tatanyengo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2011
- 1,134
- 280
Pengine katika kudhihirisha kuwa watanzania wamechoka na mbio za Mwenge za kila mwaka, magazeti ya Tanzania hayaandiki tena habari hizo. Ikumbukwe kuwa mbio za mwenge kwa mwaka 2014 zilizinduliwa na Dr.Gharib Bilal tarehe 2/5/2014 katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Pia uzoefu unaonyesha kuwa hata miradi inayozinduliwa na mbio hizo hutelekezwa. Pengine muda umewadia wa kutafakari kama vema kuendelea na mbio hizo au la.