Magreat Thinkers ninaowafeel...........

ulijuwa kufariji, allah akakukareem.
ikawa mujib kuwapokea , wale walio muhimu
ukakupamba kwa huba , na ucheshi hakukunyima.

ukayapita mapana , kumridhisha kila muungwana..
ikawa ni tunu , kuwatunuku na siha kuwajulia..
hayupo mfano wako , ndani ya hii dunia..
akujaalia rahim , kwa siha na ukareem...



usinicheki ndio najifunza okay??) heheheh lol mpaka umenitia bilisi lol..

 
Baraza la kiswahili wanafanya nini sasa kumbe vipaji tunavyo humuhumu jamii forum ninyi ndio mlitakiwa muongoze kweli nimekupa saluti kipaji uacho mzee hongera sana man!

 
Realman wanichesha, meneja uso kitambi
Tungo hujasherehesha, usije niwacha kwa kumbi
Nadhani mdomo wakuwasha,ukazungumza kimatumbi
Kana unaumwimbi,si ungekula tambi?
Duh nimechoka maneno sina

Meneja kitambi cha nini, yeye wake weredi.
Kwa ujanja mjini, umahiri nawazidi.
Mapromota wa nini, kama meneja si fisadi?
Umeneja wanifaa, haki zako nizilinde.

Mo kipaji unacho, Maulana umshukuru
Wengine wana kijicho, wanapita hawashukuru
Utausahau mchacho, kipaji kukuweka huru
Umeneja wanifaa, haki zako nizilinde.
 

Wala sitakucheka hilo shaka ondoa
Umenitahidi hoja kupangilia
Unataka kuwashinda malenga walotangulia
Maneno yako tiba yashinda za asilia
Ukarimu wako ni sifa alokupa Jalia

Haya sasa aamka ghani kutupatia
Uzipange kwa ubeti wala si zakutupia
Utujuze yako hali na aila yako pia
Usinisahau kwa dua pamoja na nabia
Mungu atkupe ya kheri na wanajamvi pia
Sitachoka kukutunza hadia


Kaditama namaliza kwa kuusia
Uwache kumcha Allah na mtume kumsalia
Uwarehemu wazazi wote walotangulia
Ulichona tugawane alokutunuku Jalia
Siwezi kukiweka bayana kila moja talila
Najua wengi wakitaka na wanakifatila.
 

Mameneja mahasidi haki zetu kuziviza
Hamnatofauti na mafisadi pesa munazitukuza
Huwezi fanya mradi peso usio zaa
Lengo lako ufaidi, uniletee kizaazaa
Au ilikuwa midadi, umeneja kuukuza?
Sidhani kama umweledi, ujuzi wangu kuukuza
 
Baraza la kiswahili wanafanya nini sasa kumbe vipaji tunavyo humuhumu jamii forum ninyi ndio mlitakiwa muongoze kweli nimekupa saluti kipaji uacho mzee hongera sana man!

Mimi ningali mwanafunzi katika hii tansia
Bado singuli kutunga nje ya tanzania
Baraza watu mahiri Kimensera acha kutania
Ila umetoa wazo zuri kazi talifanyia
Sivibaya kuijenga lugha yetu sawia
Nawe pia umo njoo tupige kasia
Usijitoe kundini kusema utenzi ni kadhia
Tungo huleta faraja penye dhiki na ghasia
Malenga hutoa hoja za msingi na wosia
Namaliza kukuomba tunga japo kwa kukisia.
Wajuzi walo jamvini watakufunda kiintelejensia.
Utakuwa mahiri na kuwapiku na waasia.
 
Darlington wangu nini kimekusibu
Hekima zako zimwage usiwe kama bubu
Fikra zako mwanana tamu kama zabibu
Malenga wakusubiri wa dar na bububu
Hakuna asiekujua unaeng'aa kama balbu
Haya fanya hima utuletee majibu
Na upate wasaa ueleza kinachokusibu
Tungo utuletee ukivunje na kibubu
Zilizoficha za hemima ulizoridhi kwa mababu
 
Wadau nawauliza mbona mmeingia mitini
Au mwajipanga ili mnawiri jamvini
Ngongoja si mambo naona hamnithamini
Au nahau zimekishwa mnagoogle netini
Kama umalenga umewashinda nendeni uvuvini
Huko mliwe na papa na nyangumi baharini
 
Sasa umetamanisha, kujifunza mashairi
shabani robati amsha, tufunze yako shairi
medani nimechemsha, wapi vitabu shairi
 
Sasa umetamanisha, kujifunza mashairi
shabani robati amsha, tufunze yako shairi
medani nimechemsha, wapi vitabu shairi

Tena utumie fasihi hoja kusherehesha
Usije uneokana kioja ukajachekesha
Utume na nahau kiswahili kukisherehesha
Lete nyingi fakuri zile zenye bashasha
Usichokoze vigori ukadhaniwa ni basha
Vigori niwachiie mie nwape mshawasha
 
Mameneja mahasidi haki zetu kuziviza
Hamnatofauti na mafisadi pesa munazitukuza
Huwezi fanya mradi peso usio zaa
Lengo lako ufaidi, uniletee kizaazaa
Au ilikuwa midadi, umeneja kuukuza?
Sidhani kama umweledi, ujuzi wangu kuukuza

Hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,
Marijani ajuta meneja kukosekana,
Kazi za babaye mtaani zapatikana,
Familia haipati cha maana,
Usipuuze mameneja haki kuzikinga.

Lionel Mess wake ujuzi,
Lakini meneja hampuuzi,
Dunia leo sio ya juzi,
Mwenye kuijua njia mwache aongoze

CBE mikataba umefunzwa,
Muhimu sheria kujuzwa,
Ili njiani usije kwazwa,
Copy raiti wakumbuka?

Meneja mikataba najua,
Fungamtama anazingua,
Yake dowans tunajua,
Realman si Fungamtama.

Mo wewe kweli malenga,
Mashairi yako ni mwanga,
Mimi sijui vina kutunga,
Usibanie umeneja
 
Mkuu kazi njema kabisa!!:clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2:
 
Mkuu kazi njema kabisa!!:clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2::clap2:

Si kazi njema kabisa bali tungo za kisasa
Usinitie bashasha moto kuuendeleza
Wameingia mitini wanajmvi mpaka sasa
Simuoni PJ amniacha kwenye giza
Wiselady hakunijibu kile kisa
Nilimtaka ujira kisha akanyamaza
Na wewe ndugu upo wapi sasa
Nakumbuka ahadi utatembelea mbeza
Bado upo mjini au umepatwa na mkasa?
Sharifu akusubiri anamengi ya kukujuza.
Fanya hima wende safari unangoja nini sasa?
 

Asante sana ndugu Mola akupe fanaka
Wala usijiweke nyuma twende utafika
Msingi bora unao njoo tulikomboe taifa

Ombi lako nafikiri jibu nitakupatia
Kama sheria najua labda mkzo kutia
Haki zangu haziibwi ataedhubu tajutia

Dunia imeharibika kila mmja mwogope
Anaweza jifanya mwema kumbe sawa na dope
Akakutia shimoni ukakwama kwenye tope
Subiri nifikirie na yawache mapepe.
 
Shukrani zangu za dhati kwenu waungwana
Hamkusita kunipongeza na kushia kuguna
Mimi muungwana nawaombea kwa Rabana
Yeye mstahiki mwenye sifa mwanana
Unadhani tungekuaje kama pumzi angebana?

Nyie ndio msingi nyie ndio kioo
Siwezi wadhikaki nikawaona kideo
Nistakuwa na ihsani nispowashukuru leo


Pongezi nawapa na wasiochangia pia
Wapo kashindwa kuchangia
Muda wao adhim si waliutumia
Wakasoma tungo na nahau pia
Shukrani wandugu wote mlochangia.
Mmoja mmoja kwa mafungu majina nimepangia.

The Following 32 Users Say Thank You to Mohammed Shossi For This Useful Post:
afrodenzi (Yesterday), Asprin (Yesterday), Bubu Ataka Kusema (Yesterday), engmtolera (Today), Fidel80 (Yesterday), Freestyler (Yesterday), Gurudumu (Yesterday), GY (Yesterday), Henge (Yesterday), Inkoskaz (Yesterday), Kaizer (Yesterday), KakaJambazi (Yesterday), Katavi (Yesterday), Kiraka (Today), LD (Yesterday), Mawazo1109 (Yesterday), Michelle (Yesterday), Miss Judith (Yesterday), MwanajamiiOne (Yesterday), Mzee Mwanakijiji (Yesterday), Nguruvi3 (Today), NILHAM RASHED (Today), RealMan (Yesterday), Rose1980 (Yesterday), Shapu (Today), Teamo (Yesterday), The Finest (Yesterday), VoiceOfReason (Yesterday), Wa Ndima (Yesterday), WiseLady (Yesterday), WomanOfSubstance (Yesterday), Yo Yo (Yesterday)​
 
 
Hongereni ma great thinker mliotajwa, hakika mwastahili.
 
Hongereni ma great thinker mliotajwa, hakika mwastahili.

Nilingoja lako neno na wewe nikutaje
Mtoto uliye na hiba nikushau iweje
Mwenye ladha ya mapenzi na macho ya huba
Siku zote sikinai kwenye prof yako naganda kama luba
DaMie hupo nyuma kuchangia jamvini
Sasa noa panga na jembe tia mpini
Nani asojua mchango wako jamvini?


Napata tabu as natumia simu. Nikipost beti hjazikai inavyotakiwa I am out nikirudi nitaedit nakukupa sifa zako.
 
Hakika umetamba,
Tenzi kutaramba,
Mods kuwapamba,
Members kuwaimba,
Niaba ya Robot MTAMBA,
Shukurani kutoifumba,
Kwako tumeiumba,
Kwa tungo kujiramba
SHOSSI umebamba

Kanuni shika,
Hutoguswa hakika,
wale mlahaka,
walo na dhihaka,
JamiiForums siyo chaka,
Ni kiota kwa wahajaka,
SHOSSI umesomeka


 
Kweli kiswahili ni fani za watu Mohammed Shossi na JF Moderator na wengineo nawapeni heshima yenu maana kutunga shairi kama hili ni ngumu jamani. Vihisishi, vivumishi, vitenzi nawapeni sifa zenu. Hongereni sana!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…