Magreth Sakaya ametambuliwa na Msajili wa vyama kama Katibu Mkuu wa CUF

Kwanini mnaitumbukiza CCM kwenye masuala ya CUF na msajili? Au ni chuki sisizo na msingi? Mbona alipo shinda Lema, hamkuisifia CCM kwa kumtoa Lema?
 
Mkuu Huu Udaktari wa Kweli au Mbwembwe Tu?? Wapi Nimetaja Chadema? Kwani Ukawa ni Chadema Siku Hizi? Nauliza tu
Yaani wewe bado unaamini kuna UKAWA? Hujui kuwa mwasisi wa UKAWA ni Mh. Lipumba hata hilo jina lilitengenezwa na Prof. Lipumba. Malengo (objectives) za UKAWA ziliwekwa wazi na zinajulikana.

Kila mwenye akili timamu anajua UKAWA haipo tena duniani. Hata watu makini kama Lowasa na Mbowe hawataji jina hilo kwani katika umoja huo alisha baki Mbatia tu na CHADEMA. Halafu UKAWA wala haikuwa chama cha siasa. Hivyo Seif akiamua kuhamia chama kingine cha siasa hatahamia UKAWA maana hicho si chama cha siasa. Atahamia chadema kwa masharti ya kupewa ukatibu mkuu wa chadema na ugombea urais wa Zanzibar 2020. Ndiyo hapo swali linakuja Mangi atakubali masharti hayo ya Seif kama alivyokubali masharti ya Lowassa? Jibu swali, acha blaa blaa.
 
Siioni kbs tofauti ya lipumba na bashite ni bora wazazi wao wangekula tu ada zao.
Mtatiro alisema ingekuwa wanapambana na Lipumba Peke yake angekuwa washamaliza mchezo saa mbili asubuhi lakini hawapambani na Lipumba bali wanapambana na TrumpRapa na Serikali yake ndio maana issue inakuwa ngumu...Leprpfeseli kawekwa Front tu ila nyuma kuna Sirikali Nzima.
 
Natamani kuwa proffessor ,
Ila nikikumbuka kuna proffessor I H Lupu...... Nakosa hamu Na huo uproffesa .
 
Hivi Maalim
Katika pitapita zangu nmekutana na hii barua sina uhakika kama ni ya kweli mwenye information zaidi naomba ufafanuzi
ab624ec3e446b67e3f2c82fd77155b25.jpg
Hii tarehe ya barua mbona inaonyesha kuwa Msajili amemtambua katibu mpya kabla ile ya juzi kina Lipumba kudai kuwa wamemvua Seif sharif Ukatibu wa chama?
Jee hii ndio inathibitisha kuwa Msajili na Lipumba wote wanafanya uhuni huo pamoja? na ndio inathibitisha kuwa serikali ndio inayotoa msaada kupitia msajili kuvuruga CUF ili kina Seif Sharif wapate tabu kuisumbua CCM zanzibar?
 
Nimefurahi Sana. Hongera sakaya
Na kwa wadhifa huo wa Katibu Mkuu , jambo la kwanza ni kuzuru Makao Makuu ya chama cha CUF Zanzibar,Tutampa ushirikiano. Lakini nae akishindwa kufanya hivyo Msajili aweza pia kuchukua hatua stahiki kwa kushindwa kukamilisha majukumu yake ya kichama. Hongera sakaya
 
Na kwa wadhifa huo wa Katibu Mkuu , jambo la kwanza ni kuzuru Makao Makuu ya chama cha CUF Zanzibar,Tutampa ushirikiano. Lakini nae akishindwa kufanya hivyo Msajili aweza pia kuchukua hatua stahiki kwa kushindwa kukamilisha majukumu yake ya kichama. Hongera sakaya
Nakuɓaliana na wewe kwa sharti moja siƙu hiyo hiyo sakaya akienɗa zanziɓar kuimarisha chama hamad aje bara naye kuimarisha chama huku pia tutampa ushirikiano
 
lissu mbona haingilii kuweka mambo ya kisheria sawa??? au anafaidika na uwepo wa lipumba cuf???
 
Mbona nasikia kunapingamizi la kisheria pesa hizo zisipelekwe CUF LIPUMBA ,MBAYA EEH
 
Mtapiga kelele mtanyamaza wenyewe achana na msomi anaumaliza mimi kwenye CUF MWALIM SEFU alijiona mungu sasa anamalizwa kisomi
 
Back
Top Bottom