Magodoro Na Mitumba Kama Packing cushions kwenye Container la Magari!

Magodoro Na Mitumba Kama Packing cushions kwenye Container la Magari!

Nani ameona documents za makontena yale..Rais amesema ni mitumba ya nguo ndani yake ni magari ya kifahari..Rais ni mwanasiasa anaweza pia akawa anasema uongo..Bandari wamemfungulia Rais aone ndani ya kontena hawajaweka wala hakuna aliyeweka nyaraka kama kielelezo cha story ile pale..hapo napo ni tatizo kubwa sana. Sijui tuamini Rais kasema au nyarka husika ambazo kaona yeye mwenyewe..au TL Marandu na assumption zake za aina ya usafirishwaji wa magari. Mwisho eti nasikia yale mankotena yanaenda Zambia sio yamekuja Tanzania bandari au TZ ni transit tu basi..hivi tumeibiwa kwa kuwa ni transit country au anaibiwa Zambia anapoelekea mzigo?? Wajuvi mnieleweshe akiwamo mtoa mada.
Kuna mambo mengi huyaelewi wewe au umegubikwa na Siasa. Ule mzigo unaandikwa transit na nadani yake kuna mitumba. Unaondolewa bandarini halafu magari yanashushwa Ilala, inapakiwa mitumba kwenda destination kwa mujibu wa documentation. Huko nako kuna mopkeaji wa hiyo mitumba ambaye ni sehemu ya network, plat # wanabandika za sinza. Mchezo umekwisha.
 
Kwa hiyo tuamini porojo tu wakati mtu huyo akiwa chattle aliwahi kutuambia kuwa kuna meli ziliingia nchini bila kuonekana zikashusha mizigo na kutokomea bila kuonekana,sasa sijuwi meli hizo ni "nyambizi" au za kishirikina!Bila documents ni vigumu sana kumuamini huyu mtu.
Acha porojo na kujitoa fahamu.Meli zimeingia lakini hazikuingiwa kwenye kumbukumbu,genge la wapiga dili wakagawana ushuru wa kutia nanga,kushusha mizigo n.k
 
Acha porojo na kujitoa fahamu.Meli zimeingia lakini hazikuingiwa kwenye kumbukumbu,genge la wapiga dili wakagawana ushuru wa kutia nanga,kushusha mizigo n.k




Hivi kuna kujitoa ufahamu zaidi ya kujifanya unatumbua watumishi hewa huku ukiiacha "hewa ya ukaa" ikitamalaki katika utumishi kwa kutumia cheti na jina feki?

Halafu tukisema mnakimbilia kuuita udaku wakati lisemwalo lina ukweli wa 100%.
 
Punguza mambo yako ya ukabila. That's not even funny.

What's So Funny Bout ???????
You owe it to yourself to find out what you missed. Either way, you'll enjoy finding out "what's so funny here....
Chadema mnatetea wanaotuibia nchi yetu, hii dhambi itawatafuna milele. Mnafeli sana nyie Wachaga kutetea maovu yote yanayopigwa vita na serikali ya Magufuli.
 
Mi nauliza kwanini lema alienda kwenye mkutano wa ACT-wazalendo

haha hapo sasa ndo utajua unafika wa wanasiasa wakati watu waliongoza kumshambulia na kuhakikisha zito anakufa kisiasa ni lema na ACT ilipigwa madongo na akina lema na mbowe kuwa ni CCM B , lakini ghafla lema anahudhururia mkutano wa CCM B na wasaliti wa mabadiliko
 
Lakini document zinaonyesha ndani kuna nguo za mitumba. Mbona mnatetea vitu vya kifisadi nyie ukawa.
Hivi munataka kutudanganya kuwa aliyaagiza yale magar hajui kua bandarin kuna scan inayoweza kuona kilichopo ndani?pili ilikuaje magar hayo yaje na plate no ya tz?hizi sinema za kitoto kabisa nch yenye wasomi hamuwezi kucheza michezo kama hii nikutudanganya.hata hayo makontena ya mchanga bado hainingii akilini kua amekamata sio pipi kua yalifichwa mifukon wakati rais anatoa amri ya kutosafirisha mchanga aliitoa kwenye hadhara hakua amewapa agizo wawekezaji kabla ya kutangaza.maana yake nikua wao walikua wanaendelea kusafirisha kabla amr haijatolewa.hii inaonyesha kua kontena zile zilikutana na amri hiyo zikiwa tayari bandarin.sasaleo useme umezishika kivipi!tutashuhudia mengi sana awamu hii.
 
Magari ni ya nani yaleee? Nasubiri muhusika apelekwe mahakamani baaaas! Sheria ichukue mkondo!
Wala hutakaa uone akipelekwa ila kaa tayar kuona taifa likija kulipa wawekezaji
 
siku ile alikuwa anatafuta kiki tu kumpiku nape kwenye vichwa vya habari
 
View attachment 487098 Sio Kweli ati Kuwa Watu wanaficha Magari kwenye Makontainer ya Magari hasa ya Thamwni ili Kuyaficha. Magodoro makuuku na Mitumba inatumika ili Kuzuia Magarari hayo yasikwaruzike. Kwani Utakuta Marobota Mawili ya Mtumba hata Laki 5 hayafiki kwa hiyo ni Busara kununua Mitumba na Kuitumia kama picking cushions!

Kwa hiyo ni Uwezekano Mkubwa upo kuwa. Ile Movie ya Magufuli ilikuwa ni Kukata Makuguli kwenye container zenye Magari yaliyokuwa yamekuwa cushioned na Mitumba na sio yaliyodanganyiwa ni ya Mitumba!

Kadhalika Pia yamesemekana Kuna Makontainer ya udongo wa dhahabu ambao eti haturuhusiwi kuuona ati Rais anaogopa Tutalia Machozi,

1)Mawazo alipouawa kinyama na kisha akakataliwa asizikwe tulilia machozi
2)Wabunge walipopelekewa Mbwa Bungeni tulilia Machozi
3)Watoto 7900 walipotimuliwa katika stendi za Magari na kuitwa Vilazza Tulitlia Machozi
4)Lipumba alivyosaidiwa na Polisi Kuvunja Ofisi za Cuf tulilia machozi
5)Lema alivhokamatwa kwa kusimulia Ndoto aliyoiota na kuwekwa rumande miezi 4 tulilia machozi
6)Vita vya Madawa vilipogeuzwa na kutumiwa Kisiasa na kuchafuana tulilia Machozi
7)Bashite RC wa Dar alipogeuza Vita vya madawa kuwa mtaji wa kujipatia Magari ya thamani na Magu unaiona hiyo ni kazi, ukamwambia aichape, tulilia machozi
8) Bashite alipovamia Clouds tulilia Machozi.
9) Ulivyotujibu Kunya pale Ubungo tulilia machozi
10) Nape alipolengwa na kutishiwa na bastola, tulilia machozi.

Sasa Kulia Tumezoea Tunataka Kuona kwa kuwakilishwa na Wanahabari, Tunataka kuona Makontena hayo uliyosema na Yale Speaker Ndugai anayosema yote yakifuunguliwa, sio kazi yako Kutuzuia Kulia au kutokulia, Acha tulie nchi ni yetu, macho ni yetu na machozi ni yetu, vinginevyo tutachukulia ni Mediea Manipulation.

Hili ndilo tatizo la watu kama wewe ambae unaishi Marekani na nchi zingine zilizoendelea, kuongea mambo bila kuwa na vigezo na nyezo husika wakati haupo kwenye uwanja wa mapambano.

Mada yako ingekuwa na uzito zaidi kama unavyo vigezo vyote mezani.

Raisi amekwishatoa maagizo makontena yakamatwe na baadae yafunguliwe ili kilichomo ndani kijulikane.

Spika wa Bunge nae ametoa maelezo hayohayo, hivyo hakuna haja ya kuanza kuandika nadharia nyingi kupita kiasi.

Yaani imejaa nadharia zaidi za uhalisia.
 
Kama taarifa zilisema mzigo unaosafirishwa ni magari, na kodi kulipwa ya magari hakuna tatizo. Ubaya unakuja kama taarifa zinasema ni mitumba ndio inasafirishwa kumbe ndani ni magari. Tusiwatetee wanaotuibia. Tukumbuke kuna wananchi masikini na hasa watumishi serikalini ambao wanalipa kodi kila mwezi.
Hivu CT scan yetu haifanyi kazi? Nani mmiliki wa hayo makontena? Tunasubiri nini asishitakiwe?
 
Lakini document zinaonyesha ndani kuna nguo za mitumba. Mbona mnatetea vitu vya kifisadi nyie ukawa.
Ukiwa tatizo ni documents kulikuwa na umuhimu gani wa hiyo drama ya Rais?
Mbona hiyo doc haikuwekwa hadharani?
 
Jaman naomba niwajuze na muache kupotoshana jambo hilo sio kiki kila kitu ni kweli mimi nilikuwepo eneo husika na alokamata ule mzigo ni TRA wengne wameambiwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom