Magufuli aendelea kutumbua Majipu: Mkurugenzi Hospitali ya Ocean Road Asimamishwa

Nadhani kuna haja ya kuangalia upya suala la madaktari kuwa na hospitali zao binafsi na maduka ya dawa. Hili bila kupepeta macho lina mgongano mkubwa wa kimaslahi

Kabisa. Akiwa Mkurugenzi kuna machine za mionzi zilitoweka pale Ocean Rd. Katika vetting ya viongozi wa Muhimbili, Ocean Rd, Rufaa zote, hospital za mikoa na wilaya, vituo vya afya na zahanati, mwenye hospital binafsi au duka la dawa awe disqualified.
Ni rahisi kuwajua maana wametumia vyeti vyao kufungua hospital au maduka ya madawa.
Itabidi daktari achugue kipi anataka. Na waruhusiwe kufungua hospital zao baada ya kuitukia serikali miaka kadhaa.
 
Haitaishia kwenye afya tuu, itendelea na bungeni , mbunge asifanye biashara wala kuwa mkurugenzi wa kampuni kwani kunaweza kuwa na mgongano wa maslahi.
 
.....nimeuguza mgonjwa wa saratani akiwa ni mke wangu. napaelewa sana hapo na michezo yao. ni dhulma kubwa inayoendelea katika taasisi hizi za umma. Chemotherapy zinachakachuliwa hivi hivi tunaona. member kama Lwesye hawezi kujua !

Kwa yeyote ambaye amepitia adha za Ocean Road ni ngumu sana kumkosoa Ummy kwa hatua aliyochukua. Mgonjwa anapokuwa ktk hatua ya kupigwa mionzi walau kuna unafuu maana mionzi inapigwa bure. Kilio cha wengi kipo kwenye hatua ya chemotherapy. Mgonjwa anaweza kupangiwa drip 3, 4, 5 ama zaidi. Sasa kila moja dawa zake zinagharimu kuanzia laki 3 mpk laki nane kutokana na uzito wa ugonjwa. Na hapa ndipo wenye kujuana na madaktari kwa rushwa hupewa dawa kwa mlango wa nyuma. Lakini asilimia kubwa hukatisha dozi na kurudi mikoani kwao. Hali ni tete Ocean Road
 
To be honest, naona kuna maamuzi ya mihemko hapa. Kama Wizara iliridhia watumishi kuwa na vituo binafsi, hivyo kwa cheo chake kumiliki kituo kuna mgongano wa maslahi basi hatua stahiki ni kumvua madaraka, sio kumsimamisha kazi.
Kama kuna kosa lingine linatakiwa libainishwe kwa uwazi na liwe na substance ya kusimamishwa kazi sio sababu za kuunga unga.

makosa haya yalifanyika wakati nchi haina kiongozi
 
Kwani hiyo bodi ya Ocean Road na mamlaka iliyompa Madaraka ya Ukurugenzi Dr Msemo kweli hawakujua huyu jamaa ana clinic yake ya cancer kwa zaidi ya miaka 5. Nachopendekeza kabla ya kumsulubu Dr Msemo ni vyema mkamtumbua Jipu Dr Mbando Katibu Mkuu wizara ya Afya na Bodi ya Ocean road.

Wanajua ila nao ni majipu
 
Kabisa. Akiwa Mkurugenzi kuna machine za mionzi zilitoweka pale Ocean Rd. Katika vetting ya viongozi wa Muhimbili, Ocean Rd, Rufaa zote, hospital za mikoa na wilaya, vituo vya afya na zahanati, mwenye hospital binafsi au duka la dawa awe disqualified.
Ni rahisi kuwajua maana wametumia vyeti vyao kufungua hospital au maduka ya madawa.
Itabidi daktari achugue kipi anataka. Na waruhusiwe kufungua hospital zao baada ya kuitukia serikali miaka kadhaa.

Kweli kabisa, hakuna namna aisee, nadhani kina Ummy Mwalimu wanapitia humu wataona haya mawazo
 
Bado wanazungukazunguka tuu. Chamsingi hapa ni kuboresha Maslahi ya Watumishi ikiwa ni pamoja na Mishahara ili wafurahie kazi kama wao.
 
Natamani majipu yatumbuliwe kwa kutoa hadi kiini cha jipu sio usaha tu! Mfno wa TAKUKURU nilitamani waivunje yote waiunde upya!

kuwa Na busara. Watumishi wa chini wanakosa gani? kama wao wanapata maelekezo au wanabinywa ktk kufanya jambo flani nani wa kulaumiwa!? mbona Kiini cha jipu kiliisha ng'olewa na mtumbuaji
 
To be honest, naona kuna maamuzi ya mihemko hapa. Kama Wizara iliridhia watumishi kuwa na vituo binafsi, hivyo kwa cheo chake kumiliki kituo kuna mgongano wa maslahi basi hatua stahiki ni kumvua madaraka, sio kumsimamisha kazi.
Kama kuna kosa lingine linatakiwa libainishwe kwa uwazi na liwe na substance ya kusimamishwa kazi sio sababu za kuunga unga.

Uko sahihi lakini ukisoma barua ina utangulizi wenye maana pana zaidi. Mgongano unaoelezwa unaweza kuwa umezalisha ubadhilifu. Mtu anapokuwa anatoa huduma bora kwa kliniki yake na hafanyi hivyo kwa mwajili, hiyo ina maana sana! Lakini pia kisiasa, tangazo kama hili linatia woga wale wenye lengo bovu badala ya kumuondoa, halafu aendelee na kliniki yake huku kwa mwajili asiwe anawajibika.
 
Sasa nchi nzima itajaa usaha , maana majipu yakitumbuliwa hutoa usaha, sasa kwa idadi ambayo yameshatumbuliwa na inavyoendelea usaha utazidi

Mbona ili si tatizo kwa nchi kama yetu iliyojaa maziwa, mito, na bahari? Usaha ukijaa maji lukuki tuliyonayo yatasafisha tu, hapa kazi iliyobaki ni kuzidi kutumbua majibu maji ya kutosha tunayo.
 
Alipofika ocean road alikuta upungufu mkubwa Wa dawa hali ya kuwa kumbukumbu za wiki tatu kabla zilionesha kiasi kikubwa cha dawa zilizopelekwa hospitalini ambacho hakiendani na dawa zilizokutwa hospitalini na zile walizopewa wagonjwa Wa saratani. Takwimu zilikuwa haziendani.

Jamani ma Doctors hawa wameuwa watu wangapi sasa wa cancer kwa ukosefu wa hizo dawa?
 
sijaandika hili kwa dharau wala msukumo wa degree yangu ya arts ila naongelea document ya serikali kwa ujumla..

am sorry siko kisiasa ila nikutaka kujua kama hivyo ndivyo inavyotakiwa kwa watumishi wa serikali kwa cheo cha uwaziri.

Hebu tueleweshe kwani saini ina formula maalum?
 
kuwa Na busara. Watumishi wa chini wanakosa gani? kama wao wanapata maelekezo au wanabinywa ktk kufanya jambo flani nani wa kulaumiwa!? mbona Kiini cha jipu kiliisha ng'olewa na mtumbuaji
Ok watumishi wa chini ni malaika hawana makosa. Hata rushwa zinazolalamikiwa na wananchi hasa katika police, mahakama, na sekta ya afya haziwahusu hawa malaika.
 
Back
Top Bottom