Leo tarehe 12 Dec, 2010 Rais wa Ghana amefungua Valvu na mafuta yameanza kutiririka kwenda kwenye matanki nchini Ghana kwa mara ya kwanza. Mafuta haya yaligunduliwa miaka 3 iliyopita na inaaminika kuna mapipa kama Bi. 2 na katika miaka miwili ijayo Ghana itakuwa na uwezo wa kutoa mapipa 250,000 kwa siku.
Katika hotuba yake wakati wa ufunguzi, Rais wa Ghana ametahadharisha waghana kuwa wawe waangalifu wasijekuwa kama majirani zao Nigeria na Mafuta. Ikumbukwe kuwa ugunduzi wa mafuta katika nchi ya Angola umepandisha uchumi wake na kuifanye ilipe madeni yake yote na kumwamuru mwakilishi wa Benki ya Dunia kuondoka chini Angola lakini hali si hiyo nchini Nigeria. Uchumi wa Angola na nchi nyingine nyingi za Afrika na dunia kwa ujumla zinazotoa mafuta umenufaika na kupanda kwa bei ya mafuta katika miaka ya karibuni.
Zipo nchi nyingine barani Afrika ambazo mafuta hayajaweza kubadilisha kwa kiasi kikubwa maisha ya wanachi na hapa ndipo swali hili linakuja. Je Ghana itaweza kuinua maisha ya wananchi wake kwa uchimbaji huu wa mafuta?