Magoli Matano(05) yaliyonivutia kwenye Soka(magoli bora kwangu) ni haya...

Balantanda, mie yangu ni haya hapa chini. Ila nimekuja kujua juzi tu kuwa upigaji mpira wa namna hii unaofanya rotation, ulianzishwa na Mbrazil mmoja (Arthur Friedenreich ) mwenye baba Mjeruman na mama Mbrazil (black). Jamaa alikuwa akijitahidi sana kuficha weusi wake. Ila jamaa ndiye aliyewafanya Wabrazil waanze kuupenda Mpira wa Miguu. Hadi leo anabaki mchezaji pekee aliyefunga magoli mengi mno (around 1300).

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=dwRYYeEk5Eg&NR=1"]YouTube- Roberto Carlos Impossible Goal[/ame]

Hili goal chini, Zidane anasema aliangalia mpira unavyopita, akainamisha kichwa chini na kuhuzunika kuwa huo mpira unaenda kumuuwa rafiki yake Bartez. Kweli Kipa alisimama tu.
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=W5XpXU8TBoo"]YouTube- roberto carlos super goal[/ame]

Hapa bibie Marta akifanya Mambozi.
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=Iba7RiOuvEQ"]YouTube- Brazil Marta Amazing Goal vs USA (World Cup China)[/ame]

Mpira mwingine uliopigwa na kutengeneza curve ni huu hapa chini, hapa ni Etoo.
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=lEhONxEOy68"]YouTube- Eto'o best goal FC Barcelona[/ame]

Mwisho namaliza na Carlos Alberto. Hii ilikuwa ni mwaka 1970, World Cup huko Mexico kati ya Brazil na Italy. Brazil walifahamu kuwa back ya Italy si ya kuipita kiurahisi. Hivyo wakawa wamefanya mazoezi ya kupiga mashuti wakiwa mbaaali. Ila hii njia waliitumia mara moja tu kwenye goli la mwisho. Nafikiri ukiangalia ile nyumbani wanalia "niachieee....." utaona kuwa hapa kila kitu kilikuwa kimefanyiwa mazoezi mapema na hakuna cha niachie, just Eye Contact.
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=NZkR5Wb2KQs&feature=related"]YouTube- Carlos Alberto 1970 wondergoal[/ame]
 
  1. Ryan Giggs-Man U VS Arsenal
  2. Leo Messi-Barca VS Getafe
  3. Zinedine Zidane-Real VS Leverkusen
  4. Dennis Bergkamp-Arsenal VS Newcastle
  5. Steven Gerrard-England VS Germany
  6. Luis Garcia-Liverpool VS Juventus
  7. Rivaldo-Barca VS Valencia
  8. Samuel Etoo-Cameroon VS Brazil
  9. Christiano Ronaldo-Man U VS Porto
  10. Patrick Mboma-France VS Cameroon

Belo nae kwa nongwa doh...
Si tumeambiwa magoli matano?
 
Hahaaaaaaaaa..Haya mzee mwenzangu nawe nipe yako matano basi(najua la Mtakatifu Dinho halitakosa)...

Nazungumzia goli kama hili

[ame="http://http://www.youtube.com/watch?v=ijR1WX2bLIo&feature=PlayList&p=162E09F90BC30B1D&playnext=1&playnext_from=PL&index=23"]http://http://www.youtube.com/watch?v=ijR1WX2bLIo&feature=PlayList&p=162E09F90BC30B1D&playnext=1&playnext_from=PL&index=23[/ame]

Na hili

[ame="http://http://www.youtube.com/watch?v=uLzHmQQ-Wfc&feature=PlayList&p=162E09F90BC30B1D&playnext=1&playnext_from=PL&index=11"]http://http://www.youtube.com/watch?v=uLzHmQQ-Wfc&feature=PlayList&p=162E09F90BC30B1D&playnext=1&playnext_from=PL&index=11[/ame]
 
Kwa heshima na taadhima nikiwa na akili timamu pasipokushinikizwa na kiumbe cha jinsia yoyote napenda kuorodhesha magoli matano ninayoyaheshimu...

5] Maesto DENIS BERGKAMP dhidi ya newcastle.

4] Dikteta wa kiungo ClLARENCE SEEDORF alipokuwa Madrid enzi hizo alipata kupiga shuti ktk mechi moja hivi. Shuti hilo lilisadikiwa kuwa na uwezo wa kutoka Posta mpk Mlandizi...
Seedorf kwa sasa yuko AC Milan.

3] BENY MWALALA wa Yanga ya Tanzania...
Alipata kufunga goli mardaaad dhidi ya simba ya Ilala ktk uwanja mpya wa Taifa.
Simba walikufa kwa goli 1-0.

2] alianza nafkiri Keegan, akaja Glein Hodle, akafuata sijui mkulima gani, akaja stuart peace, kisha akamaliziwa Peter Sheelton na ARMANDO DIEGO MARADONA akafunga goli na kudhihirisha kuwa England hawajui mpira.

1] goli langu bora lililobeba top 5 yangu linatoka kwa yule kiungo mbarikiwa anayeaminika kuwa ameshushwa toka mbinguni ili kuja kutuonyesha soka la huko linavyochezwa.
Goli hili alilifunga dhidi ya Chelsea ktk mechi ya ligi ya mabingwa hapo stamford bridge.

Mtakatifu huyu alimchezesha kwasakwasa + tukunyema nahodha wa chelsea na kumchambua kipa wa kilabu hicho toka magharibi mwa London.

Hapa namzungumzia Ronaldo de Assis Moreirra ama waweza kumuita The Saint Ronaldinho ''dinho'' Gaucho ambaye kwa sasa yupo AC Milan, mabingwa mara 7 wa ligi ya mabingwa na pia ndio timu yenye mafanikio mengi zaidi ya kimataifa.

Forza Milan
Sempre Dinho
 
Back
Top Bottom