Magonjwa 10 yatokanayo na Pombe (hio unayokunywa wewe)

tilmikha

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
496
604
Pombe imekuwa kimbilio la wengi kama sehemu ya starehe au moja ya kitu cha kuondoshea msongo wa mawazo.

Kiukweli Pombe ni neurotoxin (sumu ishambuliayo mfumo wa fahamu) ambayo huharibu ubongo kwa njia ngumu kupitia kufuta kwa muda mrefu na uondoaji wa mara kwa mara wa kumbukumbu, na kusababisha ugonjwa mkubwa na vifo pia.

Yafuatayo ni magonjwa 10 yanayosababishwa na unywaji wa Pombe.

1) Ugonjwa wa ini
Pombe ukisha inywa sehemu yake kuu inapokua inavunjwa vunjwa ni katika ini, hivo huweza kukuweka katika hatari ya kuharibikiwa na ini

2)Ugonjwa wa akili (alcohol related psychosis)
Kama nilivyotangulia kueleza hapo juu kuwa Pombe ni aina ya sumu ishambuliayo mfumo wa fahamu hivo baada ya mnywaji kunywa huwa anapata hallucinations na matokeo yake badae huharibikiwa na akili.

3)Ugonjwa wa Pancreas (pancreatitis)

4)Canser
Pombe pia ni carcinogens yaani ina vitu ambavyo hupelekea mtu kuugua kansa. Mfano wa kansa kama ya koo, mdomo, ini, uchango mkubwa na puru.

5)Vidonda vya tumbo

6)Kushuka kwa kinga ya mwili
Kinga ya mwili inaposhuka mtu huwa rahis kushambuliwa na vijidudu visababishao magonjwa mfano, ugonjwa wa TB, kisukari, hata HIV.

7)Utapiamlo

8) Ugonjwa wa kudhoofu mifupa (osteoporosis)

9)Magonjwa ya moyo (cardiovascular diseases)

10) Ajali ambazo husabisha mauti au ulemavu wa kudumu.

Najua yote haya unayafahamu, lengo ni kukumbushana tu so stay calm and leave the liquid.
 
Hatuwezi ku escape magonjwa ila kufa kwa sababu ya ulevi huoni kama ni Sawa Sawa na suicide mkuu?!

Sent using Jamii Forums mobile app

Hayo magonjwa ni myth tu mkuu, na wanaoleta propaganda ni wale wanaowaonea wivu wanywaji.

Unaweza kuhakiki kwa kutafuta statistics za nani wanaishi zaidi kati ya wasiokunywa na wanaokunywa, utakuta wanywaji wanaongoza kwa kuishi maisha marefu.
 
Back
Top Bottom