Magufuli 'apigwa' Bilioni 100

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,007
2,000


Juhudi za Rais John Pombe Magufuli kuongeza makusanya ya kodi zinahujumiwa, baada ya uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI kubaini kuwa katika wilaya moja tu ya mpakani, anapoteza zaidi ya Sh bilioni 100 kwa mwaka.

Uchunguzi wa kina uliofanywa umebaini kuwa mji wa Tunduma unaoongoza kwa mapato katika halmashauri za mji nje ya Jiji la Dar es Salaam, umekuwa kitovu cha kuvuta shati kasi ya Rais Magufuli katika kukusanya kodi.

“Mji huu unatisha. Hapa kwa biashara inayoendelea, nchi kwa ujumla inapoteza hadi Sh bilioni 300. Kuna magendo haijapata kutokea. Kuna sigara zinavushwa kutoka Zambia zinaingia Tanzania mchana kweupe katoni nyingi tu.

“Hapa baiskeli, mikokoteni, magari, waenda kwa miguu, biashara kubwa ni magendo. Kuna vipodozi, sigara, pombe kali za kila aina, Heineken, hata konyagi ya Tanzania, nguo na kila unachofahamu kuwa kinauzika, kinavushwa mchana kweupe.

“Polisi wanajitahidi, lakini unaweza kuwahurumia. Watu wa hapa wakifahamu kuwa mtu fulani anaingilia biashara yao, wanachofanya ni kumuua. Hivyo, hata polisi waliopo hapa maisha yao yako hatarini wakijipendekeza kupambana na magendo. Labda kije kikosi maalumu cha makomandoo tunaowaona katika maadhimisha ya siku ya uhuru,” anasema mtoa taarifa.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Luteni Chiku Galawa, anakiri na kuthibitisha kuwa kiwango cha mauaji Tunduma kiko juu na kuwa biashara ya magendo inayoendelea hapo Tunduma inatisha wakati bidhaa za magendo kupitia Tunduma zinasafirishwa kwa treni za Tazara, kwenda katika karibu mikoa yote nchini, ila anayo dawa ya tatizo hilo.
 

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
40,235
2,000
Si ndio hiki watu wanalialia kila siku kabana. Haya sasa bilioni 100 kuleni maisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom