Serikali yapiga marufuku nyama ya kuku kutoka nje

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,823
2,000
Serikali imepiga marufuku kuagiza na kuingiza nyama za kuku waliochinjwa kutoka nje ya nchi ili kulinda afya za walaji wa bidhaa hiyo ya nyama nchini.
Nyama%20ya%20Kuku1.JPG

Nyama ya kuku ikiwa tayari kwa kuliwa

Katazo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha kwenye mahojiano maalum na EATV ilipotaka kupata ufafanuzi wa serikali kuwa inahakikisha vipi nyama na vitoweo kutoka nje ya nchi zinaingizwa nchini zikiwa na ubora unaokidhi viwango vya afya kwa walaji.

Ole Nasha amesema hairuhusiwi kuagiza wala kuuza kuku waliochinjwa kutoka nje ya nchi kwakuwa kwa sasa nchi inajitosheleza na inajitegemea kwa kiwango kikubwa cha nyama.

Amewataka wafugaji na wafanyabiashara kutumia fursa za kuzalisha nyama kwa tija na ubora zaidi ili nchi ianze kuuza vitoweo vya nyama hasa kuku nje ya nchi.
nasha.jpg

William Ole Nasha

Ameongeza kuwa tayari serikali inaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa viongozi wanaoshirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu kuingiza nyama hizo za kuku wa nje nchini.

Chanzo: IPP Media
 
Mtu mdogo

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
525
1,000
Bora hivo kwanza kuku tunao wengi hiyo mi sumu sijui kwanini wana ya import
 
Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
9,049
2,000
Afya bora ni pamoja na madawa bora na yawe katika bei za kawaida tuu...Bongo bei za madawa ya binadamu utadhani hizo dawa zinatoka sayari ya Mars...
 
Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,760
2,000
Serikali imepiga marufuku kuagiza na kuingiza nyama za kuku waliochinjwa kutoka nje ya nchi ili kulinda afya za walaji wa bidhaa hiyo ya nyama nchini.
Nyama%20ya%20Kuku1.JPG

Nyama ya kuku ikiwa tayari kwa kuliwa

Katazo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha kwenye mahojiano maalum na EATV ilipotaka kupata ufafanuzi wa serikali kuwa inahakikisha vipi nyama na vitoweo kutoka nje ya nchi zinaingizwa nchini zikiwa na ubora unaokidhi viwango vya afya kwa walaji.

Ole Nasha amesema hairuhusiwi kuagiza wala kuuza kuku waliochinjwa kutoka nje ya nchi kwakuwa kwa sasa nchi inajitosheleza na inajitegemea kwa kiwango kikubwa cha nyama.

Amewataka wafugaji na wafanyabiashara kutumia fursa za kuzalisha nyama kwa tija na ubora zaidi ili nchi ianze kuuza vitoweo vya nyama hasa kuku nje ya nchi.
nasha.jpg

William Ole Nasha

Ameongeza kuwa tayari serikali inaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa viongozi wanaoshirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu kuingiza nyama hizo za kuku wa nje nchini.

Chanzo: IPP Media
Sasa picha za hao kuku na pia picha ya huyo kiongozi, kwanini mods amezikanseli?
 
REAGAN C.MABOGO

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
1,270
2,000
Hiyo ni kasumba ya ujamaa.! Na ni akili ya kimaskini.! Vipi na sisi tukipigwa marufuku kupeleka kwao?! Au huwa hatupeleki?! Kama huwa tunapeleka maana yake ni kwamba, soko la ndani pekee halitoshi kwa taifa lolote lenye maono! Suala ni kudhibiti viwango tu!
 
Entim

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
4,014
2,000
Kuku wanaingizwa nchini wanakaguliwa na kupitishwa na TBS, na muigizaji analipa kodu. Je kuku tunaowala mtaani nani anakagua?
 
chilubi

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
8,031
2,000
Nasubiri SMZ serikali ya kuiiga nione kama na hili watalicopy.... mana Shisha katngaza makonda basi na mkuu wa mkoa wa zenji nae kaona aige... Bia lakini kama kawaida, hazina madhara
 
Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,158
2,000
Serikali imepiga marufuku kuagiza na kuingiza nyama za kuku waliochinjwa kutoka nje ya nchi ili kulinda afya za walaji wa bidhaa hiyo ya nyama nchini.

Katazo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha kwenye mahojiano maalum na Kituo kimoja cha runinga ilipotaka kupata ufafanuzi wa serikali kuwa inahakikisha vipi nyama na vitoweo kutoka nje ya nchi zinaingizwa nchini zikiwa na ubora unaokidhi viwango vya afya kwa walaji.

Ole Nasha amesema hairuhusiwi kuagiza wala kuuza kuku waliochinjwa kutoka nje ya nchi kwakuwa kwa sasa nchi inajitosheleza na inajitegemea kwa kiwango kikubwa cha nyama.
Amewataka wafugaji na wafanyabiashara kutumia fursa za kuzalisha nyama kwa tija na ubora zaidi ili nchi ianze kuuza vitoweo vya nyama hasa kuku nje ya nchi.

Ameongeza kuwa tayari serikali inaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa viongozi wanaoshirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu kuingiza nyama hizo za kuku wa nje nchini.
 
Sefu jafary

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
382
500
Naunga mkono hoja ikiwezekana wafungie na uingizwaji wa mayai ya kizungu ili turudishe utamaduni wetu wa kula kuku na mayai ya kienjeji.Pia hii itasaidia kukuza soko kwa wafugaji kuku nchini.
 
Simara

JF-Expert Member
Oct 1, 2014
5,664
2,000
Naungana na serikali sababu nchini kuna wafugaji wengi wanaoweza kutosheleza mahitaji sasa kwanini ziagizwe nje?? Ni wakati wa wafugaji sasa ku-pack kuku zao vizuri na kutafuta masoko kwenye supermakert mbalimbali.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom