Binafsi sioni tatizo Dr. Magufuli kusambaza Ilani ya CCM kwa watendaji wa Wizara ya Ujenzi. Hofu yangu iko sehemu moja tu, JK ametoa ahadi nyingi sana zinazoangukia kwenye Wizara ya Ujenzi ambayo sasa itakuwa inashughulikia Barabara na Viwanja vya Ndege.
Nina mashaka unaweza kuwa mtego wa 2015, maana na yeye ni mmoja wa wanaohisiwa kuwa na nia ya kutaka kumrithi JK. Iwapo Magufuli atashindwa kutimiza Ilani ya CCM na Ahadi za JK, basi wapizani wake wanaweza kutumia hilo kama kigezo cha mtu aliyeshindwa na as usual watasema si mchapakazi. Mfano, JK ameadi Upanuzi/Ujenzi wa Viwanja 4 vya ndege [Bukoba, Kigoma, Mwanza na Mbeya] ndani ya miaka 5. Pia kuna barabara kibao ambazo ameahidi ndani ya miaka hiyo hiyo mitano. Iwapo Magufuli ataweza kutimiza hizo ahadi bila kuwa frustrated na serikali basi chati yake ya zama za Mkapa itarejea, iwapo atashindwa kutimiza hizo ahadi basi wabaya wake watasema kwamba ameshindwa ku-perform na hapo subiri scandals kutoka kwenye hiyo wizara.
Kitendo cha kuwaweka Mwakyembe na Magufuli kwenye wizara moja, kuna acha maswali kiaina. Inabidi waende vyema na ili kufikia malengo yao wanatakiwa kuifumua TANROADS maana sote tunajua mgogoro uliokuwepo kati ya Mrema [TANROADS], Bodi ya TANROADS na Wizara. Ili kufikia malengo lazima hizo pande 3 ziwe kwenye page moja, na hapo alipoanzia Magufuli ni mahali muafaka kwa maoni yangu. Mrema wa TANROAD alishaonyesha kuwa ni mkubwa kuliko Bodi ya TANROADS na mkubwa kuliko hata Wizara. Hilo likishughulikiwa kwa ukamilifu, barabara zitajengwa na Ilani ya CCM inaweza kutekelezeka. Labda kwa upande wa Viwanja vya Ndege hapo ndipo sijui taratibu zake.
NB: Wambea walikuwa wanasema Mrema aliwekwa na mafisadi na hata baadhi ya mabadiliko ya mkataba wake yalifanywa na aliyekuwa Waziri wa Miundo Mbinu [Mzee wa Vijisenti]. Mgogoro wa Mrema, Bodi na Wizara umedumu kwa muda mrefu sana na hakuna aliyekuwa na uwezo wa kumaliza mgogoro huo. Je, alikuwa analindwa na nani? Kwanini alikuwa na nguvu kuliko Bodi na Wizara? Je, Magufuli ataweza kumng'oa na hivyo kuifumua TANROADS yote?
Kila la Heri Dr. Magufuli, kumbuka kwamba umerudishwa hapo kwa kazi maalum, ama ya kukumaliza au kuirudisha CCM kwenye chati.