Rais Mwinyi afanya ziara ya kushtukiza bandari ya Wete na kukuta Karafuu za magendo tani 9.5

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
868
552
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametembelea Bandari ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba katika ziara ya kushtukiza na kushuhudia karafuu za magendo tani 9.5 zenye thamani ya shilingi milioni 140 zilizotaka kusafirishwa kwa magendo na kukamatwa kwa ushirikiano wa Vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Kaskazini Pemba vikiwemo Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) na Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM) tarehe 04 Januari 2024 , Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Aidha Rais Dkt. Mwinyi ameleeza kuwa Serikali imeamua asilimia 80 ya mauzo ya karafuu katika soko la Dunia kumpatia mkulima wa karafuu na 20 kwa shirika la biashara Zanzibar (ZSTC) kutumika katika uendeshaji.

Vilevile Rais Dkt. Mwinyi amesema karafuu iliyokuwa bora inatoka Zanzibar kwa kuitunza vizuri na kuisafisha bei yake itaendelea kuimarika duniani.

Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi amewasihi wananchi wasifanye magendo kwa maana watapata hasara kulingana na sheria za nchi, pia amesema Serikali itaendelea kuongeza bei ya karafuu.
IMG-20240105-WA0013.jpg
IMG-20240105-WA0017.jpg
IMG-20240105-WA0011.jpg
IMG-20240105-WA0015.jpg
IMG-20240105-WA0014.jpg
IMG-20240105-WA0016.jpg
IMG-20240105-WA0009.jpg
IMG-20240105-WA0010.jpg
IMG-20240105-WA0012.jpg
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametembelea Bandari ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba katika ziara ya kushtukiza na kushuhudia karafuu za magendo tani 9.5 zenye thamani ya shilingi milioni 140 zilizotaka kusafirishwa kwa magendo na kukamatwa kwa ushirikiano wa Vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Kaskazini Pemba vikiwemo Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) na Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM) tarehe 04 Januari 2024 , Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Aidha Rais Dkt. Mwinyi ameleeza kuwa Serikali imeamua asilimia 80 ya mauzo ya karafuu katika soko la Dunia kumpatia mkulima wa karafuu na 20 kwa shirika la biashara Zanzibar (ZSTC) kutumika katika uendeshaji.

Vilevile Rais Dkt. Mwinyi amesema karafuu iliyokuwa bora inatoka Zanzibar kwa kuitunza vizuri na kuisafisha bei yake itaendelea kuimarika duniani.

Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi amewasihi wananchi wasifanye magendo kwa maana watapata hasara kulingana na sheria za nchi, pia amesema Serikali itaendelea kuongeza bei ya karafuu.View attachment 2862293View attachment 2862295View attachment 2862296View attachment 2862297View attachment 2862298View attachment 2862299View attachment 2862300View attachment 2862301View attachment 2862302
Mambo ya Kuokota vichwa Vya Treni
 
ujinga ujinga tu, karafuu ya m140 mpaka Rahisi naye akaione, hiyo ni kazi ya mkuu wa kituo na hao watu wa operation huko baharini.

Rais ni taasisi kuuubwa inayopaswa kufanya na kucoordinate issue kubwa kubwa zenye impact kuuubwa kwa Taifa na haya mengine nikugawanya majukumu kwa watu wachini kabisa huko..

Kuna haja ya kutengeneza Job description ya Urais hata kwa kuomba ushauri huko USA na mataifa mengine halafu ndio zitumike hapa.
 
Kwa uelewa wangu mdogo kitu chochote kinachomhusisha rais kinachukuliwa kwa uzito mkubwa zaidi,ukiangalia dhima kuu ya hii habari wananchi kukumbushwa kuhusu ubaya wa kufanya magendo ya karafuu.kwavile rais mwenyewe kaliongelea na kalikataza imebeba ujumbe mzito kwa wafanya magendo
 
Yan Rahisi mzima anakimbizana na tani 9 tu za karafuu? Si bora angeenda kuangalia mpira kwenye Uwanja wake mpya wa Amaan🤷
 
Back
Top Bottom