Magufuli atakumbukwa kwa uthubutu wake lakini pia kwa makosa makubwa ya msingi

Status
Not open for further replies.

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Naandika haya kwa mtazamo wa kihistoria. Chukulia unasoma hili mwaka 2075 (miaka 55 kutoka sasa).

Inawezekana ni mapema kuyaandika haya kwa sababu utawala wake bado unaendelea na amebakisha mwaka mmoja kabla hatujaenda tena kwenye uchaguzi.

Ila niseme tu kwa ufupi kuwa Rais Magufuli alithubutu kufanya mambo kadhaa mazuri ila approach ndiyo ilimuangusha sana.

Inawezekana alijitwika mzigo mkubwa sana kurekebisha matatizo ya msingi ambayo watangulizi wake yaliwashinda hasa suala la rushwa iliyoota mizizi katika ngazi zote.

Hakuna mwananchi wa kawaida ambaye si muhanga wa tatizo hili la rushwa na kwa hilo Magufuli alistahili kupata support kubwa ya wananchi wengi wa kawaida. Lakini nadhani hakuelewa ukubwa wa tatizo na kwa kiasi gani liliota mizizi hata kupenya katika taasisi nyeti. Tatizo lake lilikuwa kubwa zaidi kwa kuamua kutumia njia ambazo wengi waliona hazikuwa zinafuata katiba na sheria za nchi.

Kuna watu muhimu ambao wangemsaidia sana katika vita yake ya rushwa ila badala ya kuwaweka karibu wamsaidie ndiyo akawafanya maadui zake. Hilo lilikuwa ni kosa kubwa.

Atakumbukwa pia kwa kuamua kulifufua shirika la ndege la Air Tanzania ambalo baada ya kusuasua mwanzoni mwa utawala wake sasa ni moja ya mashirika bora kabisa Afrika likiwa lina ndege 114.

Tuendelee kuliombea taifa letu ili hila za shetani zilizoanza kuota mizizi zishindwe. Tuendelee kuipiga vita rushwa kwa nguvu zetu zote ila turudi kwenye utawala wa haki na sheria. Hatujachelewa.
 
Atakumbukwa pia kwa kuamua kulifufua shirika la ndege la Air Tanzania ambalo baada ya kusuasua mwanzoni mwa utawala wake sasa ni moja ya mashirika bora kabisa Afrika likiwa lina ndege 114.
Sikujua kama tayari zimefika ndege 114. Kuwa serious mkuu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom