Magogo ya kukatia nyama mwisho September 30

Alafu mbadala wa hayo magogo ni nini.Au ndo ile wanakataza alafu wananchi watajijua wenyewe.Kuna matamko yanatoka utadhani nchi hii kila sehemu iko kama daresalam.
 
Ukifanya risk assessment utaona kuwa ;
Ni afadhali mara 100% kuendelea kutumia hayo magogo kuliko mashine za viwandani!

Werevu wakifika bichani wanapendelea kukatiwa nyama kwa kutumia magogo kuliko zile mashine za viwandani
 
Magogo yalitumika toka enzi za Mababu na hawakupata madhara yeyote waliishi miaka mingi mno,msrmeni kukata mifupa uwezekano wa kula chuma ni mkubwa,bora utafune mti kuliko chuma,mi nafikiria ingekua option,mabucha yachague
Ni kweli, ila mababu zetu walikula vyakula vingi vya asili na vyenye virutubisho, walifanya mazoezi kila mara kwa kufanya kazi ngumu na kutembea umbli mrefu. Hii iliwasaidia kiafya na kuweza kukabiliana na magonjwa mengi. Sisi vyakula na maisha yetu ya kisasa yanaupungufu sana na hivyo ni nyema kuchukua tahadhari.
 
Mbona bucha zote zina machine za kukatia nyama? Japo zile mashine naziogopa sana..sijaona magogo siku za karibuni hapa.

Na je hao vijidudu ukienda kupika nyama hawafi)
V(joke)
Isitoshe tungekuwa tumeshakufa kwa miongo mingi kwani tumeanza kula nyama ya gogo tokea tuko wadogo.
 
Magogo ni mazuri kukatia nyama Ila wauza bucha wengi hawajui namna ya kukatia na kufanya usafi kwenye magogo. Pia wanatumia hayo magogo miaka mingi pasipokubadilisha. Hii huleta athari na kutengeneza magonjwa kwenye hayo magogo
Serkal kupitia wizara ya afya ,mifugo na uvuvi imepiga marufuku magogo ya kukatia nyama mabuchani ikitaja kuwa yana madhara kwa afya ya walaji

Kiongea na kituo cha EATV mkuu wa kitengo cha afya ya walaji kutoka bodi ya nyama bwana Selvester amesema kuwa wamewapa taarifa ma afsa afya wote wa mikoa na wilaya kisimamia zoezi hilo kwa umakini

Yale magogo ya kukatia nyama huhifadhi uchafu wa mabaki ya nyama na vijidudu na baadae huleta magonjwa kwa walaji,alikaliliwa bwana Silvester akiiiambia EATV

My take

Walikuwa wapi tangu tumeuziwa uchafu na nini mbadala wa magogo haya

Chanzo EATV
 
Mbona bucha zote zina machine za kukatia nyama? Japo zile mashine naziogopa sana..sijaona magogo siku za karibuni hapa.

Na je hao vijidudu ukienda kupika nyama hawafi)
V(joke)
Kuna vijidudu haistahili kukaa kwenye joto Kali na pia sehemu kama migahawani au mahotelini watachemsaha inavyostahili ili hivyo vidudu vife
 
Back
Top Bottom