Magari ya Rais yazimika tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magari ya Rais yazimika tena

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bagamoyo, Jun 9, 2010.

 1. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,519
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  Magari hayo ya ulinzi yaliyowekewa mafuta kwa ajili ya kujiandaa kwenda Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) kwa ajili ya kumpokea Rais Jakaya Kikwete, ambaye alitarajiwa kuwasili saa 11:40 jioni.

  Habari za uhakika zilizothibitishwa na maofisa wa vyombo vya dola ziliidokeza Mwananchi kuwa kituo hicho kimewekwa chini ya ulinzi wa polisi na maofisa Usalama wa Taifa na watu watatu wanashikiliwa na polisi.

  Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, mara baada ya magari hayo aina ya Toyota VX V8 rangi nyeusi kuweka mafuta, kifaa maalumu (sensor) ndani ya magari hayo kilibaini kuwa mafuta hayo hayana ubora unaokubalika.

  Jitihada za maofisa usalama kuyawasha magari hayo zilishindikana hadi mafundi wa kampuni ya Rajinder Motors walipoitwa na kumwaga mafuta yote yaliyokuwa yamewekwa katika magari hayo.
  Endelea kusoma sakata zima lilivyotokea mkoani Kilimanjaro kama ilivyoripotiwa na gazeti la Mwananchi Link:
  Magari ya Rais yazima tena safarini
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  na ule mwendo wanaoendaga kwakweli, kama gari haijakaa sawa, rais wetu tutaenda kumwokota uchochoroni karushwa...
   
 3. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaa waache mchezo hadi gari la rais kuwekewa maji badala ya diesel UWT wako wapi, kuna siku rais tutamtoa chini ya uvungu wa gari bado Rweyemamu atadai ni mambo ya kawaida tu.
   
 4. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  That tells me jinsi gani vyombo vetu vya usalama vimeanza kuzembea kiasi cha kuyachukulia mambo ya msingi kirahisi rahisi tu. Hivi jamani, gari ya raisi inajazwa mafuta popote? Anyway its a good thing kwamba haikuleta madhara kwa raisi. Ila on the other side raisi naye ajue ni jinsi gani wananchi wanapata hasara ya kuharibbikiwa na magari yao kutokana na kuuziwa mafuta machafu ama yaliyochanganywa.

  Mr Presidaa, how does it feel? Sucks huh...? Thats Tanzania friend, get used to it or do something about it. Hivi kwani SUMATRA inapanga bei ya mafuta tu? Hao SUMATRA wakishirikiana na TBS, TRA, POLISI hivi majanga kama haya hayataisha upesi Mr Presidaaa?

  Natishika na muenendo wa maadili wa vyombo vya umma. Mbona sioni nidhamu na maadili ya kweli toka moyoni? Nikitazama naona maadili, uwajibikaji na nidhamu ya unafiki tu pindi pale unapofika wewe Mr Presidaa ama Waziri Mkuu ama Makamu wako. Tunakwendaje namna hii?

  NIDNAMU........ NIDHAMU............... NIDHAMU............. NIDHAMU.............. NIDHAMU.......... NIDHAMU........ NIDHAMU......... NIDHAMU

  UADILIFU............. UADILIFU.................... UADILIFU........................UADILIFU.......... UADILIFU................. UADILIFU

  UWAJIBIKAJI........................ UWAJIBIKAJI.................. UWAJIBIKAJI..................UWAJIBIKAJI

  Ukosefu wa hayo ni mojawapo ya magonjwa yanayoambukiza sana katika serikali na vyombo vya umma kwa hivi sasa. Matokeo yake ni RUSHWA na KUDUMAA kwa huduma na hatimaye kila kitu kupewa uthamani wa hela. Imefika mahali nikitaka uwajibikaji nitumie pesa, nikitaka uadilifu nitumie pesa, nikitaka nidhamu nitumie pesa. Tutafika?

  TRA mpo?
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,999
  Trophy Points: 280
  Kikwete anahujumiwa na nani?
  Nyere magari yalikuwa ya gharama nafuu sana na yalikuwa hayazimiki .
  Mwinyi naye hali kadhalika.
  Mkapa hatujawahi kusikia hata siku moja kuwa gari lake limezimika wala kung'oka matairi.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  nimesema nyie ngojeni tu.. siku moja watashtuka wako angani na rubani wamemuacha ardhini!
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Hili tatizo ni kubwa sana na ukweli ni kuwa Ewura na Serikali wanalilea.

  Haiwezekani price ya mafuta Dar ikawa ni kubwa kuliko ya Arusha na Moshi especially baada ya transportation charges. Entry point ya mafuta mengi ni Dar. Lakini pamoja na kujua tatizo, Ewura inaelekea kuna watu wanapona kwa kupewa chochote kitu.

  This is not a wake up call...it is a call for action. Hizi rushwa kuna siku tutaangusha ndege. Badala ya kuweka mafuta tutaweka maji.!!!
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Jun 9, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Kama mambo yenyewe ndio hivi tusubiri janga kubwa zaidi kwa rais WETU.
   
 9. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  duh.....hivi ule utaratibu wa magari ya serikali kuchukua mafuta ujenzi siku hizi haupo?
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Da! Hiyo itakuwa kali sana.
   
 11. kmp

  kmp Member

  #11
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  “Tayari wataalamu wa Ewura wako njiani kuja Moshi kwa ajili ya kuchunguza kituo hicho kama kulikuwa na hujuma kwa msafara wa Rais Kikwete au ni hujuma za uchanganyaji wa mafuta,” kilidokeza chanzo kimoja cha habari.

  Nimesoma habari hii na kuchukua sehemu tu ya article nzima kutoka kwenye webpage ya mwananchi, hivi hawa EWURA wanasubiri mpaka magari ya ikulu yazime ndio wachunguze, wananchi wanalalamika kila siku kuhusu mafuta machafu lakini hatua hazichukuliwi au hata zikichukuliwa ni baada ya muda mrefu sana.

  Sina records za vituo vingapi vimefungiwa kwa kuuza mafuta machafu, mwenye hizo data atuwekee hapa jamvini lakini ni kwamba wanasubiri mpaka mkubwa fulani apate mapatizo ndio washughulike then kwisha.

  Hizi taasisi zetu je zimeundwa ili kufanya kazi kwa ajili ya wakubwa tu?

  Angalia hata barabara zinakarabatiwa mara tu wanaposikia raisi anakwenda kufanya ziara, hivi hizo barabara nzuri ni kwa ajili ya kupita raisi na wateule wachache tu?

  Hivi tutafika kweli kwa hali hii jamani????

  Aha, lakini wote wakumbuke kwamba ANYTHING GOES AROUND COMES AROUND!!!!

  Let the chosen ones also fill the pitch which the non chosen ones (wananchi)are feeling!
   
 12. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #12
  Jun 9, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,848
  Likes Received: 2,423
  Trophy Points: 280

  ...msijisumbue kuwalaumu ewura wala mwenye kituo...kikwete anapambana na maaadui zake anaowajua na hii ni impact.....kosa kubwa la kikwete ni kuwa wakati anagombea kuanzia mwaka 1995 na hata mwaka 2005 aliwaumiza watu wengi mno[political suicide]..kupitia mtandao wake ambao haukuwa na huruma wala simile......kosa kubwa alilofanya ambalo wanasiasa wengi wastaarab hufanya ..hakukutana na maasimu wake ili kuweka mkono wa maridhiano na ikibidi kumbana radhi....for sure now this people are heating him back from all angles........haiwezekani ndani ya wiki 2 anakuana na mauza uza ya ajabu...acha yale ambayo hatuyajuwi...alafu eti watu waseme rais wenu yupo salama...no...no..no!!!

  namuonea huruma sana rais...kwani anayo safari nzito mbele yake.....na kama hata gari zimepenyezewa mafuta machafu basi..tujuwe hata ndege inaweza kuwekewa mafuta machafu.......na ni bora huko mbeleni wanasiasa wakajifunza kutauta nafasi za kisiasa bila kuchafuana...na kuacha makundi !!!
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Inabidi Rais mwenyewe awe makini na uhai wake lasivyo mmmh tunaweza anza kuongea mengine hivi kituo hicho ni BP au TOTAL maana hawa wanasifika kwa kuuza mafuta yenye kiwango cha juu kama hao madereva walijiamulia kujaza kwenye vituo bubu vya kitaa lazima madereva washikiliwe na si wamiliki wa kituo
   
 14. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  HTML:
  
  
  Kwani siku hizi hakuna 'depot' ya serikali ambapo magari yanatakiwa kujazwa mafuta katika hizo depot? Usalama kwanza... haya mambo ya kubinafsisha kila kitu mwisho wake unaweza kuwa mbaya.
   
 15. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #15
  Jun 9, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,848
  Likes Received: 2,423
  Trophy Points: 280

  nashangaa wao walifikiri walioweka utaratibu huu wajinga ...siku hizi mabepari ndio wanajaza mafuta ya misafara ya rais...zile idara za ufundi na umeme ,karakana,commonworks,bohari za mikoa, alizoanzisha mwalimu wameziuwa ili wao wanasiasa wauze mafuta yao au wanakopewa chochote....ukiweka mafuta pale rso anakula hadi dereva...ukiweka bohari ya mkoa ..atakula dereva peke yake kwa kupiga nyoka mzee akiondoka!!!!..du!!!...all in all idea ya mwalimu ilikuwa kuweka udhibiti wa magari ya umma kuanzia matengenezo yake hadi mafuta kwa usalama wa dola kwa ujumla.....sisi tumeuwa hiyo.....kaakana za serikali haziwezi hata kubadili matairi siku hizi ..na zilikuwa kila mkoa!!!!
   
 16. M

  Malila JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Mramba yalimkuta hayo akiw mafinga,maadamu na mheshimiwa kaona live,labda serikali inaweza kuamka.
   
 17. bona

  bona JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  am i missing a point? ivi rais anaweka mafuta ya kijiko kwenye vituo vya mitaani? moshi hamna ikulu ndogo yenye pump ya mafuta? kama naota vile!
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Uzuri wa serikali yetu mpaka litokee janga limkumbe mkubwa ndo wanakumbuka kumulika wanajaua kuwa aaah kumbe kuna giza hapa...
   
 19. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hiyo ni sabotage!!! iko wazi na bado... tutasikia mengi kwani aliowaumiza wako wengi na kibaya zaidi wanawatumia watu walewale aliowatumia yeye!!!!
   
 20. F

  Froida JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kikwete anatakiwa aondolewa kwa box la kura lakini sio kumfanyia vitu vya aina hii vya kutaka kuhatarisha maisha yake bila sababu amfute kazi mkuu wa itifaki ikulu akingojea mengine yatokee watammaliza,hawana nia njema mambo gani hayo bwana waache uzembe ujinga mtupu kabisa yaani hawana vituo maalumu wanaweza wakajaza mafuta popote pale ,hii ni hatari sana hatuna tena watu tuliokuwa tunawaamini waliokuwa wnalinda viongozi wetu ,mbaya,mbaya mbaya ,KIKWETE fukuza mkuu wa itifaki hapo IKULU wanakula bure kodi za wananchi
   
Loading...