Tumekuwekea hapa namna magonjwa mbalimbali yanavyo ibuka kitaalamu kutokana na Obesity

OCC Doctors

Senior Member
Jul 20, 2018
104
151
Mafuta ya ziada kwenye tumbo (Obesity) husababisha mshipa unaoleta damu ndani ya ini (Portal vein) kujaa mafuta ya asidi yasiyo na kazi (free fatty acids), na kuongeza mkusanyiko wa mafuta kwenye ini.

Mafuta pia hujilimbikiza kwenye seli za misuli. Ambapo sasa kunaanzishwa ukinzani dhidi ya homoni inayo dhibiti sukari mwilini (Insulin resistance), na hatimae homoni ya insulin kuzagaa kwenye damu kuliko kawaida (hyperinsulinemia), na hapo ndipo uratibu wa sukari mwilini unaharibika, ugonjwa wa kisukari unaanza.

Baada ya mafuta kuzagaa kwenye misuli, hatua inayofuata ni ongezeko la mafuta kuanza kuenea kwenye damu (dyslipidemias) na hapo sasa shinikizo la juu la damu (hypertension) hujitokeza.

Hali hiyo hupelekea viwango vya sumu-taka (uric acid) kuongezeka katika damu, na hapo ndipo hali ya kuganda kwa damu huanza (prothrombotic state) ambayo huongeza viwango vya protini ya kugandisha damu 'fibrinogen' na kuzuia-vizuizi vya kuyeyusha damu "plasminogen inhibitor I'' kufikia hapo sasa damu itaanza kuganda ambapo uvimbe wa kizazi (Fibroid) utajiunda mfano wa nyama ya maini kwenye kizazi cha mwanamke.

Wagonjwa hao wenye ongezeko la tumbo (obesity) wana hatari ya kupatwa na ongezeko la kukosa pumzi wakati wa kulala kutokana na sehemu ya kupitisha hewa kuziba ambapo huanza kukoroma wakilala (obstructive sleep apnea) ni kutokana na uhaba wa kupita kwa pumzi kwenye bomba la hewa.

Hatari zingine ni pamoja na hatua ya juu ya ugonjwa wa ini usiohusiana na pombe (nonalcoholic steatohepatitis), kutokana na mwili kuhifadhi mafuta mengi kwenye ini.

Pia ugonjwa sugu wa figo, ugonjwa wa vimbe kwenye vifuko vya mayai (polycystic ovary syndrome) kwa wanawake.

Uwepo wa tumbo kubwa na mafuta ya ziada hushusha homoni ya kiume kua chini, hupelekea kiwango cha chini cha homoni ya kiume kwa wanaume (low serum testosterone), ambapo sasa huleta shida ya kusimamisha uume au upungufu wa nguvu za kiume au vyote kwa pamoja.


1692956010010.png
 
Tupatie na njia za kuepuka na kama mtu anakitambi anakiondoaje
Punguza sana wanga. Sio unakula hadi unahemea kwenye mbavu.
Kama una kitambi asubuhi kunywa chai na andazi 1 au mkate vipande 2.
Mchana ugali/wali unaojaa kwenye kikombe cha chai au nusu na mboga kwawingi
Usiku kama mchana na unaweza punguza kiwango.
Kuwa active kwa mazoezi, kazini sio bali tembea.
Jaribu mwezi halafu kapime uzito.
 
Back
Top Bottom