Magereza pagumu kama jwtz?

tizo1

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
856
145
Wadau naomben msaada.Kozi ya uaskari magereza na jwtz ipi ngumu zaid?Nauliza kwa sababu dogo anataka kujiunga sehemu 1 kati ya hizo.huku uswahilin kuna maneno ya kutisha kuliko vitendo!MSAADA TAFADHARI
 
Jeshi zaidi,mshauri aende jeshini...magereza wala usimshauri labda kama ana target zake huko magereza!!!
 
Japo woteni askari lakini nature ya kazi zao zinatofautiana: magereza kulinda wahalifu, Jw kulinda mipaka. Mafunzo yao ni tofauti kwa sababu ya malengo yao kuwa tofauti. Ila wote wanachangia kimoja: utii kwa wakubwa wao. Yeye asichague magereza au JW kwa sababu ya ugumu au urahisi wa kozi. Achague kile kinachokufaa, unachokipenda kadiri moyo unavomtuma; labda pia chenye maslahi zaidi ya kiuchumi kwake na kwa familia yake. Aachane na ugumu na urahisi.
 
Dogo yeye anataka kazi tu.ila kuna watu wamemuambia kwamba magereza pagumu zaid...
 
Sikiliza kwa mafunzo ya kijeshi JWTZ ni ngumu zaidi kulingana na majukumu yao. Sasa kama unataka kazi tu basi achague kati ya mbili hizo lakini nikuulize huyo dogo ana elimu gani kwa msaada zaidi.
 
Mkuu nahisi hamko serious, enzi za kuchagua kazi hasa hizi za majeshi ziliishapita siku nyingi sana. Lakini pia kama sikosei ule utaratibu wa kuajiri JWTZ moja kwa moja ni kama umesitishwa(mtanikosoa) wanachukuwa recruits kutoka JKT, so kwa mwenye bahati na godfather anachukuliwa kujiunga na JWTZ kwa wale wanaobaki kuna wanaopata ajira ya kudumu kwenye JKT na waliosalia tunakutana nao mitaani. Kwa upande wa Jeshi la Magereza nadhani bado wana utaratibu ule wa zamani wa kuchukua maoja kwa moja recruits kutoka mtaani-nahisi inaweza kuwa rahisi kucheza karata zako ili uchaguliwe.

Upande wa mafunzo siwezi ksema sana maana kama wengine wanamaliza iweje dogo ashindwe- anaweza wala asihofu. Mimi nachojua watu tunaangalia maslahi kwanza kabla ya ugumu wa kazi. Kiukweli JWTZ wanalipwa vizuri kuliko Magereza, hili liko wazi.
So, mi namshauri dogo kama anataka kazi asiwaze ugumu wa kazi, yeye akomae tu. Lakini pia kama anataka ulaini wa mambo mwambie arudi shule.
 
Da! kama kuna alternative mwambie dogo asijiunge na jeshi lolote, a'fight ajira nyingine.
 
Dah dogo kasoma mpaka fm 6 akapata div 4.Dogo anataka jesh halafu muoga sana.nimempa asome maoni ya wadau kafurahia na anajidai yupo fit kwenda popote.ILA ANACHOTAKA NI KUJUA HALI HALISI YA JESHINI ANAOGOPA KUTESWA KULIKO MAELEZO.NI KWELI UKIANZA KOZI MAGEREZA UNAPEWA NUSU MSHAHARA?
 
dogo acha uoga hakuna kazi nyepesi katika maisha, na kmunataka ulaini nenda posta kalambe stamp, umenipata? au kafanye kazi ya laana ya kuokota chupa za uhai.
 
dogo acha uoga hakuna kazi nyepesi katika maisha, na kmunataka ulaini nenda posta kalambe stamp, umenipata? au kafanye kazi ya laana ya kuokota chupa za uhai.

Ni rahisi Askari magereza kuwa mfungwa kuliko Mfungwa kuwa askari magereza,ni mtazamo tu wakuu msijenge chuki zote kazi!
 
Wadau naomben msaada.Kozi ya uaskari magereza na jwtz ipi ngumu zaid?Nauliza kwa sababu dogo anataka kujiunga sehemu 1 kati ya hizo.huku uswahilin kuna maneno ya kutisha kuliko vitendo!MSAADA TAFADHARI

Kote pagumu.
 
dogo acha uoga hakuna kazi nyepesi katika maisha, na kmunataka ulaini nenda posta kalambe stamp, umenipata? au kafanye kazi ya laana ya kuokota chupa za uhai.

dah kuna watu wameenda shule na bado wanaokota chupa.unamjua ticha?ni muokota chupa mwenye elimu nzurii!ni maarufu sana hapo dsm
 
dogo kapata zero=four form six halafu bado anachagua kazi? Mwambie kuna nchi mtu akipata ziro na four ananyongwa ..dogo amepata hata muda wa kuchagua kazi? Lol!! Anabahati kweli kweli dogo wengine hizo bahati hawana kabisa
 
mwambie aende JWTZ magereza hapana mpango biashara ya kumchunga mwanadam mwenzio ni utumwa
 
Back
Top Bottom