Kutoka kwa DOTTO BULENDU
Toka niione clip ya video ikimuonesha mwanafunzi wa shule ya sekondary huko Mbeya akiadhibiwa na walimu, ambao taarifa zinasema walikuwa kwenye mafunzo ya vitendo,na jinsi jamii ilivyojadili tukio hilo na serikali kutoa tamko lake linalozunguka humu mitandaoni,huu ni uthibitisho tosha kuwa mitandao ya kijamii si kitu kibaya,mitandao ya kijamii ni ulingo mzuri,ukitumiwa ipasavyo utaleta mabadiliko makubwa ndani ya jamii yetu,najiuliza isingekuwa mitandao ya jamii nani angelijua tukio hilo?mitandao ya kijamii kwa mtazamo wangu ina faida kubwa kuliko hasara,"wale unethical social media users"ndiyo tatizo,mitandao yenyewe si tatizo hata kidogo.Nimependa jinsi waziri Mwigulu anavyotumia mitandao siku ya leo kutoa ufafanuzi juu ya tukio hilo,nimependa jinsi waliopo Mbeya wanavyotupa taarifa sahihi,nimeona mpaka barua ya mkuu wa shule husika,kitu ambacho huwezi kiona kwenye vyombo vingi vya habari.Tusiilani na kuitungia sheria mbaya mitandao,tuendelee kupeana elimu juu ya faida ya mitandao ya kijamii katika kusukuma maendeleo.