Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,310
- Thread starter
-
- #161
Hakika umetamba,
Tenzi kutaramba,
Mods kuwapamba,
Members kuwaimba,
Niaba ya Robot MTAMBA,
Shukurani kutoifumba,
Kwako tumeiumba,
Kwa tungo kujiramba
SHOSSI umebamba
Kanuni shika,
Hutoguswa hakika,
wale mlahaka,
walo na dhihaka,
JamiiForums siyo chaka,
Ni kiota kwa wahajaka,
SHOSSI umesomeka
nimekuwa bubu gafla
asante sana dear
kweli maneno yameni kimbia
:A S-rose::hug::busu
Usisingizie maneno ila wewe ndo mekimbia
Nanakujua fika, tangu mwanzo nimekusifia
Usifiche nahau na semi pia
Zimwage tena kwa wingi mpaka watu wakimbie
Zikunjue na methali na bonzo pia
Kuna wakati nimechoka natamani nijiliwaze
Nikiwa kwetu Tanga hakuna upweke
napakumbuka sana Tanga nikiwa mpweke
Inshallah nitarudi kuijenga Tanga yetu
Nimejifunza mengi nikiwa safarini
Natamani nirudi kwetu niyaenzi
Nyumbani ni nyumbani
Inshallah nitarudi kuijenga Tanga yetu
Nakumbuka sana ngoma zetu
Kamwe sikuwahi kosa la kufanya kwetu
Sijaona na sitaona kama Tanga kwangu
Inshallah nitarudi kuijenga Tanga yetu
Shossi ndugu yangu nafurahi kukufahamu
Dunia bila ndugu waweza pata wazimu
JF napapenda pamenifunza mengi muhimu
Inshallah nitarudi kuijenga Tanga yetu
Nipo ndugu yangu... Sikukuona mndenyi vp?
Mbona mi simo au kwa vile ni mwana ccm
Aisee ngoja nikakariri mistari, nikujibu kishairi.
Kwa sasa wacha nikugongee senksi kwanza.
BRB!
Mimi ningali mwanafunzi katika hii tansia
Bado singuli kutunga nje ya tanzania
Baraza watu mahiri Kimensera acha kutania
Ila umetoa wazo zuri kazi talifanyia
Sivibaya kuijenga lugha yetu sawia
Nawe pia umo njoo tupige kasia
Usijitoe kundini kusema utenzi ni kadhia
Tungo huleta faraja penye dhiki na ghasia
Malenga hutoa hoja za msingi na wosia
Namaliza kukuomba tunga japo kwa kukisia.
Wajuzi walo jamvini watakufunda kiintelejensia.
Utakuwa mahiri na kuwapiku na waasia.
duh humu malenga mko wengi mnaenda kimashairi na tenzi hongereni
duh humu malenga mko wengi mnaenda kimashairi na tenzi hongereni
Nilingoja lako neno na wewe nikutaje
Mtoto uliye na hiba nikushau iweje
Mwenye ladha ya mapenzi na macho ya huba
Siku zote sikinai kwenye prof yako naganda kama luba
DaMie hupo nyuma kuchangia jamvini
Sasa noa panga na jembe tia mpini
Nani asojua mchango wako jamvini?
Napata tabu as natumia simu. Nikipost beti hazikai inavyotakiwa I am out nikirudi nitaedit nakukupa sifa zako.
i see asante sana Mohammed shossi
Kumbe uwepo wangu unautambua
Nashukuru sana kwa kompulimentaliri
Naombi maalumu kwako hili lifanyie kazi
Na mimi ninatamani kuwa mtunzi wa shairi
2011 naweka nadhiri moyoni
Kuwa mtunzi mzuri wa shairi ,
nikienda sambamba na MJ1, Asprin,Teamo
Mzee Mwanakijiji,Michelle ,wewe mwenyewe na wengine wengi
walo katika fani hii
Asante kwa kweli
nami nasubiri,
beti zenye sifa zaidi,
ili kunipa ahueni.
Michelle nimefurahi kutangaza yako nia
Karibu tena nyumbani uje kuhamia
Tena uje kwa kasi ilizidi spidi mia
Uje tule bada, ngogwe na bamia
Tanga imekuwa takujengea sahare
Uione bahari na samaki narenare
Tuijenge Tanga jetu tusicheze segere
Mimi ndugu yako umejiwahi mapema
Ingekuwa sijajua ningekutongoza zamani
Wewe ni dada yangu tumeshea mama
Tusitupane ndugu tukajenge nyumbani
Sahare Sahare nitafurahi kujengewa
Nitajiona wa thamani sahare ukinijengea
Niko njiani ndugu yangu Tanga ntarejea
Kufurahi na kusahau magumu ya ugenini