Magufuli amekosea wapi, mbona 'anachuja' haraka?

Rais ana mapambano magumu Tumuombee tusiangalie mapungufu tu na kucheka hakuna mtu ambae yuko perfect Tumshauri pia .
 
Wewe ni mgeni huko Mwanza? Kwa miaka sasa nimekuwa natambua Mwanza ni mji wa wajajanja au ndio wewe uliyepelekwa kudeki barabara wakati wa kampeni?
Sheria ya uhujumu uchumi inakifungu kinachokataza mfanyabiashara kuhifadhi bidhaa bila ya kuiuza kwa lengo la kusababisha upungufu wa bidhaa hiyo. Hili ni kosa la jinai hivyo swala la kuchunguza nia ovu ni muhimu. Hivyo vuteni subira uchunguzi ufanyike watu hao watapelekwa mahakamani au kuachiwa huru kwa kushindwa kuthibitisha nia ovu.
Kama godauni husika huwa linauza tani mia tano kila siku ghafla anaanza kuuza tani tano kwa siku kisha anasema hakuna sukari wakati ndani ya godauni kuna tani elfu ishirini. Hapa kosa linakuwa limetendeka ila nia haijulikani. Huyu mtu atakamatwa kwanza halafu ndipo nia yake ichunguzwe kutokana na utetezi wake. Naamini hata kama ukuwa mjinga vipi utakuwa umenielewa.
Miaka ya nyuma ukanda huo ulitoa maprofesa wanane enzi za utawala wa Mwl Nyerere na Mwinyi. Sasa hivi eneo hilo linatoa wajinga wengi mpaka inatisha.
 
Siku zinahesabika lazima achuje haraka kwani hakujipanga kuwa raisi.c unajua ka kaimu nafasi ya mwingine aliyejipanga kuwa raisi kwa mda mrefu
 
 
Siku zinahesabika lazima achuje haraka kwani hakujipanga kuwa raisi.c unajua ka kaimu nafasi ya mwingine aliyejipanga kuwa raisi kwa mda mrefu
Tatizo la kukaimu huonekana pale ambapo anayekaimishwa hakuwahi kuwa karibu na anayeondoka kwa hiyo anakuwa haijui sana ofisi aliyopewa inavyofanya kazi.
 
upinzani ndio ume to let down, it seems for 20 yrs they dont know how to win election..pity
Duh, let me reserve my comments for now...yaani CCM ishindwe kazi, lawama zielekezwe kwa upinzani! It is hard, really hard, to believe this kind of response comes from the Waberoya I knew sometime back. Si ajabu idadi ya waliochuja ni kubwa na inazidi kuongezeka, what a pity!
 
Kwa hoja ulizoandika, asilimia kubwa kesi hizo kama zitafunguliwa zitatupiliwa mbali. Justification ya kuficha kwa mtu mwenye godown utathibitisha vipi. Halafu huwez kusema trend ya kuuza kubadilika imtie mtu hatiani. Naona ni dosari kubwa kama kweli mwendesha mashataka atafungua kesi kwa nadharia uliyoandika. Anyway tusubiri ila mengine yanakuzwa na kuongezewa tension bila sababu.
 

Mkuu umewasilisha ukweli. Utawala wa sheria unapuuzwa. Tukiendelea kumsifia tu bila kusema ukweli kama anavyopenda nchi haitapiga hatua ya maana ya maendeleleo. Tumwombe Mungu amsaidie aongoze nchi yatu kwa haki ili kusudi amani itamalaki.
 
Mwanzoni mwa utawala wake ilikuwa kila gazeti linamwandika yeye tena vizuri. Vijiwe vyote kuanzia vya kahawa, daladala, bar na maofisini story alikuwa ni yeye tena watu wakimsema kama malaika mkombozi.

Amegundua na yeye ni jipu
 
Hivi kuna mtu anaamini magufuli ataleta mabadiliko akiwa ndani ya ccm???

Hii nchi hovyo kweli
 
Ni kweli hayo yanaweza kutokea iwapo upande wa mashitaka utakuwa na hoja nzito ambazo zitaizidi za utetezi. Pia hoja za utetezi zaweza kuzidi. Chamsingi hapa ni kwamba kitendo kinachokatazwa na sheria kimetendeka. Kuhusu kupata hukumu nzuri ni swala lingine. Hivyo kitendo cha kukamata kipo sahihi kufanyika.
 
nimekuelewa mkuu
 
Ni kweli mkuu. Nilikuwa nawaambia watu kuwa Magu ni mzuri kuwa mtendaji chini ya boss badala ya kuwa Rais kwa sababu yeye sio "mwanasiasa" wakawa wananibishia.
Nimempa miaka 2 kumtathmini.
Wananchi tunaumia kiuchumi. Let's wait, time will tell
 
Hao wanaojichanganya kimajukumu wamejuzwa majukumu yao na aliyewateua?
Kama hakubainisha mipaka ya majukumu yao nani alaumiwe?
 
Hao wanaojichanganya kimajukumu wamejuzwa majukumu yao na aliyewateua?
Kama hakubainisha mipaka ya majukumu yao nani alaumiwe?

Sio rais anayetoa majukumu ya anaowateua, ipo tume ya utumishi hii ndio Ina majukumu ya kuanisha wajibu, mamlaka,majukumu na kadhalika.
Rais anateua tu hivi vyeo vipo kikatiba ILA kwa kuwa Mara nyingi watu hubaki na vyeo na sio wajibu na majukumu ya cheo husika.
 
Nimekupata.
Je, hiyo tume inawajibika kwa nani?
Je, Rais anayajua majukumu yao?
Kama anayajua majukumu yao, mbona hawaonyi/kuwakanya wanapoingiliana kimajukumu?
 
Mtu ukichuja mara nyingi huwa na hoja zilizochuja kama hii ya mleta uzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…