PostGE2025 Magereza yajibu malalamiko ya CHADEMA kuzuiliwa kumuona Lissu gerezani

PostGE2025 Magereza yajibu malalamiko ya CHADEMA kuzuiliwa kumuona Lissu gerezani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
432
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema viongozi wake wamezuiwa kumwona mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu aliyepo katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam.

Lissu yupo mahabusu kwa kesi ya uhaini inayomkabili kwa takriban miezi minane sasa, tangu alipokamatwa Aprili 2025, akiwa mkoani Ruvuma kwa ziara ya chama hicho.

Hata hivyo, Msemaji wa Jeshi la Magereza, Elizabeth Mbezi amesema hana taarifa iwapo kuna zuio la viongozi wa Chadema kumwona Lissu.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema viongozi wake wamezuiwa kumwona mwenyekiti.jpg

Taarifa ya kuzuiwa kumwona kiongozi huyo, imetolewa leo, Jumapili Novemba 30, 2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, Brenda Rupia.Brenda kupitia taarifa hiyo, amesema viongozi hao wamezuiwa kuingia katika gereza hilo siku za karibuni walipokwenda kumuona kiongozi wao huyo.

Pia Soma: CHADEMA: Jeshi la Magereza limezuia viongozi wa Chama kumuona Mwenyekiti Taifa, Tundu Lissu Gereza la Ukonga
 
Sabb za raia kufanya maandamano ni nyingi na za wazi kbs, halafu wanajifanya kujizima data...hakuna anayelipwa hizo ni propaganda za kufanganya wajinga!

Hili la Lissu ni moja ya sabb kubwa za maandamano!
 
Back
Top Bottom