OPARESHENI: Vigogo vya kukatia nyama Buchani kukamatwa na kuchomwa moto

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,571
2,000
Bodi ya nyama Tanzania, inatarajia kuanzisha Operesheni nchi nzima ya kukamata na kuchoma magogo yanayotumika kukatia nyama kwenye mabucha ikisema kuwa kufanya hivyo kutasaidia watumiaji wa kitoweo hicho, kula nyama ambayo haina uchafu wowote.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama, Imani Sichalwe kwenye Mkutano Mkuu wa shirikisho la wanachama wa biashara ya mifugo na nyama Tanzania (TALIMETA), uliofanyaka Jijini Dodoma ambapo akijibu hoja ya Mwenyekiti wa wauza nyama Jijini Arusha Alex Lasiki kuhusu upatikanaji wa mashine za kukatia nyama nchini.

Akijibu hoja hiyo, Sichalwe amesema wafanyabiashara hao wanatakiwa kuyaondoa magogo hayo mara moja na kutumia mashine za kukatia nyama na kwamba mashine hizo zinapatikana nchini kwa gharama nafuu.

Akizungumzia juu ya wafanyabiashara wanaouza nyama kwenye ndoo Sichalwe amesema kufanya hivyo ni kinyume cha sheria, huku akitumia nafasi hiyo kuwataka wenye tabia hiyo kuacha mara moja.

Kwa upande wake Afisa nyama wa Bodi hiyo Edgar Mambo, amesema nyama ikikatwa kwenye Gogo na kuhifadhiwa kwenye Friji baada ya muda hubadilika rangi kutokana na uchafu unaokuwepo kwenye gogo hilo.

Katibu mkuu wa TALIMETA, Raphael Chacha amebainisha baadhi ya changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na usimamizi hafifu wa machinjio nchini unaoruhusu uuzaji holela wa nyama na kupelekea wao kupata hasara na kufilisika.
 
Fuqin

JF-Expert Member
Dec 2, 2018
200
500

Umeme wenyewe unakatika kila mara ina maana watu hatuli nyama kisa umeme umekatika??
Kwahiyo serikali ya CCM imegundua kuwa vitambulisho vya wamachinga havinunuliwi kwa sababu ya vigogo vya mabuchani!!!!!!
Na pia korosho imedoda sababu ya vigogo vya mabuchani,weeeeeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
stephot

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
11,511
2,000
Waweke utaratibi mzuri kabla ya kuanza kuvamia mabucha na kuchoma hivyo vigogo..
 
Statesman

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
23,340
2,000
Inasikitisha sana kuna watu wanapinga hata jambo hili jema kabisa la kulinda afya zao.
 
marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
14,421
2,000
Je mafunzo ya namna ya kutumia mashine hizo yamepangiwa utaratibu gani, maana tutegemee wauzaji kukatwa vidole mara kwa mara kama mafunzo ya usalama kazini hayatatolewa
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
24,805
2,000
Hizo mashine zinatumia umeme,vipi huko vijijini ambako umeme haujafika?
Kukurupuka tumezaliwa vigogo vilikuwepo tumekua mara GHAFLA! vimekuwa vinaifaua nyama wakati huohuo unakula Utumbo ambao bado una Kinye cha Mbuzi

Nchii jwa kukurupuka Mara GHAFLA!..Lowassa Anakata Mitaa ya Miji na Vijiji Kuinadi CCM.
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,963
2,000
Chupa mpya, mvinyo ule ule. Mnakumbuka spidi gavana za magari wakati ule? Ilikuwa tenda ya mtu na lazima kuchukua kwake.

Sitashangaa hili kuna mtu kapewa tenda ya kuuza hizo mashine. Ukileta toka nje, utaambiwa haina kiwango.

Kwa umeme upi wa Bongo? Unakatika toka asubuhi hadi jioni. Muda wa biashara kwa bucha zetu. Hata hao wachache wenye mashine, wana magogo pembeni. Ukikatika, biashara inaendelea.

Awamu hii ni ya aina yake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom