Savimbi Jr
JF-Expert Member
- Sep 23, 2011
- 6,819
- 9,172
Akianza kutumbua Tanapa na nssf ni tagini.
Nadhani kuna haja ya kuangalia upya suala la madaktari kuwa na hospitali zao binafsi na maduka ya dawa. Hili bila kupepeta macho lina mgongano mkubwa wa kimaslahi
.....nimeuguza mgonjwa wa saratani akiwa ni mke wangu. napaelewa sana hapo na michezo yao. ni dhulma kubwa inayoendelea katika taasisi hizi za umma. Chemotherapy zinachakachuliwa hivi hivi tunaona. member kama Lwesye hawezi kujua !
To be honest, naona kuna maamuzi ya mihemko hapa. Kama Wizara iliridhia watumishi kuwa na vituo binafsi, hivyo kwa cheo chake kumiliki kituo kuna mgongano wa maslahi basi hatua stahiki ni kumvua madaraka, sio kumsimamisha kazi.
Kama kuna kosa lingine linatakiwa libainishwe kwa uwazi na liwe na substance ya kusimamishwa kazi sio sababu za kuunga unga.
Kwani hiyo bodi ya Ocean Road na mamlaka iliyompa Madaraka ya Ukurugenzi Dr Msemo kweli hawakujua huyu jamaa ana clinic yake ya cancer kwa zaidi ya miaka 5. Nachopendekeza kabla ya kumsulubu Dr Msemo ni vyema mkamtumbua Jipu Dr Mbando Katibu Mkuu wizara ya Afya na Bodi ya Ocean road.
Kabisa. Akiwa Mkurugenzi kuna machine za mionzi zilitoweka pale Ocean Rd. Katika vetting ya viongozi wa Muhimbili, Ocean Rd, Rufaa zote, hospital za mikoa na wilaya, vituo vya afya na zahanati, mwenye hospital binafsi au duka la dawa awe disqualified.
Ni rahisi kuwajua maana wametumia vyeti vyao kufungua hospital au maduka ya madawa.
Itabidi daktari achugue kipi anataka. Na waruhusiwe kufungua hospital zao baada ya kuitukia serikali miaka kadhaa.
Natamani majipu yatumbuliwe kwa kutoa hadi kiini cha jipu sio usaha tu! Mfno wa TAKUKURU nilitamani waivunje yote waiunde upya!
To be honest, naona kuna maamuzi ya mihemko hapa. Kama Wizara iliridhia watumishi kuwa na vituo binafsi, hivyo kwa cheo chake kumiliki kituo kuna mgongano wa maslahi basi hatua stahiki ni kumvua madaraka, sio kumsimamisha kazi.
Kama kuna kosa lingine linatakiwa libainishwe kwa uwazi na liwe na substance ya kusimamishwa kazi sio sababu za kuunga unga.
Sasa nchi nzima itajaa usaha , maana majipu yakitumbuliwa hutoa usaha, sasa kwa idadi ambayo yameshatumbuliwa na inavyoendelea usaha utazidi
Alipofika ocean road alikuta upungufu mkubwa Wa dawa hali ya kuwa kumbukumbu za wiki tatu kabla zilionesha kiasi kikubwa cha dawa zilizopelekwa hospitalini ambacho hakiendani na dawa zilizokutwa hospitalini na zile walizopewa wagonjwa Wa saratani. Takwimu zilikuwa haziendani.
sijaandika hili kwa dharau wala msukumo wa degree yangu ya arts ila naongelea document ya serikali kwa ujumla..
am sorry siko kisiasa ila nikutaka kujua kama hivyo ndivyo inavyotakiwa kwa watumishi wa serikali kwa cheo cha uwaziri.
Ok watumishi wa chini ni malaika hawana makosa. Hata rushwa zinazolalamikiwa na wananchi hasa katika police, mahakama, na sekta ya afya haziwahusu hawa malaika.kuwa Na busara. Watumishi wa chini wanakosa gani? kama wao wanapata maelekezo au wanabinywa ktk kufanya jambo flani nani wa kulaumiwa!? mbona Kiini cha jipu kiliisha ng'olewa na mtumbuaji
hahahaha...baada ya jipu kutumbuliwa!. funny.Utasikia amestaafu