Magufuli 'anajihujumu' mwenyewe...

Magufuli 'anajihujumu' mwenyewe...

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,615
Kuna vitu Rais yoyote akifanya ni rahisi mno kutengeneza maadui wapya weengi mno

La kwanza ni kuongeza kodi

La pili ni kupiga marufuku 'watu wasiongee'

Kiongozi yoyote akifanya hayo ni dhahiri upepo utabadilika na 'atachukiwa'
haraka mno.

Huhitaji hata vyama vya siasa kubadili huo upepo.

Sasa kama kuna watu wa kumshauri Magufuli, basi wamueleze tu ukweli.

Kwanza awe makini na kupandisha kodi.

Kodi na tozo za biashara mbalimbali zimepandishwa kiholela.

Na sasa watu hawaruhusiwi hata kufanya mikutano, wala makongamano
wala kukosoa kwenye media, hivi vitu viwili vinaweza kufanya Serikali
kutumia 'Jeshi la Polisi' kila siku na kila wakati.

Kuna gharama kubwa mno Serikali itaingia ili kuimarisha Jeshi la Polisi
na kuliweka ready kila siku kwa mambo ambayo busara kidogo ingetumika
kusingekuwa na ulazima.
 
Majizi Chadema mnatapatapa sana.

Kila saa Magufuli Magufuli hakauki midomoni mwenu.

Shem to you
Epuka kuchanganya haya madude
1471970651726.jpg
 
Huwezi kupigana na ukuta kama upotimamu kiakili jamani kwani wahenga walisha tuambia kuwa
Mpiga Ngumi ukutani huumiza mkonowe!!!

Ni methali za zamani lakini watu hawa wanashindwa kuelewa
 
Ni kweli kabisa mkuu.. Mfano mzuri niliona bagamoyo stend kodi imetoka 500 per day mpaka 2000 per route.. Kulikua na mgomo ambao ulishindikana kusolve mpaka muda wa jion naondoka hapo.. Hebu angalia hilo niongezeko la tozo kwa asilimia ngapi ?? Tena limewekwa bila kushirikisha wadau/walipa tozo wenyewe...
 
Huyu Magufuli mimi simwelewi kabisa siku hizi.

Alipoanza kuna baadhi ya mambo nilimuunga mkono.

Lakini sasa hivi naona haeleweki kabisa.

Bada ya kupiga kazi tu anaishia kukimbizana na CHADEMA.

Tatizo lake ni nini?

Hana ustahmilizu wa kukosolewa?
 
Kwa mahahara wa laki 2.5 ni lazma wauze mechi.
Ndio wasiwasi wangu tu huo, si wakuwaamini sana! Wale Polisi watiifu sidhani kama bado wengi kiasi hicho! Wale wa Misri waliuza game kipindi kile hahaahahaaah tusifike mbali. Niko kwenye maombi ya mfungo Mungu atuepushe na mambo haya
 
Huyu Magufuli mimi simwelewi kabisa siku hizi.

Alipoanza kuna baadhi ya mambo nilimuunga mkono.

Lakini sasa hivi naona haeleweki kabisa.

Bada ya kupiga kazi tu anaishia kukimbizana na CHADEMA.

Tatizo lake ni nini?

Hana ustahmilizu wa kukosolewa?

Ni kama anaonekana akikosolewa 'ataaibishwa'
hajui kukosolewa ni 'lazima' nyakati hizi
Hata akigawa chakula bure kwa Watanzania
kumkosoa hakuepukiki
 
Huwezi kupigana na ukuta kama upotimamu kiakili jamani kwani wahenga walisha tuambia kuwa
Mpiga Ngumi ukutani huumiza mkonowe!!!

Ni methali za zamani lakini watu hawa wanashindwa kuelewa
It more active in social media...I can assure you!
 
Ni kama anaonekana akikosolewa 'ataaibishwa'
hajui kukosolewa ni 'lazima' nyakati hizi
Hata akigawa chakula bure kwa Watanzania
kumkosoa hakuepukiki

Sijui anataka watu wamwogope...?

Eti yeye hajaribiwi...kwani yeye nani? Mungu?

Keshaanza kuniboa sana kwa kweli.

Badala ya kukimbizana na majizi na mafisadi kabakia kutisha wananchi.
 
Back
Top Bottom