Maggid Mjengwa Akiri CCM ni ya Mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maggid Mjengwa Akiri CCM ni ya Mafisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by admissionletter, Nov 2, 2010.

 1. admissionletter

  admissionletter Senior Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyu Maggid ni mnafiki (hypocrite) kweli kweli. Kabla ya uchaguzi alikuwa akijikomba kwa CCM na kubeza mabadiliko kwa kukejeli kwa maneno mbali mbali kama vile kumuita Slaa ni "mti mmoja ambao hauwezi kujenga msitu." Sasa ameona mabadiliko yanatokea na yeye anabadilisha mwelekeo wa maoni yake. La muhimu kwenye makala yake hii ni kwamba anakiri CCM ni ya mafisadi. Hata hivyo, sikupenda hiyo analogy ya mtu "kuhangaika na kushika titi na kunyonya hata kama si la mama yake" sababu inakejeli mabadikiko. Inabidi aombe radhi kwa hii kauli. Na vive vile, inaonesha bado anadhani CCM itabadilika. Ujumbe wangu kwako Maggid ni kwamba: Its too late for CCM, the train has left the station :
  ................................................................................................

  Na Maggid Mjengwa,

  MTOTO anayetegemea maziwa toka titi la mama anafanyaje anapolikosa? Jibu lake; mtoto huyo atahangaika sana, na kama ataliona titi lingine, atalishika alinyonye, hata kama si la mama yake. Na mtu mzima anafanyaje? Nawe una majibu yako.

  Hatimaye Watanzania tumeshiriki tena kwenye zoezi la kuwachagua viongozi wetu. Katika nchi , matokeo ya uchaguzi yana maana pia ya ujumbe au salamu zinazotolewa na walioshiriki uchaguzi huo, yaani wananchi kwenda kwa viongozi. Nionavyo, matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu yamebeba ujumbe mmoja mkubwa, lakini mfupi sana; MABADILIKO.

  Kwamba umma umeanza kwa dhati kabisa kuonyesha unataka mabadiliko. Hamasa ya kisiasa imeongezeka. Kazi ya wanasiasa na hususan vyama vya siasa ni kusaidia kuyaongoza mabadaliko hayo katika njia salama. Na matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu, kwa mara nyingine tena, kama kutakuwapo na dhamira ya kisiasa, yanakipa Chama Cha Mapinduzi, jukumu hilo kubwa la kuyaongoza mabadiliko hayo.

  Kama Chama Cha Mapinduzi kina nia ya kupunguza kupotea kwa imani ya umma kwa chama hicho, basi, kutahitajika sio tu kufanyika mabadiliko makubwa ndani ya muundo wa Serikali na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi, bali kufanyika kwa mabadiliko makubwa yenye kishindo.

  Kuna watakaopuuza, lakini, kuna ukweli, kuwa tuhuma za ufisadi zimeipaka matope mno CCM. Kwenye macho ya umma, Chama hicho kimechafuliwa na tuhuma hizo za ufisadi. Kuna wana CCM leo wanajiuliza kama wavae sare za chama au la wapitapo mitaani. Maana, kuna Watanzania walioanza kuchukia rangi za chama hicho. Wanazihusisha na ufisadi.

  Na matokeo ya uchaguzi wa mwaka huu yawe ni fundisho kwa chama tawala. Kama CCM inataka kubaki kwenye mioyo ya Watanzania wengi, kuwa na uhalali wa kubaki madarakani, basi, ina lazima ya kujipambanua kwa vitendo kutoka kwenye yote makubwa yenye kuhusiana na ufisadi na maovu mengine. Ibaki kuwa kimbilio la wanyonge. Isifike mahali, Chama kikajikuta katikati ya mgogoro na umma. Hilo laweza kuharakisha mazishi ya chama yasiyo na kisomo. Na hilo ni Neno La Leo.


  ( Neno hilo ni sehemu tu ya makala yangu Raia Mwema, juma hili)

  Maggid,
  Iringa,

  http://mjengwa.blogspot.com/
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Huyu bwwana bora kutomuongelea kabisa manake ni....................... tu!
   
 3. Bob_Dash

  Bob_Dash Member

  #3
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 91
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naye BWABWA NINI?
   
 4. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Another loser.
   
 5. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,042
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Confirmed ni: B.w.a.b.wa
   
 6. B

  Bull JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyie walokole mjadili hoja sio mitsu na dharau.
   
 7. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2010
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,587
  Likes Received: 6,751
  Trophy Points: 280
  Mwacheni Majjid awe na fikra huru, Acheni kufuata mob psychology nyinyi.
  Yeye anaandika anachokiona, anachojifunza, kwa sababu kila siku binadamu anajifunza.
  Matusi hayajengi bali yanaonyesha ujinga, dharau na utwana
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,239
  Likes Received: 414,667
  Trophy Points: 280
  Poor, naive, Maggid...........CCM can only get worse not better.................once you steal the right to rule you will be a thief in Chief in government resisting all forms of reforms............hata NEC kuwa huru na ya haki JK hatataka kusikia katika miaka mitano ijayo.............will you ever learn that sikio la kufa halisikii dawa?
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  hivi huyu ni nani hapa duniani mpaka tumuongelee????????:tape:
   
 10. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Tuachane naye jamani huyu jamaa!!!
   
 11. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145

  Nimecheka mpaka basi lol!! lol!!!! lol!!!
   
 12. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,507
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Jamani kosa la Mjengwa ni nini? Au dini yake
   
 13. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,780
  Likes Received: 6,264
  Trophy Points: 280
  WEWE ndio umesema. Na sijui umefikaje huko. Watch your thoughts mkuu - they determine your character
   
 14. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Huyu ndugu yangu naona kama ni Bendera Fuata Upepo'. Kabla ya uchaguzi alitumia muda mwingi kuipiga madongo Chadema na Slaa bila shaka kama walivyo ccm wengine akiqmini kuwa wangeifagilia mbali chadema. sasa ameona jinsi ambavyo watanzania wanaotaka mabadiliko walivyokikubali kuliko mwaka 2005 sasa anabadilisha upepo kuelekea huko. Gari limejaa.
   
 15. Amigo

  Amigo Senior Member

  #15
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mfa maji haachi kutapatapa
   
 16. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  dah,first lady upo?
   
Loading...