Mafuta yaanza kutiririka ghana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafuta yaanza kutiririka ghana!

Discussion in 'International Forum' started by kayumba, Dec 16, 2010.

 1. k

  kayumba JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Leo tarehe 12 Dec, 2010 Rais wa Ghana amefungua Valvu na mafuta yameanza kutiririka kwenda kwenye matanki nchini Ghana kwa mara ya kwanza. Mafuta haya yaligunduliwa miaka 3 iliyopita na inaaminika kuna mapipa kama Bi. 2 na katika miaka miwili ijayo Ghana itakuwa na uwezo wa kutoa mapipa 250,000 kwa siku.

  Katika hotuba yake wakati wa ufunguzi, Rais wa Ghana ametahadharisha waghana kuwa wawe waangalifu wasijekuwa kama majirani zao Nigeria na Mafuta. Ikumbukwe kuwa ugunduzi wa mafuta katika nchi ya Angola umepandisha uchumi wake na kuifanye ilipe madeni yake yote na kumwamuru mwakilishi wa Benki ya Dunia kuondoka chini Angola lakini hali si hiyo nchini Nigeria. Uchumi wa Angola na nchi nyingine nyingi za Afrika na dunia kwa ujumla zinazotoa mafuta umenufaika na kupanda kwa bei ya mafuta katika miaka ya karibuni.

  Zipo nchi nyingine barani Afrika ambazo mafuta hayajaweza kubadilisha kwa kiasi kikubwa maisha ya wanachi na hapa ndipo swali hili linakuja. Je Ghana itaweza kuinua maisha ya wananchi wake kwa uchimbaji huu wa mafuta?
   
 2. N

  Nonda JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Waje TZ kujifunza jinsi ya kusimamia na kuendeleza(kugida) rasilimali na maliasili za Taifa. TZ imepiga hatua kubwa katika hili.Tumeweza kuwa na maisha bora kwa kila mtanzania, pia tunajivunia amani na utulivu. Kwa hiyo kukujibu suali lako, ndio mkuu itawezekana kama sisi tulivyoweza.
   
 3. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2010
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,867
  Trophy Points: 280
  Mkuu taratibu, maana naona unaongea wt ful gadhabu.., usijali ni mapito tu ka alivyoimba Bukuku :(
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280

  Nawaombea Mungu mafuta haya yasiwaletee kizaazaa kama kilichokuwepo kule Nigeria. Faida yake itumike katika kuinua viwango vya maisha vya Waghana wote ndani na nje ya nchi. Waganda nao nadhani hawako mbali kuanza kuzalisha mafuta yao.
   
 5. r

  rmb JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Siasa za Ghana ni za kuigwa katika bara letu na mifumo yao ni imara, naamini kuwa haya mafuta yatawanufaisha waghana wote. Huu ni mfano mzuri wa kuigwa hasa na taifa letu katika kusimamia rasilimali adimu ambazo Mungu katujaalia sisi watanzania. Inashangaza na kusikitisha sana kuona rasilimali zetu zinazinufaisha nchi nyingine kwa kutoa ajili na mambo mengine wakati sisi wenye nazo tukiendelea kutaabika!
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Natumaini haya mafuta yatawanufaisha waghana wote kwa ujumla kama ilivyo angola na kuepuka dhahama kama kule nigeria ni jambo la kujivunia kwa waghana wote ingekuwa bongo sijuiingekuwaje maana tanzania nchi ya tatu kwa kutoa madini afrika lakini hakuna maendeleo yoyote yaliyopatikana kupitia madini
   
 7. A

  August JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2010
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,507
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  atta mills ametoa hutuba safi saana sasa sijui ni kwa sababu ya uzalendo au kwa kuwa ni mchumi aliye elemika? nilimsikia kwenye sky news kama wataweka video clip yake nita ipost hapa, sasa ili ya wenzetu na dhahabu ngoja ni niitafutie maneno yanayo faa, tena Mkapa? aliyepata elimu nzuri tu na expose.
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  nitaitafuta hotuba yake nione kama nitaipata
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Wananchi wa Ghana watanufaika; hilo naliamini, hapa kwetu naomba hata wasianze kuchimba katika mfumo huu tulionao sasa!
   
 10. H

  Hute JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,053
  Likes Received: 3,920
  Trophy Points: 280
  sisi mafuta tutagundua lini?hapa bongo? au hatutafuti?
   
 11. r

  rmb JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna kampuni kadhaa zinatafuta mafuta kwenye pwani ya nchi yetu na kuna dalili ya kupatikana so tuvute subira tuone mwisho wake utawaje!
   
 12. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,861
  Likes Received: 2,786
  Trophy Points: 280
  Mungu awabariki! Naamini kwa Ghana wataenda yaani shaka ondoa! Kati ya nchi ambazo tunapaswa kuziangalia kwa jicho la husda ni Ghana wenzetu wamefanikiwa katika nyanja nyingi sana. Angalia wanavyoachiana madaraka ni zaidi hata ya baadhi ya nchi za Magharibi au Kaskazini ukipenda. Rais aliyeko madarakani akipigwa mweleka kwenye uchaguzi anakubali haraka au chama chake kikishindwa anakabidhi madaraka kwa amani na nchi inasonga. Angalia chama cha Jerry Rawlings kilishindwa na John Kuffour waungwana wakakubali yaishe! Jamaa amekaa madarakani kwa vipindi viwili mfululizo naye chama chake kimebwagwa kwenye uchaguzi uliopita na wakakubali kumwachia madaraka Rais wa sasa John Atta Mills bila shida wala hujasikia jitihada za kuchakachua.

  Kwa jinsi nchi hiyo ilivyo na misingi bora ya utawala bora wataweza kusimamia mafuta hayo vizuri na nchi itasonga mbele katika maendeleo. Watuache sisi na Mbayu wayu wetu ambaye kazi yake yeye ni kuruka tu kila siku jana nimemsikia alikuwa Zambia! Yaani maumivu tu kila kukicha. Madini yetu yanasombwa tu yeye anakimbilia Ulaya tu kuponda raha kwa kweli Mungu atusaidie!

  Hivi Watawala wetu hawawezi hata kwenda kujifunza kwa wenzetu hao jinsi wanavyozingatia utawala bora? Yaani Mkwere asingechakachua tungemweka kwenye kumbu kumbu zetu!
   
 13. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #13
  Dec 16, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mungu nusuru tu kama TZ kuna mafuta yasigundulike na kichimbwa wakati huu, mpaka hapo Majangili yatakapoachia nchi hii na kuwa na viongozi waaminifu ambao wanajali maslahi ya nchi hii.
   
 14. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #14
  Dec 16, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,861
  Likes Received: 2,786
  Trophy Points: 280
  Ni kweli Mkuu wako wanatafuta ila juzi wametoa taarifa kuwa kwenye kisima kimoja ambacho kinaitwa PWEZA 1 wamekutana na Gas. Hivyo tuwe wavumilivu tu ingawa kwa upande mwingine unaweza kusema afadhali hata yaspatikane tu maana hawa jamaa watatuibia tu!!!!! Na hivi hatujapata dawa ya kuwachakachua hivyo tutazidi kuwa maskini tu huku akina EL, RA, RK, AC n.k wataendelea kuneemeka tu!
   
 15. bona

  bona JF-Expert Member

  #15
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  the only people who regret to have oil in their back yard are the ''kurds'' in iraq. ghana have very stable democratic process and people seems to enjoy and see there is democracy unlike here where the word democracy does not make sense to most of the people!
   
 16. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #16
  Dec 16, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,453
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Upatikanaji wa mafuta ni laana kwa watawala mbumbumbu kama Chifu Mangungu,ni faraja kwa viongozi walio makini kwa ajili ya nchi yao na wananchi wao.Kwetu bado ni kitendawili,hiyo gesi iliyopatikana haijatumika vizuri kwa maendeleo ya mwananchi.Ni propanganda na ngonjera zisizokwisha.Bora kuyaacha/kuiacha ardhini mpaka hapo utawala bora ,na ufanisi wa hali ya juu,ndipo tutafaidika na mali asili zetu.Ulafi haujengi unabomoa.
   
 17. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #17
  Dec 16, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kuna makampuni zaidi ya manne yanatafuta mafuta apa kwetu ila wakishayagundua lazima watayafyonza mpka mtaji wao urudi na ndipo watatutangazia kuwa wamepata mafuta.
   
 18. r

  rmb JF-Expert Member

  #18
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Mdau hapo napingana na wewe kwa sababu hawa watu watakuwepo tu hawawezi kuondoka, wakifa watawarithisha wengine nadhani mifano mizuri ipo ya watu wenye uchu na uhoro kama wa hao uliowataja! Si rahisi kuwa na watu wasafi 100% tunachotakiwa kukifanya ni kukemea ili wapungue au waache! Hata huko Ghana, rais ni msafi lakini baadhi ya mawaziri wake si wasafi na wengine wanahusishwa na usafirishaji wa madawa ya kulevya. Hawa wachafu tupambane nao tu
   
 19. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #19
  Dec 16, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Dhahabu inachimbwa kila siku na jamaa wanalipa only 3%.
  Mafuta yakipatikana Tanzania mtasikia wachimbaji wanalipa only 0.5%
  Tumerogwa na tumekuwa mazoba hadi inatia aibu. Ujanja wa kuongea tu lakini kichwani watanzania ni ZERO!!
   
 20. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #20
  Dec 16, 2010
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Unaongea kama mnywa kangara.
  Wewe ukishiba makongoro na utumbo huko kilabuni, kwa ujumla unachukulia kwamba hata mkeo na wanao nyumbani nao wameshiba.
  Ukipungukiwa hata hujiju.
  Waghana waje kujifunza kwetu WaTz kusimamia rasilimali??
  Uliona wapi mtu anajinoa kimasumbwi kwa kumuonja japs mgonjwa alolala pale Mwaisela?
   
Loading...