cheusimangala
JF-Expert Member
- Feb 27, 2010
- 2,585
- 500
ewe cheusi mangala, salamu nakutmia,
mola anayetawala, akupe nyingi jalia,
usijeingia hila, nduguzo kutuchukia
...upatapo siku mbili, moja ututembelee.
uliondoka ghafula, ukatuacha na njia
ndege ukaidandila, ukapotea sawia
hatuna hamu ya kula, hata maji kunawia
...ile namba ya nduguyo,
Cheusimangala upo? Mudy Shossi hajasahau,
Labda beti lijalo umo, ataghani kwa nahau,
Wala usiwe na kinyongo, kwenye listi hatakusahau.
Kazi unayonituma, sina budi ujira kupatana Utaweza kubali, matai tusije kamatana Nataka nyama ilonona tena mwanana Sitakiutumbo japo wachanga wanapikia banana Walasitaki yakidadi kwenye meno yashikana Wala sitaki ya mbuzi hata iwe kilo nane Nataka paja la swala alienona mwanana Wiselady nauliza je wajua kuwinda?
Wa kuwinda Wiselady? Sijui wamaanisha nini,
Au wataka weledi, watufumba tuachwe mjini,
Asije akamaindi, akakasirika mwandani
kusaidiana ni jadi, akuomba Wiseladi
GT wake mdogodogo mwendo, wajulikana zamani
Mwendo usio vishindo, haufeli abadani
Asoweza huwa kando, awezae huwa ndani
Wanajamvi mbona mmeingia mitini Au tungo zenye vina Vimeishia kichwanI Mwanakijiji hajanena au yupo kazini
gt humu tu wawili, japo moja ni wa longi
gt mimi nipo tuli, wanajamii siwasongi
tena bado sina mwali, bado naruka vigingi
punde taweka tangazo, nami nipate mwandani
Nimechoka, nimechoka mie, nataka enda mie jama,
Wajibu nikatimizie, wangu ubavu unalalama,
Hizi kazi nisisingizie, kumbe JF nimezama
Mudy Shossi tutaonana, huenda kesho ya Maulana,
PakaJimmy sijamuona, namuaga hata kama,
Cheusimangala mama, nakutakia usiku mwema
Mwandani kanikonyeza, anitega kinamna,
Vidole kavitembeza, kunako akanibinya,
Nikaona mmh anichokoza, cha moto atakiona
ooooooh kibodi siwezi bonya......
Kweli wewe si wasongi, malenga mashuhuri Umejikita kama kigingi, mwingi wa sururi Usijeoa giningi, walakwa waikwiriri Usije oa shangingi maisha ukayaona shubiri
Kaka Mo mie najitolea kuwa meneja wako ili kusiwe na piracy ya kazi zako. Big up to yourself
Bora iweke moyoni , hiyo siri mwana flani
Siri ibaki sirini, siyo tena hadharani
Hapo utaweza wini, ewe mtunzi makini
Nipo ndugu yangu... Sikukuona mndenyi vp?Wakuu safi sana ndio nawasoma saizi, mko fiti, kumbe WOS sio mchezo, nilikuwa nakutafuta sana sisteri umepotelea wapi?? Mohamed unatisha mkuu, uko juu, vina vimetulia kinoma. Kweli watokea Tanga.