Mafuta yameanza kuchimbwa Tanzania

Andrew Kellei

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
348
123
Wadau,leo asubuhi nilikua nasikiliza redio MAGIC FM katika kipindi cha morning magic,katika kile kipindi cha zaidi ya habari mwandishi Kibwana Dachi ametuambia leo ni siku ya tatu (3) tangu mafuta yaanze kuchimbwa Tanzania.Kwa siku wanachimba mapipa 100 (mia moja).Hii ina maana kwmba tayari watakua wamechimba mapipa mia tatu.
Swali la kujiuliza ni kwamba,mbona hii ishu ipo kimya kimya sana?
Ina maana serikali haijui au wanataka kutuambia kuwa bado jamaa wanafanya utafiti?
jamani hebu tulifuatilie kwa kina hili jambo isije kuwa ndo mtindo ule ule wa wachimba madini.
Nawakilisha.
 
yanachimbwa sehemu gani? sisi tusitegemee kitu chochote kutoka kwenye hayo mafuta.....wametumia ghrama nyngi sana kwa hiyo wakijilipa na kilichobaki kikichotwa na mafisadi ndio basi hatubakiwi na kitu.
 
Hivi kuna ukweli hapa?
-Swali la kwanza hujataja eneo, well
-Lakini inawezekana kuwa siku ya kwanza ya uchimbaji wakapata pipa 100, ya pili 100 na ya tatu?...unless kama matayarisho ya awali yalishafanyika tayari, na hiyo unayoongelea wewe ni Official commissioning kamili ya kazi yenyewe, na si majaribio.
Na je tayari kuna mitambo ya PROCESSING ya hayo mafuta ghafi, au unaposema pipa 100 una maana yaliyosafishwa?
 
Yanachimbwa Mtwara huko walikokua wanafanya utafiti wa siku nyingi sana.Nafikiri kunaitwa Mnazi Bay.
 
Hivi kuna ukweli hapa?
-Swali la kwanza hujataja eneo, well
-Lakini inawezekana kuwa siku ya kwanza ya uchimbaji wakapata pipa 100, ya pili 100 na ya tatu?...unless kama matayarisho ya awali yalishafanyika tayari, na hiyo unayoongelea wewe ni Official commissioning kamili ya kazi yenyewe, na si majaribio.
Na je tayari kuna mitambo ya PROCESSING ya hayo mafuta ghafi, au unaposema pipa 100 una maana yaliyosafishwa?
Pakajimmy,
Ukweli upo huyo mwandishi kasema aliongea na wachimbaji wenyewe na tena ameshauri tumwulize waziri ili aliweke sawa.Hayo mapipa mia ndo uwezo wa mitambo yao kuchimba kwa siku ila ni ambayo hayajwa processed.
 
wadanganyika mnataka mpewe taarifa ya mafuta ya kitu gani bana.
Maji yenyewe serikali yenu imeshindwa kuwapa maji itakuwa mafuta?
 
Jamani Haya mapipa kamwe hayatamsaidia mkulima wa miwa, mpiga debe wa daladala, muokota chupa za plastiki, msukuma mkokoteni, mama lishe nakadhalika.

Haya mafuta ni kwa ajili ya wanene, wabenzi, waheshimiwa etc Kama ulivyo kwa dhahabu, sie tulie tu, midomo juu ka mbwa, hatutaambulia kitu.
 
ukisikia mia ujue ndo mia mara mia...ridhiwan yupo kwenye biashara ya mafuta hapo ndipo napopaogopa mimi.
 
wewe sema Unafanya Biashara tu ya mafuta,maana ukikutaka mafuta hayapatika nenda BIgBon hivi Bigbon ya Nani?Naomba kuambiwa na evidence kama mtu anayo
 
Wadau,leo asubuhi nilikua nasikiliza redio MAGIC FM katika kipindi cha morning magic,katika kile kipindi cha zaidi ya habari mwandishi Kibwana Dachi ametuambia leo ni siku ya tatu (3) tangu mafuta yaanze kuchimbwa Tanzania.Kwa siku wanachimba mapipa 100 (mia moja).Hii ina maana kwmba tayari watakua wamechimba mapipa mia tatu.
Swali la kujiuliza ni kwamba,mbona hii ishu ipo kimya kimya sana?
Ina maana serikali haijui au wanataka kutuambia kuwa bado jamaa wanafanya utafiti?
jamani hebu tulifuatilie kwa kina hili jambo isije kuwa ndo mtindo ule ule wa wachimba madini.
Nawakilisha.
Labda huyo mwandishi alikuwa hajui ni nini alichoambiwa. Uchimbaji wa mafuta bado upo kwenye hatua za utafiti. Ni kweli kuna baadhi ya maeneo ya Ruvuma basin kumeonyesha dalili za kuwapo mafuta, na ndiko huko ambako utafiti huo unafanyika katika hatua za mwisho mwisho
 
mia mia mia mia mia mia mia. kila kitu mia. Ukweli ni kwamba wanachimba zaidi ya mapipa mia kila siku. kama ikipatikana meli kubwa wanaweza chimba hata zaidi ya pipa 700. ova
 
Waandishi wetu wa habari hawajui chochote zaidi ya historia.hakuna waandishi wanasayansi Tanzania
 
dhahabu inachimbwa
almasi inachimbwa
uranium inachimbwa
mafuta yanachimbwa(ingawa vituoni hawauzi)

hakuna kisichochimbwa, hakuna faida ya uchimbaji maisha yanazidi kuwa magumu!
 
Back
Top Bottom