Haya mafuta Asili yake ni kwetu huko Kigoma
Haya kwa watu wa Kigoma tunayaita Mafuta ya Mise.
Maana kwa lugha uliyotumia hapo juu ukikutana na mtu wa Kigoma lazima akuulize mawese au.
Maana mbegu za Chikichi zinaitwa MISE na mafuta yake ni Mafuta ya Mise.
Nenda Pale magomeni yapo telee.
Kuna Jamaa wa Kigoma wanaduka Kubwa sana la bidhaa zote za kule,Mawezse ,Dagaa wa bichi na wakavu,Samaki wabichi aina ya Migebuka na wakavu pia,maana jamaa wamejipanga kweli,we samaki mbichi wa Kigoma unamla Dar.Na Pia hayo Mafuta ya Mise na mawase yapo..
Ngoja nitakuulizia Jina la mtaa na maeneo waliyopo,maana mie nipo Zanzibar ila asili yangu ni Kigoma na huwa naagiza kwa mdogo wangu ndio anaenda kunichukulia.