizo ya msongamano wa magari, na kutaka wataalamu waandae hoja yenye kuonyesha tija ambayo nchi itapata iwapo barabara zote muhimu za kupunguza foleni zinapandishwa hadhi na kujengwa kwa pamoja kwa kipindi kifupi inavyowezekana.
Ajenda nyingine iliyovuta hisia za wachangiaji ni taarifa ya utekelezaji ya miradi ya barabara katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ambapo wajumbe walihoji ufanisi wa kazi zinazofanywa na wakandarasi mbalimbali, kupungua kwa utawala wa sheria katika masuala ya barabara hali ambayo inachangia katika ongezeko la foleni na ajali na mpango mpya wa njia moja katika barabara za katikati ya mji ambao utazinduliwa karibuni baada ya kufanyika kwa mkutano na wadau.