Wakati wa kampeni wa uchaguzi mkuu uliopita mgombea urais kupitia CCM ndugu Magufuli alitoa kauli mbiu kwamba Watanzania wakimchagua yeye ndiye ataleta mabadiliko (Magufuli for Change), mie binafsi sikuamini kama mgombea huyo wa CCM anaweza kuleta mabadiliko hayo.
Mheshimiwa Rais Magufuli kwa asilimia mia moja na amini ahadi uliyoitoa kwa Watanzania umetimiza kwa kasi kubwa sana na Watanzania wameliona hilo, hakuna binadamu aliyekamilika Mhe. Rais Magufuli anaweza kuwa na mapungufu lakini kazi aliyoifanya ni kubwa kubwa sana haswa kwa vita dhidi ya Ufisadi, matumizi mabaya ya fedha serikalini, nidhamu ya watumishi wa umma na nk.
Kwa hali iliyokuwa nayo Chama cha Mapinduzi mwaka jana kwasasa imani ya Watanzania imerudi kwenye Chama hicho. Ndugu zangu Watanzania kwa kila hali tumuunge mkono huyu kiongozi shujaa ili atuongozee kwenda kwenye Tanzania yenye matumaini, kweli hakuna mabadiliko yasiyokuja na maumivu yake ila baada ya maumivu kuna matumaini mazuri. Vijana ama wanaharakati wanaotumika vibaya kupitia mitandao ya kijaamii watafakari kwanza kutoa maoni ya kumbeza kiongozi huyu shujaa.