Mafuvu 40 ya watu yakutwa chini ya mbuyu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafuvu 40 ya watu yakutwa chini ya mbuyu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kasheshe, Jan 16, 2009.

 1. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mwandishi Wetu
  Daily News; Friday,January 16, 2009 @20:00


  JESHI la Polisi mkoani Shinyanga limegundua mafuvu 40 ya binadamu na mifupa mingine katika shimo chini ya mti wa mbuyu.Taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Shaibu Ibrahim, ilisema mafuvu 35 yaliweza kuhesabika na mengine matano yalikuwa vipande vipande.

  JESHI la Polisi mkoani Shinyanga limegundua mafuvu 40 ya binadamu na mifupa mingine katika shimo chini ya mti wa mbuyu.Taarifa iliyotolShaibu Ibrahim, ilisema mafuvu 35 yaliweza kuhesabika na mengine matano yalikuwa vipande vipande.

  Ilisema mafuvu hayo yaligundulika Januari 13 mwaka huu saa 10 jioni, mbali kidogo na makazi ya watu katika kijiji cha Mayangi kata
  ya Ukenyenge wilayani Kishapu.

  Kamanda Ibrahim alisema inaonekana mafuvu hayo yaliwekwa katika eneo hilo kwa muda mrefu bila kutambulika na hata hivyo umri wa binadamu wenye mafuvu hayo haukuweza kujulikana mara moja. Taarifa ya Kamanda huyo ilisema mafuvu hayo yamehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi, ili kubaini umri na jinsia ya binadamu wanaohusika nayo.

  Tukio hilo limejitokeza huku wimbi la mauaji ya maalbino likiwa limeelemea zaidi maeneo ya Kanda ya Ziwa, pia mauaji ya vikongwe ambayo zamani yalisikika sana maeneo ya Shinyanga. Hata hivyo, haijaweza kubainika kama yana uhusiano na mauaji hayo, hadi uchunguzi utakapokamilika na kubaini ukweli.

  Pia Kamanda Ibrahimu alisema katika matukio tofauti mkoani humo, watu wawili wamekufa akiwamo mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Butambata, Buya Joel, kwa kutumbukia kwenye kisima wakati akichota maji.

  Alisema tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita jioni katika kijiji cha Butambala wilayani Bukombe wakati mwanafunzi huyo akichota maji katika kisima cha nyumbani kwao na polisi wanaendelea na uchunguzi kujua sababu za tukio hilo.

  Alisema siku hiyo mchana, katika kijiji cha Nyasubi mjini Kahama, mwanaume mmoja (30-35) aliuawa na wananchi na kuchomwa moto kwa tuhuma za kuwa mwizi wa dirishani.

  Katika tukio lingine, Polisi ilifanikiwa kumkamata jambazi sugu aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu, Mseveni Jonathan (34) mkazi wa Majengo Ushirombo akiwa na risasi mbili za SMG na SAR vikiwa nyumbani kwake Jumatano iliyopita jioni.
   
 2. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Hiyo lab ya sayansi.
   
 3. Kafara

  Kafara JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2009
  Joined: Feb 17, 2007
  Messages: 1,392
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  kama kuna watu waliokamatwa wanaweza kusaidia uchunguzi.

  japokuwa tunadai tunaamani lakini mambo mengine yanayotendeka
  yanafanya mtu ujiulize amani hii tafsiri yake ni nini? je mtu/jamii
  ya watu kuishi katika mazingira kama hayo yanayopelekea vikongwe
  na maalbino kuuawa ana/wanayo amani?
   
 4. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  kwa akina NN huko
  tena chini ya mbuyu hao lazima watakuwa walikuwa wanagawana mavuno au ndio sehemu zao za kufanyia kalamu.....
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Jan 17, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hisije ikawa na mahusiano na yale mauwaji yaliotokea Shinyanga miaka ile ya Themanini (80)...!

  Tusubiri wataalam wetu wa kitengo cha CSIs (Crime Scene Investigators) {...Kama kipo} watatuambia nini...!
   
 6. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mama We! :eek:
   
 7. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  KATIKA tukio lisilo la kawaida nchini, mafuvu 40 ya vichwa vya watu yamegundulika yakiwa yamefukiwa ndani ya pango lililo chini ya mti wa mbuyu, kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga.


  Matukio kama hayo yamekuwa yakiripotiwa kwenye nchi zilizowahi kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, lakini Jeshi la Polisi limeeleza kuwa limegundua mafuvu hayo katika kijiji cha Mayangi kilicho katika Kata ya Ukenyenge tarafa ya Negezi wilayani Kishapu.  Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, ACP Shaibu Ibrahim alisema jana kuwa mafuvu hayo yalikutwa pamoja na mabaki mengine ya miili ya binadamu.


  Alisema tukio polisi walibaini mabaki hayo ya binadamu Januari 13 wakati walipoenda kwenye eneo hilo majira ya saa 10:35, ingawa taarifa yake haikueleza kiini cha kwenda eneo la tukio kufanya uchunguzi uliosababisha kugundulika kwa mabaki hayo.


  "Kati ya mabaki hayo, mafuvu 35 yaliweza kuhesabika na matano mengine kukutwa vipande vipande na yalikutwa yamefunikwa pangoni chini ya mti wa mbuyu," alisema


  Kwa mujibu wa Kamanda huyo, inaonekana mafuvu na mifupa hiyo ya watu wasiofahamika, imekuwapo eneo hilo muda mrefu bila kujulikana.


  "Pia hatukuweza kufahamu mifupa na mafuvu haya na ya watu wa jinsia gani lakini tumeyahifadhi kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kubaini umri na jinsia za watu hao," alisema.


  MAfuvu hayo yamechukuliwa na kuhifadhiwa kwenye kituo cha polisi cha mkoa jana huku polisi hao wakiwa na vikao kadhaa vya ndani kujadili suala hilo.


  Iwapo si mauaji ya watu wengi, mabaki hayo yanaweza kuwa yanatokana na imani za watu wengi kuwa wakoloni walipoondoka waliacha madini, na hasa rubi, chini ya miti ya mibuyu, imani ambayo hufanya watu wengi wanaoishi kwenye maeneo yenye madini kuchimba mashimo marefu karibu na mibuyu kusaka vito hivyo.


  Hata hivyo, idadi ya mafuvu hayo ni kubwa. Si rahisi watu 40 kuchimba shimo moja na kuingia kusaka madini yaliyoachwa na wakoloni na ukweli kwamba mabaki hayo yalikuwa yamefunikwa unaacha maswali mengi, hasa kwenye maeneo hayo ambayo yamekuwa na mauaji makubwa kutokana na imani za kishirikiana.


  Katika matukio mengine watu wawili wamekufa mkoani Shinyanga katika matukio tofauti likiwemo la mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi kufa maji baada ya kutumbukia kwenye

  kisima.


  Kamanda Ibrahim alisema tukio la kwanza lilitokea Januari 13 mwaka huu majira ya saa 12:00 jioni katika Kijiji cha Butambala kilicho Kata ya Ushirombo wakati mwanafunzi wa darasa la kwanza

  katika Shule ya Msingi Butambala, Buya Joel, 18, alipokufa maji baada ya kutumbukia

  kwenye kisima wakati akichota maji eneo la nyumbani kwao.


  Kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi kuwa makini na watoto wao hasa katika kipindi hiki cha mvua, akitaka wasiwaruhusu kwenda kuchota maji peke yao.


  Matukio ya watoto kutumbukia kwenye visima yamekuwa yakiongezeka mkoani Shinyanga

  kutokana na wananchi wengi kujihusisha na machimbo ya madini aina mbalimbali na

  pindi wanapopata au kukosa madini hayo, huyatelekeza bila ya kuyafukia.

  Source:Mwananchi


  Mashimo mengine hutokana na watu kutafuta maji wakati wa kiangaz na hivyo kuwa hatari wakati mvua zinapoanza.


  Katika kipindi cha mwaka 2007, watoto wadogo zaidi ya 10 walitumbukia na kufa

  maji kwenye visima mablimbali katika maeneo tofauti mkoani Shinyanga, zikiwemo wilayaza Kahama, Bukombe na Shinyanga.
   
 8. C

  Canady Member

  #8
  Jan 17, 2009
  Joined: Jan 1, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu kunakazi duniani, mungu atusamehe AMEEEEEN.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,703
  Likes Received: 82,626
  Trophy Points: 280
  Mass grave with at least 40 bodies found in Shinyanga

  THISDAY CORRESPONDENT
  Shinyanga ​

  A MASS grave holding the remains of more than 40 people has been discovered in Shinyanga, sending shock waves across the region.

  Police officials say they believe the mass grave is at least 20 years old.

  The Shinyanga Regional Police Commander, Assistant Commissioner of Police (ACP) Shaibu Ibrahimu, told reporters that the grave was discovered yesterday.

  He said the human remains were discovered in Mayangi Village, Ukenyenge Ward, Kishapu District, some 65 kilometres from Shinyanga Municipality.

  The RPC said some villagers had tipped off the police about the existence of the mass grave, which was discovered inside a cave under a huge baobab tree within the village.

  Police could not immediately establish the cause(s) of death of the human beings whose remains were found inside the grave.

  Said RPC Ibrahimu: ’’A team of doctors from the regional hospital assisted the police in retrieving the remains from the grave. They (doctors) ascertained that the grave must be about 20 years old.’’

  He said a formal statement will be issued after doctors at the Shinyanga Regional Hospital conclude their own thorough examination of the human remains from the grave.
   
 10. T

  Tango Member

  #10
  Jan 18, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  This is really shocking...how this can happen in a 'peaceful' country like ours? naomba kama kutakuwa na update uendelee kutujulisha mzee.
   
Loading...