Magazeti yasusia mbio za Mwenge

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Pengine katika kudhihirisha kuwa watanzania wamechoka na mbio za Mwenge za kila mwaka, magazeti ya Tanzania hayaandiki tena habari hizo. Ikumbukwe kuwa mbio za mwenge kwa mwaka 2014 zilizinduliwa na Dr.Gharib Bilal tarehe 2/5/2014 katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Pia uzoefu unaonyesha kuwa hata miradi inayozinduliwa na mbio hizo hutelekezwa. Pengine muda umewadia wa kutafakari kama vema kuendelea na mbio hizo au la.
 
mimi ninajenga kakibanda kangu nataka mwenge uje uzindue.
utakuwa umechok na wananchi kwa sababu mwenge wa zmn ulikuwa unamulika wezi, majangili, lakini wa sasa unawamulikia ili waibe, naona na wananchi wamestuka sasa.
 
Mkuu mleta mada kumbuka sasa hivi bungeni kuna ile kauli ya ndimi mbili pia zama za uongo zimekwisha naona anguko la Jk
 
Bahasha adimu labda siku hizi,si mnaelewa maisha yao yanavyokuwa hawa ndugu zetu bila bahasha na appointment
 
Pengine katika kudhihirisha kuwa watanzania wamechoka na mbio za Mwenge za kila mwaka, magazeti ya Tanzania hayaandiki tena habari hizo. Ikumbukwe kuwa mbio za mwenge kwa mwaka 2014 zilizinduliwa na Dr.Gharib Bilal tarehe 2/5/2014 katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Pia uzoefu unaonyesha kuwa hata miradi inayozinduliwa na mbio hizo hutelekezwa. Pengine muda umewadia wa kutafakari kama vema kuendelea na mbio hizo au la.

ukawa mkichukuwa nchi mwaka 2015
 
hapo sipati picha hiyo mikesha yake....

Hii kitu imechokwa na wananchi lakini chama twawala inapeleka mafungu kila sehemu ili hata wanafunzi masomo yasimame kuongeza idadi ya watu:smile-big:
 
Wazo langu ni kuishauri Serikali Kama kuna uwezekano wafanye maadhimisho ya Mbio za Mwenge kila baada ya miaka mi5 au 10, yaani kuwe na interval fulani hivi ili kupunguza matumizi mabaya ya fedha za walipakodi wa Tanzania!!!
Nawakilisha....
 
Back
Top Bottom