kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,732
Ni mabishano makali baina ya wamiliki wa kiwanda hiki raia wa uchina na maofisa wa NEMC yaliyochukua muda mrefu kabla ya maofisa hao kutoa tamko la kufungwa kwa kiwanda hicho ambacho mbali na kuzalisha nyama ya Punda ambayo ni kinyume na utamaduni wa watanzania lakini pia mazingira ya uzalishaji wake ni hatarishi kwa afya za wafanyakazi na majirani wa eneo hilo.
Kiwanda hiki ambacho kwa siku kinadaiwa kuchinja Punda wasiopungua 200 inaelezwa kuwa mbali na kukiuka utamaduni lakini pia kinaharibu kizazi cha wanyama hao ambao uzao wake unatajwa kuwa ni mdogo hali inayotishia wanyama hao ambao kwa kanda ya kati hutumiwa katika kazi mbalimbali kupungua ama kutoweka kabisa.
Mohamed Hamis ni meneja msaidizi wa kiwanda hiki ambaye anazungumza kwa niaba ya raia hao wa uchina anasema nyama hizo za Punda zinasafirishwa kwenda kuuzwa nchini China.
Wakazi wa mji wa Dodoma ambao wanatupa lawama kwa mamlaka za mkoa kutobaini kiwanda hicho na kukichukulia hatua huku kukiwa na taarifa ya nyama hizo kuzagaa na kuuzwa katika maeneo mbalimbali ya mji huo hasa kwenye mabaa na migahawa ya chakula.
Chanzo: ITV
1. Wauaji wa Tembo = Wachina
2. Wasafirishaji wa Pembe za Ndovu = Wachina
3. Wawekezaji wa Gesi nchini = Wachina
4. Madawa ya kulevya mengi kutoka Tanzania yanayosafirishwa na wasanii na washabiki wa CCM yanakamatiwa China
Ebu tutafakari kwa kina hawa wachina wanadhamira ya dhati kwa nchi hii? leo hii wanachinja Punda na kujifanya wanasafirisha nje ya nchi.
Kuna post mbili tayari kuhusiana na hiki kiwanda , lakini nimekuja na post hii makusudi kwakuwa ina mengi ambayo hayakusemwa.
Binafsi nilifika pale kiwandani na kukaa karibia wiki tatu hivi, kiwanda kiko eneo la four ways Ikungi njia ya kwenda Singida nyuma ya magodown ya Bhanji, ni eneo la viwanda tupu.
Hiki kiwanda kina eneo kubwa sana, na ni uwekezaji usiopungua USD 1,000,000/= Kiwanda kinajishughulisha na kuchinja punda na pia ukusanyaji wa ngozi za ng'ombe, kuziprocess mpaka hatua ya mwisho na kuzisafirisha kwenda China.
Hapo kiwandani pana facilities zote za kufanyia hiyo shughuli ya ngozi, (nitaweka picha) na pia baadhi ya facilities kwa ajili ya uchinjaji punda kama cold room kubwa sana, containers za friji machinjio nk
Hiki kiwanda kilikamilika mwaka jana na kuanza shughuli zake za ngozi na uchinjaji, lakini sina uhakika kama leseni yake ni kwa ajili ya biashara gani.
Baada ya kuchinja punda wanaofikia container 3 za 40ft, walistukiwa na mamlaka husika kuwa hawana kibali cha kuchinja na kusafirisha nyama ya punda, kwahiyo pale kulikuwa na rumbesa wa nyama za punda za tangu October mwaka jana, zikiwa cold room( nimezila sana karibia siku zote 21 nilipokea pale)
Wachina wakaanza kusaka kibali kwa nguvu zote huku biashara ya ngozi ambayo haikuwa na tatizo ikiendelea.
Katika kuhangaika kwao wakakutana na bwana mmoja aliyekuwa karibu na Waziri husika. Huyu waziri bila kutafakari na kufanya fitina (kibongobongo), akalazimisha mpaka kibali kikapatikana kwa njia za mkato/panya (hapa shekeli ilitumika sana).
Huyu Waziri alivyokuwa juha au mpuuzi (naomba radhi kwa kutumia maneno haya) kwenye bunge la bajeti la mwaka huu alisimama bungeni na kukifagilia sana hiki kiwanda. Kumbukumbu za video zipo na kwenye Hansard rasmi za bunge pia pamoja na taarifa za habari.
Aliihusisha serikali moja kwa moja na kiwanda hiki na kuita ni uwekezaji uliotukuka(siku hiyo nilishangaa mpaka watu wakanishangaa.
Hiki kiwanda pamoja na uwekezaji mkubwa ni kiwanda cha ujanjaujanja kinachofanya mambo yake mengi bila kufuata kanuni na tararibu za uwekezaji nchini, kuna mapungufu mengi sana pale, kuanzia kwa wafanyakazi management mpaka utendaji kazi.
Najiuliza hivi Waziri mzima anayaiwakilisha serikali aliweza vipi kusimamia mpaka kibali kikapatikana bila kwanza kujiridhisha na huo uwekezaji?
Hakika hii ni kasha kubwa kwa chama na serikali na Taifa pia.