Camilo Cienfuegos
JF-Expert Member
- Apr 23, 2015
- 19,234
- 68,270
Kuna vitu Rais yoyote akifanya ni rahisi mno kutengeneza maadui wapya weengi mno
La kwanza ni kuongeza kodi
La pili ni kupiga marufuku 'watu wasiongee'
Kiongozi yoyote akifanya hayo ni dhahiri upepo utabadilika na 'atachukiwa'
haraka mno.
Huhitaji hata vyama vya siasa kubadili huo upepo.
Sasa kama kuna watu wa kumshauri Magufuli, basi wamueleze tu ukweli.
Kwanza awe makini na kupandisha kodi.
Kodi na tozo za biashara mbalimbali zimepandishwa kiholela.
Na sasa watu hawaruhusiwi hata kufanya mikutano, wala makongamano
wala kukosoa kwenye media, hivi vitu viwili vinaweza kufanya Serikali
kutumia 'Jeshi la Polisi' kila siku na kila wakati.
Kuna gharama kubwa mno Serikali itaingia ili kuimarisha Jeshi la Polisi
na kuliweka ready kila siku kwa mambo ambayo busara kidogo ingetumika
kusingekuwa na ulazima.
The boss una maoni