Magufuli aanza kazi Jumapili kwa vitisho, Kweli aanza vibaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magufuli aanza kazi Jumapili kwa vitisho, Kweli aanza vibaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Nov 28, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,741
  Trophy Points: 280
  taarifa ya habarii ya saa moja jioni ya leo ya TBC1, Waziri wa Miundo mbinu Dr. Magufuli amesambaza Ilani za uchaguzi za CCM katika hali inayonyesha anachapa siasa na kuwataka watendaji wote kwenye Wizara yake kuisoma, kuielewa na kuifuata..................au vinginevyo waache kazi au wataondolewa.....................

  Vile vile amesimamisha zoezi la ajira mpya TANROADS katika hali inayonyesha mwingiliano kati ya Bodi ya Wakurugenzi na Wizara Mama.............Kiutaratibu Wizara mama haipaswi kujiingiza katika shughuli za kiutendaji za TANROADS.................

  La kusikitisha zaidi ni sababu alizozitumia katika kuhalalisha Uongozi wa Wizara kuingilia zoezi la ajira mpya za Wahandisi wa Mikoa Wa TANROADS............alidai wao wanataka barabara zijengwe tu............................

  Magufuli anashindwa kuelewa ya kuwa ni sera ya TANROADS ili kuimarisha ufanisi ajira ni za mikataba na kama watendaji wataelewa ajira ni za kudumu hawatakuwa na motisha wa kuongeza ufanisi...............................Pia TANROADS ina kashfa nyingi za matengenezo bomu ya baraba ikilinganishgwa na fedha ambazo serikali hutumiwa kwenye shughuli hizo zikiongeza umuhimu wa kuubadilisha uongozi mzima wa TANROADS....................

  Mbaya zaidi, zoezi la mabadiliko ya uongozi ndani ya TANROADS yamekuwa yakipingwa na wabunge kwa sababu hizohizo za kujenga barabara wakati barabara nyingi ni bomu................hii yaashiria Regional Engineers na watendaji ndani ya TANROADS wana sauti kubwa kuliko hata Bodi yao ya wakurugenzi katika kuchalewesha mabadiliko ya uongozi ndani ya TANROADS kwa masilahi yao binafsi tu......
   
 2. A

  A Lady Senior Member

  #2
  Nov 28, 2010
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I cant really call them threats or a bad start. Its quite refreshing to see somebody with balls and spine, any balls(good or bad) just balls for a change. This country needs balls, people are too sheep like.
  Thats my view!
   
 3. jyfranca

  jyfranca JF-Expert Member

  #3
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 299
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Akirudisha nyumaba za serikali walizouziana kwa bei ya peremende ndo nasi tutamuamini
   
 4. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  It was not his cal.......i bet it was his BOSS. That guy is a hard worker n let him do it in his own way.........Am sure he'll deliver at the end of day.....
   
 5. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #5
  Nov 28, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Huyu atakuwa ni mfanyakazi wa Wizara au Tanroads.Naona tangu Magufuli ateuliwe kuwa Waziri wa Ujenzi ,wafanyakazi wa wizara ,Tanroads,contactors na wahandisi wa serikali wamekuwa wakija hapa JF na kumpaka matope Magufuli.

  Kama hamuwezi kufanya kazi chini ya Magufuli basi mjiuzulu
  .
   
 6. m

  masoudmwevi Member

  #6
  Nov 28, 2010
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  jamani walichofanya DR.Magufuli na DR.Mwakyembe nikuwaandaa watendaji wao kujipanga na speed yao mpya ya kiutendaji kazi so let us give them muda tuone impact ya utangulizi wa huu kama utakuwa na tija
   
 7. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #7
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Let him do whatever he believe will make them corrupted guys work without thinking of ten pacents. He might have his own weaknesses but mtoa maada seems anatoka tanroad
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Nov 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  The Tanzania National Roads Agency (TANROADS) is an Executive Agency under the Ministry of Infrastructure Development, established under section 3(1) of the Executive Agencies Act (Cap 245) and came into operation in July, 2000. The Agency is responsible for the maintenance and development of the trunk and regional road network in Tanzania Mainland.
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Nov 28, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mAGUFULI AMEANZA VIZURI SANA... ile ilani ndio mwongozo wake kichama na anachokumbusha tu ni alichotumwa kufanya, si kosa hata angekua wa CHADEMA ningempongeza inawa sijui kama kuna any implications

  Hilo la ajira na mambo mengine ya TANROADS, nadhani huko kuna siasa kuliko sehemu nyingine yoyote kwenye mambo ya ujenzi wa barabara na yeye kama waziri lazima awe na clown yake hapo, otherwise he will not be able to work with TANROADS, ukitaka kujua zaidi fuatilia shida za tanesco

  Bibafsi naona ameanza vizuri kwa kufunga paka kengele... Angekua ameamua kuteua mkurugenzi mpya yeye, then ningeogopa sana

  Utashibanyama naomba urejee facts zako upya
   
 10. Ikimita

  Ikimita JF-Expert Member

  #10
  Nov 28, 2010
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 302
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tanroads kuna matatizo mengi tu yanayohusiana na ajira na uongozi kwa ujumla. Mimi yuko sawa na hata hivyo yeye siyo mgeni kwenye hiyo wizara anajua alichodhamiria. Mwacheni afanye kazi.
   
 11. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #11
  Nov 28, 2010
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Mwisho wa siku watu wanataka kuona barabara zinajengwa. Kutokana ulegevu uliyokuwepo hapo ujenzi kwa miaka 5 iliyopita hizi constant bickering dhidi ya Magufuli kamwe watu hawatazielewa.
   
 12. P

  Patupetu Shekiu Member

  #12
  Nov 28, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Natamani Magufuli angekuwa ndiye kiongozi anaongoza huko ZNZ na muundo wao wa serikali ya sasa nikamuona na hiyo staili yake ya kusambaza ilani za uchaguzi za ccm akiwapa Maalimu Seif na wabunge wa cuf walio kwenye serikali ya mseto kuwa wange react vipi.
   
 13. K

  Keil JF-Expert Member

  #13
  Nov 29, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Binafsi sioni tatizo Dr. Magufuli kusambaza Ilani ya CCM kwa watendaji wa Wizara ya Ujenzi. Hofu yangu iko sehemu moja tu, JK ametoa ahadi nyingi sana zinazoangukia kwenye Wizara ya Ujenzi ambayo sasa itakuwa inashughulikia Barabara na Viwanja vya Ndege.

  Nina mashaka unaweza kuwa mtego wa 2015, maana na yeye ni mmoja wa wanaohisiwa kuwa na nia ya kutaka kumrithi JK. Iwapo Magufuli atashindwa kutimiza Ilani ya CCM na Ahadi za JK, basi wapizani wake wanaweza kutumia hilo kama kigezo cha mtu aliyeshindwa na as usual watasema si mchapakazi. Mfano, JK ameadi Upanuzi/Ujenzi wa Viwanja 4 vya ndege [Bukoba, Kigoma, Mwanza na Mbeya] ndani ya miaka 5. Pia kuna barabara kibao ambazo ameahidi ndani ya miaka hiyo hiyo mitano. Iwapo Magufuli ataweza kutimiza hizo ahadi bila kuwa frustrated na serikali basi chati yake ya zama za Mkapa itarejea, iwapo atashindwa kutimiza hizo ahadi basi wabaya wake watasema kwamba ameshindwa ku-perform na hapo subiri scandals kutoka kwenye hiyo wizara.

  Kitendo cha kuwaweka Mwakyembe na Magufuli kwenye wizara moja, kuna acha maswali kiaina. Inabidi waende vyema na ili kufikia malengo yao wanatakiwa kuifumua TANROADS maana sote tunajua mgogoro uliokuwepo kati ya Mrema [TANROADS], Bodi ya TANROADS na Wizara. Ili kufikia malengo lazima hizo pande 3 ziwe kwenye page moja, na hapo alipoanzia Magufuli ni mahali muafaka kwa maoni yangu. Mrema wa TANROAD alishaonyesha kuwa ni mkubwa kuliko Bodi ya TANROADS na mkubwa kuliko hata Wizara. Hilo likishughulikiwa kwa ukamilifu, barabara zitajengwa na Ilani ya CCM inaweza kutekelezeka. Labda kwa upande wa Viwanja vya Ndege hapo ndipo sijui taratibu zake.

  NB: Wambea walikuwa wanasema Mrema aliwekwa na mafisadi na hata baadhi ya mabadiliko ya mkataba wake yalifanywa na aliyekuwa Waziri wa Miundo Mbinu [Mzee wa Vijisenti]. Mgogoro wa Mrema, Bodi na Wizara umedumu kwa muda mrefu sana na hakuna aliyekuwa na uwezo wa kumaliza mgogoro huo. Je, alikuwa analindwa na nani? Kwanini alikuwa na nguvu kuliko Bodi na Wizara? Je, Magufuli ataweza kumng'oa na hivyo kuifumua TANROADS yote?

  Kila la Heri Dr. Magufuli, kumbuka kwamba umerudishwa hapo kwa kazi maalum, ama ya kukumaliza au kuirudisha CCM kwenye chati.
   
 14. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #14
  Dec 3, 2015
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  Mungu alijua kuwa utakuwa Mkuu wa Nchi utumbue majipu yaliyoshindikana.
   
Loading...