Magazeti yaache kuandika yaliyojadiliwa bungeni waandike maamuzi yaliyofikiwa bungeni tu

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Yaani magazeti unakuta yanahangaika kuandika mambo yaliyojadiliwa bungeni sijui mbunge gani alisema na mwingine akadakia na mwingine akazomea nk.Wanapotezea muda wananchi.Hoja ikitolewa na waziri wabunge hupewa nafasi ya kujadili kila mtu kwaupeo wake wa akili wenye akili na wale nusu kaputi kila mtu hupewa nafasi.Cha muhimu kwa wananchi siyo hayo makorokoro yaliyotokea humo kwenye majadiliano kinachotakiwa ni mwishoni kiliamuliwa nini? Hiyo ndiyo habari ya muhimu kwa wananchi.

Yaani vyombo vya habari vinapoteza muda kupeleka waandishi Dodoma kwenda kuandika kilichoendelea kwenye majadiliano !!!!! WASTAGE OF THEIR MONEY.

Wangeambiwa tu wakae vituo vyao vya kazi wasubiri maamuzi yaliyofikiwa kwenye mijadala wapewe na maafisa habari wa bunge.Lakini eti kuweka mwandishi bungeni eti kujuza yanayoendelea wanavyoendelea kujadili naona ni upuuzi na upotezaji pesa tu.

Mfano sehemu zingine kukiwa na tukio utakuta waandishi wa habari wanafika tu ufunguzi halafu wanakuja mwisho kuchukua maamuzi yaliyofikiwa kwenye mkutano au kongamano.Huwaoni hapo muda wote wakati mijadala inaendelea kwenye hiyo mikutano au makongamano.
 
Back
Top Bottom