Magufuli akumbwa na kashfa nzito!

Magufuli akumbwa na kashfa nzito!

Status
Not open for further replies.
Joined
Dec 11, 2010
Posts
3,321
Reaction score
6,331
Hii imetoka kwenye hotuba ya kambi ya upinzani. Sehemu hii inaonyesha ubadhirifu wa fedha kwenye wizara iliyoko chini ya Dr John Pombe Magufuli.

Mheshimiwa Spika, baada ya fedha hizi kupunguzwa kiasi cha shilingi bilioni 95 na kupelekwa wizara ya uchukuzi zilibakia kiasi cha shilingi bilioni 252.975 katika kifungu hiki, leo tumelazimika kulikumbusha Bunge kuhusiana na suala hili kwani kwa mujibu wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya mwaka husika wa fedha kuhusiana na kifungu hiki alisema, naomba kunukuu "malipo ya madeni ya mwaka wa nyuma yaliyolipwa kwa fedha za 2011/2012 kwa kutumia jina la mradi usio halisi Tshs. 252,975,000,000.

Miradi katika wizara ilipewa namba 4168 kwa ajili ya kupitisha malipo ya madeni ya miaka ya nyuma kwa miradi inayotekelezwa na TANROADS. Namba hii sio halisi" (chanzo: taarifa ya CAG uk.160,fungu 98)

Mheshimiwa Spika, fedha hizi "zilizopotea"au "kulipwa kifungu hewa" ni sawa na fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya barabara ifuatazo kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014;

i. Barabara
ya Usagara-Geita-Kyamyorwa
(KM 422)

ii. Barabara
ya Kigoma-Kidahwe-Uvinza-
Kaliua-Tabora (KM 443)

iii. Barabara
ya Nangurukuru-Mbwemkulu
(KM 95)

iv. Barabara
ya Sumbawanga-Matai-Kasanga
Port (KM 112)

v. Barabara
ya Manyoni-Itigi-Tabora (KM264)

vi. Barabara
ya Tabora-Ipole-Konga-Mpanda
(KM 359)

vii. Barabara
ya Kidatu-Ifakara-Lupilo-Malinyi-
Londo-Lumecha/Songea(KM-396)

viii. Kuondoa
msongamano barabara za Dar
(KM-102.15)

Aidha, ni sawa na kusema kuwa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 316.218 imepotea kwa kutumia mahesabu ya wizara ya ujenzi kuwa kilomita moja ya lami inajengwa kwa kiasi cha shilingi milioni mia nane (800,000,000), hii ni sawa na kusema kuwa barabara ya kutoka Manyoni-Itigi-Tabora (KM 264) Changanya na barabara ya kutoka Chunya – Makongorosi (KM 43) na Barabara ya Tangi Bovu –Goba (KM 9), zimepotea kutokana na ufisadi huu.

Chanzo: Hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni
 
Linganisheni majibu yao Bungeni na yale waliyompelekea CAG kuhusiana na suala hilo then mjitafakari upya kabla ya kufikia hitimisho, huyu jamaa ni mwizi kama walivyowengine tu,soma hotuba hii ya upinzani;
 
Jmn........hadi Mr MAKUFULI!!!!?
 
Hata hivyo mimi huwa sina imani na Magufuli,naona ni mpiga kelele tu,na siku hiz kaharibika zaidi,ni mpigaji tu nae.

Kuna mwanafalsafa mmoja alishawahi kusema "Kinacho ingia kwenye taka nacho ni taka", kwa mantiki hii ni kwamba kama CCM ina uchafu, wote wanao andama nayo pamoja na uchafu wake hawawezi kuwa wasafi watachafuka au watajichafua wafanane na wenzao wachafu ili wote wawe wachafu.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums.
 
HAdi hii miaka yao mitatu iishe tutabaki kama kuku aliyenyonyolewa...
 
huu ni uzushi, hakuna ukweli wowote hapo...hizi ni takwimu za kupakana matope na hazitafanikiwa
 
Halima Mdee amesema wazi bungeni kuwa CHADEMA wanamkubali sana Magufuli na Mwakyembe
 
Vote 98: Ministry of Works
Payment made through dummy project worth Shs.252,975,000,000
The Ministry paid a sum of Shs.252,975,000,000 through unspecified project with dummy code No.4168. It was alleged that this amount was used to pay previous year's
contractual liabilities for projects which were implemented by TANROADS. However, we were not provided with a detailed analysis of these liabilities. In addition, the amount paid was not disclosed as a previous year's liability in the financial statements.


Ina maana Magufuli hakuwa na majibu kwa Vijana wa CAG, ila hapa bungeni atapata majibu maana kule kwa CAG hakuna siasa ila bungeni ni mahala pake
 
mtahangaika sana kumchafua pombe lakini itawamwagikia tu na mtanuka wenyewe
 
Barabara anazojenga Magufuli zote hazina viwango, mashimo baada ya miezi miwili huku gharama za kujenga ziko juu (800,000,000 kwa kilomita moja). Huyu jamaa utasikia anapigiwa chapuo la kuwa rais kwa huu ubabaishaji na maCCM wenzie. CCM hakuna mwenye afadhali jamani, ngoja tusubiri utetezi wake kwa hizo hela alizokwapua
 
ni bora kuhangaika na mengine kuliko kupoteza muda kumchafua mtu asiyechafulika
 
Huyu jamaa nilimshuhudia kwa macho yangu akichukua kipisi cha Nondo anaikagua barabara kwakuigongagonga, na hakuridhika na kumwambia Mkandarasi aliyeijenga barabara hiyo anampa miezi 6 awe ameibomoa na kuirudia upya na kua na kiwango kinachoridhisha ama sivyo anamtimua na hela arudishe!

Chezea John Pombe weyee!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom