TANZIA Magambo Makongoro Amefariki Dunia

Kuna yule Dada wa USA Linda Beizedenhout amezaa na huyu Magambo anamislead watu kuwa ni mtoto wa Nyerere sasa wengi wanadhani ni Makongoro Nyerere ndio kafa.

Hebu tudadavulie kwa faida ya JF, Chifu Makongoro amefariki kabla Uhuru mwaka 1958, je Nyerere alimchukuwa huyu Magambo Makongoro na kumlea ndio sababu anaonekana ni kama mtoto wa Nyerere wa kumzaa?

Mwisho ningependa kujuwa huyu Magambo Makongoro Uislamu ameupata wapi kama amekulia kwenye familia ya kikatoliki?
 
Ningeshangaa kuandika bila kumtaja Sykes
 
Poleni sana kwa msiba. Ila mzee Mohamed ulivyohadithia ni kuwa ulipata fursa kubwa ya kukua na watu wazito wa nchi hii ila nashangaa huu UDINI ulio nao umetokana na nini?
Kizee na udini wa kenyewe kamebaki kanapigwa vumbi tu! Kamekua na kukaa na watu wazito mtaani lakini hakajanufaika na chochote itakuwa kalikazania madrasa badala ya elimu dunia!
 
Pole sana.

RIP Magambo Makongoro.
 
St. Joseph's Convenient.
St. Joseph Convent(baadaye Forodhani).
 
Ningeshangaa kuandika bila kumtaja Sykes
Njinjo,
Sykes katika makala hiyo nimewataja wawili - Kleist Sykes na mdogo wake Ebby Sykes.

Hawa ni watoto wa Abdulwahid Sykes.

''Magambo alikuwa mwenzetu na mchezo wetu ulikuwa mmoja pamoja na Kleist na mdogo wake Ebby, Yusuf Zialor, Wendo Mwapachu, Bubby Bokhari, Christopher Faraj, Abdallah Mohamed Saleh (Tambaza), Abdul Mtemvu, Edward Makwaia (sasa Chief wa Siha), Abdallah Mgambo, Eyshe na Mariam Max, Erica Kisa, Janet Zebedayo, Haitham Rashid, Esther Mzena wenzetu wengine wengi siwakumbuki.''

Ndiyo rafiki zangu hawa na ndugu zangu tumekua sote toka udogoni mchezo wetu mmoja.

Bahati mbaya kama unakasirishwa na historia hii.
Hatukupanga sisi.

Tumezaliwa Mtaa wa Kipata (Sasa Mtaa wa Kleist Sykes) na wengine Mtaa wa Stanley (sasa Max Mbwana) hapa Dar es Salaam 1950s tumewakuta baba zetu majirani na marafiki.

Na hawa baba zetu wamezaliwa 1920s wamewakuta baba zao majirani na marafiki.
Angalia picha hiyo hapo chini wakati wa ujana wetu tuko sekondari ni mwaka wa 1968.

Kleist yuko katika hiyo picha na mimi nipo pia.
Na hao wengine niliowataja wako katika picha hii:

Picha hii hapo chini tuko Kigamboni Picnic nia katika miaka hiyo hiyo tuko sekondari na hii ni hiyo nyumba ya mapumziko ya State House niliyoeleza katika makala yangu na baadhi ya walioko kwenye picha ya juu wapo hapo.



Picha hii sasa sisi ni watu wazima tumepiga Kigamboni nyumbani kwa Lily Sykes na niko katika picha hii pamoja na Kleist Sykes, Abdallah Tambaza, Bubby Bokhari na Abdul Mtemvu tulikuwa katika picha ya 1968.

Picha hiyo ya kwanza na hii zimepishana kwa nusu karne yaani miaka 50 kama nilivyoeleza hapo juu baadhi tulikuwakokatika picha ya kwanza 1968 tupo pia katika picha hii: Kleist, Bubby, Tambaza na Abdul.

Unataka nifute historia hii ya maisha yangu?
Inawezekana?

Unaweza kuwafuta ndugu na marafiki zako katika maisha yako?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…