Magufuli anapogeuka mtetezi wa mafisadi

Magufuli anapogeuka mtetezi wa mafisadi

Mbona Na sisi ukawa tunamlinda kwa nguvu zote Yule tuliezunguka tukimtangaza n fisad papa
kwaio unakiri kwamba redbrigade yetu wana nguvu na mamlaka ya sio tu kumlinda pia kumkingia kifua hili asikamatwe na jeshi lenu la polisi,jwtz,tiss,mahakama na magereza?
 
Umesahau kumtaja na lowasa na sumaye, wote watendaji wakuu katika huo uongozi but sinnce walipotoka huko naona ufisadi umewaisha
Hao hawalindwi na katiba bila shaka. Nina hakika pia hawamo kwenye orodha ya walioahidiwa ulinzi. Wapelekeni mahakamani hata leo.
 
wajinga nyie mnalalama badala ya kurudi bungeni kutetea uchafu kama huu usipite sasa unalalama nini? acha wapitishe tu ukawa bana tumewachoka pumbafu zenu.
mkuu vp mbona jazba na povu dizaini.. au ndo ishara ya kuzidiwa na kukosa hoja?
 
Mbona hata wewe Magufuli anakulinda kuhakikisha unaishi kwa amani na utulivu kwani umefanya makosa.
"Watachonga saaaaaaaaaana lakini hata wakisema msijali, tupa kule..Mimi mtoto wenu ninawahakikishia ulinzi hata kama iweje..."

Nina hakika maneno haya hayamaanishi ulinzi dhidi ya vibaka na wezi na majambazi... ambao hata hivyo juhudi zake ni ndogo sana ukilinganisha na juhudi za hao 'walinzi' kuilinda jamii dhidi ya mikutano ya chadema.
 
Ahahaha ulidhani atapambana na mafisadi? Hile ilikua ni gia ya kupata kura.
Wenye macho tushaona jinsi anavyopambana na ufisadi. mfano mmoja tu ni watumishi hewa. we endelea kulialia tu na kufunika midomo na makaratasi.
 
Like it or not hapa ni kuishiwa substantive argument. And Iam wondering, kwani kukaa kimya ni dhambi!!
Ndugu, let's wait and see. Bahati nzuri madhara ya matatizo kama haya mwisho wa siku hayachagui. Yanaweza kubagua at Party level lakini huo unakuwa mwanzo tu. Inapofikia hatua ya 'yaliyotabiriwa kufika' shati na tisheti ya kijani haitamsaidia mtu. Tutalia wote, japo wenzetu mtatafuta vijisababu vya kusingizia ili mhusika mkuu alindwe. Hili sihitaji ubishi maana nimesema tusubirie tuone. Usitake tuishi ya mwakani kwa maneno leo hii. Twende taratibu, ikifika 2018 kwa spidi hii, tutaongea vizuri.
 
Wenye macho tushaona jinsi anavyopambana na ufisadi. mfano mmoja tu ni watumishi hewa. we endelea kulialia tu na kufunika midomo na makaratasi.
Watumishi hewa ni mafisadi? Hao ni vidagaa kuna mapapa wakubwa kama kina Lugumi,masamaki wanadunda mtaani
 
Maajabu hayamuishi rais wetu Magufuli. Niliipoona mswada wa mahakama ya mafisadi unapelekwa bungeni nikajua kinachofuata ni kubadili kipengere cha katiba kuwaondolea kinga marais wastaafu ili mahakama ya mafisadi iwamulike Rais mstaafu mzee Mkapa na Mzee Kikwete.

Na hata nikaamini kwa kile kiapo cha wabunge wa CCM kupambana na mafisadi, wataweka hoja hiyo ya kubadili kipengere cha katiba ili ukweli ujulikane dhidi ya Mkapa na Kikwete. Ajabu Rais Magufuli anawakingia Kifua tena kwenye majukwaa kwamba atawalinda wasihofu. Kauli ya kusema atawalinda ni kuhalasha makosa yao.Unawezaje kumlinda mtu asiye na makosa?

Magufuli ndugu yangu dunia inakutazama jinsi unavyojichanga kwenye hii vita ya Mafisadi. Wewe mwenyewe umekuwa ukikili mizigo mizito ulioachiwa na Kikwete
Sunzu, nadhani Mh. anaeleweka tusiseme mengi. Wazungu wako mbali naye wanawezekana wasimuelewe, lakini wewe na mimi and the Tanzania public in general wanamuelewa, labda wale wa mrengo mwingine (au na wao wanamuelewa and this is most likely) ambao wanaweza kujitoa ufahamu.
 
Hii nchi wakati inapata uhuru hakukuwa na mafisadi.Chama kilichopewa dhamana kuongoza nchi ndio kiliamua kwa makusudi kuanzisha mfumo wa kifisadi na mafisadi.Hivi leo mzazi anaweza kumpiga panga mwanae?
 
Hao hawalindwi na katiba bila shaka. Nina hakika pia hawamo kwenye orodha ya walioahidiwa ulinzi. Wapelekeni mahakamani hata leo.
Mnyika, lissu na lema waanze kuwapeleka maana wao ndiyo walituambia kuwa lowasa ni fisadi na wanaushahidi 8years walituaminisha hvyo, sumaye alikubali kuhusu uuzwajwi wa nyumba za serikali na alikiri,
 
Zero kama mwenyekiti wako hujitambui.
Hajitambui kwa hoja ipi.. Mbona zile pale points tupu ndugu? Acheni ushabiki usio na tija.. Kama wewe ni mwema ruhusu watu waseme mwisho wa siku watanyamaza wenyewe wakiziona kazi zako nzuri. Mwenyewe utakuwa unajifunza coz hakuna kiongozi aliekamilika!!
 
Watumishi hewa ni mafisadi? Hao ni vidagaa kuna mapapa wakubwa kama kina Lugumi,masamaki wanadunda mtaani
ufisad uliofanywa hili suala la watumishi hewa ni zaid ya escrow na Richmond. fikiria kila mwezi likuwa inapigwa 26billion, kwa miaka mitano ni sh ngapi????ni zaidi ya 1.5trillion. (kama unajua hesabu za kuzidisha umeshapata jibu). wakati escroe haikufika hata 400b, Richmond sina record sahihi lakin naamin haikufikia huko.

we unataka ufisadi gani tena mkubwa zaidi ya huo???

njoo na record ya lugumi kala sh ngapi tulinganishe na hiyo wa watumishi hewa.
 
CCM inasema Chadema imewapokea mafisadi lakini juzi tumesikia wakubwa watalindwa Kwa gharama zote ahaaaa
 
Hv mpaka sasa fisad gan kakamatwa vile!
Fisad gan kafungwa??
 
Back
Top Bottom