Magufuli anaiga kwenye ilani ya CHADEMA

Magufuli anaiga kwenye ilani ya CHADEMA

Mi kwa kweli sijaelewa tatizo la ilani za vyama liko wapi!kwani matatizo ya watanzania ambao kama chadema au Chama chochote kilichoweka mgombea wa Urais wakipata madaraka matatizo yanatatuliwa kwa kulenga uanachama na wale ambao si wanachama wa hicho Chama wanaendelea kubaki na shida zao au inakuwaje?
 
Thats just political reasoning, hivi ata unajua maana ya political manifesto. Mtu yeyote mwenye malengo ya kuwekeza lazima akate sehemu ambazo anaona hakuna tija na kutumia hayo mapato sehemu zingine kutokana na ilani ya chama chake au malengo yake; its just commonsense kutokana na uhalisia wa mapato ya nchi.

Kuiga ilani ni kutumia sera za chama kingine kwenye vitu ambavyo vinaenda kuwapa watu impact ya moja kwa moja kama sera au kubadilisha muundo wa serikari kuongeza ufanisi wa kazi sasa CDM kuna lolote wanalolifahamu vinginevyo wangeuliza sera za Lowassa zinawezekana vipi given the current national income.
 
Nimesoma ilani ya CHADEMA na kuona mambo yote anayojaribu kuyafanya Magufuli mpaka sasa yapo kwenye ilani ya CHADEMA ya 2015-2020 na wala sijayaona kwenye ilani yake CCM.

View attachment 305632

Wewe mburula kweli kweli, maendeleo yanakuja kwa mbinu mbali mbali ikiwemo ya kuiga mambo mazuri wanayofanya waliopiga hatua kimaendeleo. Nampongeza Dk Magufuli the President kwa kuiga (kama ni kweli) mambo mazuri yaliyo kwenye ilani ya chama chochote cha siasa kwani naamini lengo la vyma kushika dola ni kuwaletea watu maendeleo
 
Siku zote wanasiasa MASLAHI huwa wanachoomba ni matatizo ya wananchi yadumu ili waendelee kuyatumia kama MTAJI wa kisiasa.WASAKA MADARAKA.
 
CCM hawanaga sera. Taarab tu na mipasho ndio mwisho wa akili zao.
Muache aige. The last time waliiga sera ya katiba mpya wakavurunda tu!
 
hakuna jambo la ajabu hapo Magufuli ana angalia namna bora ya kudhibiti matumizi
 
Ni hivi nyie hamjui kinachotendeka ndani ya ccm , Lowasa ndani ya Magufuli Lowasa a nao ngoja nchi
M nacho bishana ni kipi
 
Jaribu kufuatilia maisha ya kisiasa ya wanasiasa maarufu duniani. Ni jambo la kawaida kuiga mawazo ya wapinzani kama yana tija kwa taifa. Sasa asifute safari za nje kwa sababu ni wazo la CHADEMA? Always Tanzania kwanza. Long after CHADEMA (or any other political parties) and their cronies are gone, Tanzania itakuwepo. Daima tukumbuke hili.
 
sasa ulitaka aige mabaya yakupiga dili au? yaan hawa watu sijui wana mwezi mchanga! mtu akifanya mambo wananchi walopendekeza ni shiida akiyaacha ni shida mlitaka ajinyee pale ikulu ili mseme ni mgonjwa?
 
Hilo linathibitisha Dr. JPM ni Rais wa WaTanzania na ni wa Vyama vyote, makabila yote na dini zote.

Hata ACT wamempongeza. Aidha alipokuwa akijinadi alisema wana UKAWA wampe kura na atashirikiana nao.

Huo ni mwanzo tuu, ataendelea kuchukua Yale yote yanayofaa kwa mustakabali wa nchi yetu.

HAYO NDIO MABADILIKO YA KWELI.

Queen Esther

Nimesoma ilani ya CHADEMA na kuona mambo yote anayojaribu kuyafanya Magufuli mpaka sasa yapo kwenye ilani ya CHADEMA ya 2015-2020 na wala sijayaona kwenye ilani yake CCM.

View attachment 305632
 
Nimesoma ilani ya CHADEMA na kuona mambo yote anayojaribu kuyafanya Magufuli mpaka sasa yapo kwenye ilani ya CHADEMA ya 2015-2020 na wala sijayaona kwenye ilani yake CCM.

View attachment 305632

Sioni ubaya juu ya hilo,kama lina faida na manufaa kwa Taifa acha alifanye. Kwa maana manufaa yake yatawahusu watanzania wote bila kujali itikadi zao.
 
Nimesoma ilani ya CHADEMA na kuona mambo yote anayojaribu kuyafanya Magufuli mpaka sasa yapo kwenye ilani ya CHADEMA ya 2015-2020 na wala sijayaona kwenye ilani yake CCM.

View attachment 305632

Binafsi siwezi kuona ajabu kwa hilo,swala ni kazi ziende kwa usahihi
 
Back
Top Bottom